TUNDU LISSU:HAKUNA MJOMBA AU SHANGAZI WA KUMLILIA, NI KUELEKEA MARUDIO YA CHAGUZI NDOGO-BUYUNGU

UBELGIJI.  Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida, Mheshimiwa Tundu Lissu, amesema kuelekea marudio ya chaguzi ndogo zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni ni fursa nyingine ya mlengo upinzani kuanika wazi utawala wa Rais Magufuli na hatua nyingine ya kupigania haki za Binadamu, utawala bora na demokrasia nchini Tanzania. Mh Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni(KUB), ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Julai 16 akiwa nchini Ubelgiji, anapoendelea kupokea matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi 38 hapo Septemba mwaka jana akiwa nyumbani…

Soma Zaidi >>

MATUKIO KUELEKEA UCHAGUZI MDOGO WA MARUDIO AGOSTI 12, GODBLESS LEMA ALALAMA

Zikiwa zimesalia takribani siku 28 kuelekea kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa marudio kote nchini, Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA) Godbless Lema, ameibuka na kulalamikia baadhi ya matukio yasiyokuwa yakiungwana ambayo yamekuwa yakiendelea katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Akiandika katika ukurasa wake wa Twitter, Mbunge Lema ameilalamikia CCM na Ofisi ya Msimamizi Msaidizi katika kata ya Terrat, kushiriki katika kufanya vitendo vya hujuma dhidi ya mgombea wa CHADEMA katika kata hiyo ndugu Raymond Laizer. Lema amesema kikundi cha ulinzi CCM ‘green guard’ walishiriki kumpora fomu ndugu Raymond Laizer akiwa kwenye ofisi…

Soma Zaidi >>

CCM YAIMALIZA NCCR-MAGEUZI, MAKAMU MWENYEKITI ATIMKIA CCM

Siku ya leo Julai 13, 2018 chama cha NCCR-Mageuzi kimepata pigo mara baada ya aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho kwa upande wa Bara, Leticia Mosore, kutangaza kubwaga manyanga na kujiunga na CCM. Leticia ametangaza uamuzi huo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na wanahabari, ambapo ametaja moja ya sababu za yeye kujiunga na CCM ni kukerwa kwake na tabia ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini, ikiwemo NCCR-Mageuzi kupinga kila kitu kinachofanywa na serikali. “Kinachonikera kwenye upinzani ni kupinga kila kitu hadi mazuri wakati hayo ndio tulikua tunayasema, mpaka…

Soma Zaidi >>

RAIS SALVA KIIR WA SUDAN KUSINI AONGEZEWA MUDA KUBAKIA MADARAKANI

JUBA. Nchini Sudan Kusini Bunge la nchi hiyo, limepiga kura kurefusha muda wa Rais Salva Kiir kubakia madarakani kwa miaka mitatu zaidi hadi mwaka 2021, hatua ambayo bila shaka huenda ikatatiza juhudi za kuleta amani katika nchi hiyo changa duniani kwa kudhoofisha mazungumzo ya amani na makundi ya upinzani. Bwana Kiir amekuwa madarakani tangu Sudan Kusini ipate uhuru wake mwaka 2011 na uchaguzi wa mwaka 2015 nao ulihairishwa. Makundi ya upinzani nchini humo hivi karibuni katika siku za nyuma yalishutumu hatua kama hiyo kuwa inakwenda kinyume na sheria. “Mswada wa mabadiliko…

Soma Zaidi >>

‘TUMETEKELEZA AHADI KWENYE KATA ZINAZOONGOZWA NA CHAMA CHETU’, ACT WAZALENDO.

Mapema siku ya leo Julai 11, 2018, chama cha ACT Wazalendo kimetoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi ilizozitoa katika kata zinazoongozwa na chama hicho, wakati wa ziara maalumu ya kutembelea kata hizo kati ya tarehe 19 Februari hadi tarehe 9 Machi mwaka huu. Akitoa taarifa ya utekelezaji wa ahadi hizo kwenye ofisi za makau makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Katibu Bunge na Serikali za Mitaa, ACT Wazalendo, mama Janeth Rithe amesema kuwa mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo, chama kilianzisha harambee kwa wanachama na viongozi kwa ujumla…

Soma Zaidi >>

RIEK MACHAR MBIONI KUREJESHEWA WADHIFA WAKE

Kiongozi wa kisiasa maarufu nchini Sudan Kusini na aliyekuwa Makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Riek Machar, atarejeshwa katika wadhifa wake kama sehemu ya makubaliano ya amani ya kuvifikisha mwisho vita vya karibu miaka mitano ambavyo vimewaua maelfu ya watu na kuliharibu kabisa taifa hilo changa barani Afrika. Makubaliano hayo yaliafikiwa katika mazungumzo ya mjini Entebbe, na yalisimamiwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na kuhudhuriwa na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Sudan Omar al-Bashir na Machar. Taarifa ya ofisi ya rais ya Sudan Kusini…

Soma Zaidi >>

Tundu Lissu atoa ujumbe mzito kuhusu afya yake

Kupitia ukurasa wake wa mtandao, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye anapatiwa matibabu nchini Ubeligiji aliandika; “Wapendwa wangu natumaini wote hamjambo asubuhi hii (angalau kwangu ni saa 12 kasoro ya asubuhi). Nawaomba msamaha kwa kuwaweka roho juu jana halafu sikuonekana. Nilipata wageni na by the time nimemalizana nao muda ulishaenda sana. Naomba nianze kwa kuwapa briefing ya afya yangu. Wengi wenu mtakuwa mmeona video clips nikifanya mazoezi ya kutembea. Clip hizo zinaonyesha naendelea vizuri na ni kweli. Operesheni ya mwezi uliopita imepona, angalau kwenye muscles. Mfupa bado una kazi…

Soma Zaidi >>

“MSIIJIBU SERIKALI”, UKAWA YAWAAMBIA MAASKOFU.

Kufuatia Serikali kuiandikia barua kanisa la KKKT na Baraza la Maaskofu la Katoliki (TEC) ambapo pamoja na masuala mengine iliwataka kufuta waraka walizozitoa  ndani ya siku kumi tangu tarehe ya kupokea kwa barua hizo kwa kile kilichoelezwa kuwa zinaweza kuzusha hisia tofauti tofauti. Leo hii tarehe 7/06/2018 kambi rasmi ya upinzani Bungeni imezitaka taasisi hizo za kidini kutokuijibu serikali kwani serikali inafanya udhalilishaji  kwa waumini wa dini hizo na hali hiyo imeleta sintofahamu kwa waumini wa dini hizo. Mwenyekiti mwenza wa UKAWA na Mbunge wa jimbo   la Vunjo Mh. James…

Soma Zaidi >>

HII HAPA TAARIFA YA CUF KWA VYOMBO VYA HABARI, WALIOKWAPUA FEDHA ZA RUZUKU KIKAANGONI.

TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI WALIOIBA FEDHA ZA RUZUKU CUF WAJIANDAE KUJIBU MASHTAKA MAHAKAMANI: Imetolewa Leo Tarehe 7 June, 2018 1. THE CIVIC UNITED FRONT [CUF-Chama Cha Wananchi] Kinaungana na Watanzania wote kuwapongeza wabunge wake, wakiongozwa na Mhe. Mohamed Juma Khatib Mbunge wa Jimbo la Chonga, kwa kutekeleza wajibu wao vizuri na kuibua UFISADI WA FEDHA ZA UMMA unaofanywa na matapeli wa kisiasa, vibaraka na wasaliti ndani ya CUF kwa njia ya Ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa nchini. 2. Katika kikao cha bunge Tarehe 5/6/2018, wakati…

Soma Zaidi >>