DKT.BASHIRU “MKUU WA MKOA ATAKAYESHINDWA KUSIMAMIA HAKI ZA BODABODA NA MACHINGA HANA KAZI”

Na Allawi Kaboyo-Bukoba. Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha Mapinduzi  CCM Daktari Bashiru Ally Kakurwa, amewataka watendaji wa Serikali hususani wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya nchini,  kuwa wazalendo na kufanya kazi kwa haki wakati wa kuwatumikia Wananchi wao pasipo kulegalega. Kauli hiyo ameitoa desemba 22 mwaka huu alipokuwa akizungumza na wananchama wa chama hicho waliojitokeza kumlaki alipowasili mkoani Kagera na kumtolea mfano Mkuu wa Mkoa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Elisha Gaguti kwa Nidhamu, Uzalendo, Ujasiri na Uchapakazi wake uliotukuka aliouonyesha kwa Kipindi Kifupi toka Ameteuliwa. “Niwaombe wananchi wa mkoa wa…

Soma Zaidi >>

SALUM MWALIM:OLENASHA ALIOMBE RADHI TAIFA.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Zanzibar Salum Mwalimu amemtaka naibu waziri wa elimu William Olenasha kujitokeza na kuliomba taifa radhi kutokana na kauli yake ya kuwa mawaziri hawaendi kwenye majimbo ya wapinzani(wahuni) Mwalimu ameyasema hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho mjini Njombe. “Juzi nimeona naibu waziri mmoja bila aibu anazungumza mambo ya ajabu eti pale nilikuwa siji mlikuwa mnanialika kwasababu mbunge wenu hapa alikuwa ni CHADEMA,Olenasha atoke aliombe taifa radhi unaibu waziri sio wakwake wala sio wa baba yake ni wa watanzania…

Soma Zaidi >>

CHADEMA YAIONDOA MAHAKAMANI KESI YA UCHAGUZI

Dar es salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo( CHADEMA) kimeiondoa mahakamani kesi ya uchaguzi namba 5/2018 iliyofunguliwa Mahakama kuu kanda ya Tanga ya kupinga uchaguzi wa marudio jimbo la Korogwe vijijini. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa idara ya habari na mawasiliano CHADEMA,Tumaini Makene,imesema wameiondoa kesi hiyo baada ya kufanya uchambuzi wa kina ukihususha ushauri wa kitaalam kutoka kwa mwanasheria wa chama hicho. Katika kesi hiyo iliyokuwa ianze kutajwa Desemba 10, mwaka huu, aliyekuwa mgombea wa CHADEMA,ndugu Aminata Saguti alikuwa akilalamikia mchakato ulivyoendeshwa kwa kukiuka taratibu za…

Soma Zaidi >>

CCM WILAYA YA ILALA YAPIGA MARUFUKU WATANGAZA NIA NAFASI ZA UDIWANI

Na Heri Shaban, Dar es salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ilala, kimewapiga marufuku watangaza nia katika nafasi za udiwani kata ya Tabata, badala yake wametakiwa kujenga chama. Hayo yamesemwa jana Desemba 05, 2018 na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilala, Ndg Ubaya Chuma, wakati wa kikao cha mkutano mkuu wa chama (CCM) hicho, Tabata Mtambani jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mwenezi wa chama hicho ngazi ya taifa Ndugu Humphrey Polepole. “Napiga marufuku waliotangaza nia katika nafasi za udiwani kata ya Tabata, waache tutawachukulia hatua, badala…

Soma Zaidi >>

NAPE: CCM IMEVAMIWA NA WASAKA TONGE

Na Bakari Chijumba,Mtwara Wakati sakata la Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Dr.Bashiru Ally na kada wa Chama hicho, Bernard Membe likiendelea kuchukua nafasi kubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii, mbunge wa Mtama Nape Nnauye ameibuka na kusema CCM imevamiwa na wasaka Tonge wenye maslahi na matumbo yao kuliko chama. Nape Nnauye ambaye ni mbuge wa Mtama, ametoa kauli hiyo baada ya kuenea kwa taarifa kuhusu madai ya kuanzishwa kwa chama kipya kitakachoitwa USAWA, ambapo Bernard Membe na Nape Nnauye wametajwa kuwa miongoni mwa watakaotimkia kwenye chama hicho kipya. Taarifa…

Soma Zaidi >>

DC GODFREY NGUPULA “HAKUNA MVUTANO HALISI KATI YA MEMBE NA DKT BASHIRU

Tabora Mkuu wa wilaya ya Nzega na mjumbe wa kamati ya Siasa ya wilaya hiyo Mheshimiwa Godfrey Ngupula amesema kuwa kwa siku kadhaa sasa kila kona ni habari ya mvutano kati ya Membe na Dkt. Bashiru. Na haswa mvutano huu unavyoongezwa chumvi na pilipili katika magazeti na mitandao ya kijamii. Nilikuwepo Nzega wakati Dr. Bashiru anatoa ufafanuzi wa kilichotokea,namnukuu “Mimi kwanza nilipoyatamka yale Geita katika maongezi yangu wala sikuwa namaanisha kumuita Membe, utaratibu wa kuitana kichama naujua na unajulikana. “ikitaka kumuita basi nitafanya hivyo kwa barua au kwa simu lakini,…

Soma Zaidi >>

KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU NCHINI DRC ZAPAMBA MOTO, HALI NI PATASHIKA

Kinshasa, DRC. Kampeni za uchaguzi zinaendelea kushika kasi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23. Mgombea wa chama tawala, Bw Emmanuel Ramazani Shadary, anatarajia kujielekeza magharibi mwa nchi hiyo baada ya kufanya kampeni zake mashariki mwa nchi hiyo, huku upinzani nao ukipanga kuanza kampeni zake mashariki mwa nchi Aidha, wagombea wengi wa kiti cha urais wanaendelea kujiuzulu na kuwaunga mkono wagombea wa upinzani Felix Tchisekedi na Martin Fayulu. Jean Philibert Mabaya mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya chama…

Soma Zaidi >>

GWAJIMA AMPONGEZA LOWASA, AMPA NENO ZITO MH. RAIS MAGUFULI

Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ndugu  Methusela Gwajima, amemuomba Waziri mkuu wa zamani na mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia  na Maendeleo (CHADEMA ) Edward Lowasa, kufanyia kazi ushauri aliopewa na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ufunguzi wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Gwajima  ambaye pia ni Mwanasheria kitaaluma, amesema Kitendo cha Lowasa, kuhudhuria na kuungana na serikali katika miradi ya maendeleo ni cha kuigwa na wapinzani wengine. “Kitendo hicho kina onyesha kuwa Lowasa amekomaa kisiasa,…

Soma Zaidi >>

KILICHOSABABISHA RAIS TRUMP KUFUTA MKUTANO WAKE NA VLADIMIR PUTIN

New York, MAREKANI. Kabla ya kuanza kwa mkutano wa kundi la nchi 20 (G20) ulioanza leo mjini Buenos Aires, huko nchini Argentina, Rais wa Marekani, Donald Trump, alifuta ghalfa mkutano wake uliopangwa kufanyika hapo kesho Jumamosi, Desemba mosi na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin. Katika Ukurasa wake wa Twitter Donald Trump alishtumu Vladimir Putin kwa kutowaachilia huru askari wa kikosi cha wanamaji wa Ukraine na meli zao zilizokamatwa karibu na bahari ya Azov. Hatua hiyo inakuja tu siku chache baada ya kufichuliwa taarifa mpya nchini Marekani katika uchunguzi kuhusu madai ya…

Soma Zaidi >>

ESTHER BULAYA : SERIKALI INADAIWA DENI LA TRILIONI NANE

  Waziri Kivuli,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Walemavu Esther Bulaya amesema serikali inadaiwa deni la trilioni nane na mifuko ya hifadhi za jamii nchini jambo ambalo linatishia uhai wa mifuko hiyo. Bulaya amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari juu ya msimamo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) juu kupinga sheria mpya ya mafao ya hifadhi ya jamii na kusema serikali imekopa fedha zaidi ya shilingi trilioni nane kwenye mfuko huo na kuziwekeza kwenye miradi isiyo na tija. “Kwa mujibu wa Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali…

Soma Zaidi >>