JESHI LA MAGEREZA:TUNAWAPA UJUZI WAFUNGWA ILI WAKITOKA WAACHE UHALIFU

Inaelezwa kuwa ni muhimu wafungwa  kujifunza shughuli za Ujasiliamali wanapokuwa wanatumikia kifungo Gerezani kwakuwa zitawasaidia kujitegemea pindi watakaporejea uraiani. Hayo yalielezwa na Mrakibu wa Jeshi la Magereza kutoka makao makuu ya Jeshi hilo Dar es Salaam  Dedan Biralo,wakati wa Maonyesho ya viwanda vidogo SIDO yanayofanyika Kitaifa viwanja vya Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu. Akizungumza na Waandishi wa habari waliotembelea banda la maonyesho ya bidhaa za Magareza Biralo alisema kuwa moja ya kazi ya Magereza ni kutoa ujuzi kwa wafungwa ili wakitoka waache uhalifu lakini pia kuwajengea uwezo wa kutengeneza…

Soma Zaidi >>

Serikali kuwashughulikia wazazi ambao watoto wao watakeketwa

Ni msimu wa ukeketaji kwa wasichana na Tohara kwa Wavulana ukiwa umeanza wilayani Tarime, Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema itawakamata na Kuwafikisha mahakamani Wazazi ambao watoto wao wakike watakeketwa. Hayo yameelezwa hivi karibuni na Mkurugenzi msaidizi kutoka Idara ya Maendeleo ya Jamii  kitengo cha malezi na Familia,Grace Mwangwa alipokuwa akitoa tamko la Serikali kwenye mkutano wa kujadili namna ya kukomesha ukeketaji ulioandaliwa na shirika la Utu wa Mtoto CDF uliofanyika ukumbi wa Blue Sky mjini Tarime. Mwangwa anasema kuwa kitendo cha kuwakamata Mangariba pekee hakiwezi…

Soma Zaidi >>

UMUHIMU WA ASALI KAMA DAWA YA MAFUA.

ASALI NI NINI? Asali ni chakula kitamu katika hali kiowevu kinachotengenezwa na nyuki. Nyuki hula mbelewele pamoja na maji matamu ndani ya maua na kuitoa tena katika mzinga wa nyuki kwa kuitunza kwenye sega. Ndani ya sega kiowevu huiva kuwa asali kamili. Asali inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka maradufu kama itachanganywa na mdalasini.…

Soma Zaidi >>

KUNA HAJA YA MITIHANI YA TAIFA KUTOFAUTIANA KATI YA SHULE ZA MJINI NA VIJIJINI..

NA MWL.MGALA R.B 0715079380,0675967150 mgalaramadhan@gmail.com Leo nimeona kwa kifupi sana kuwashirikisha sehemu ya tafiti zangu binafsi juu ya Elimu yetu,nikianza na Elimu ya msingi ikiwa ni utafiti nilio ufanya siku 180 kabla ya mtihani wa taifa wa kuhitimu elimu ya msingi uliofanyika tar 5&6 sep 2018. Katika utafiti wangu niligundua changamoto zilizopo katika sekta ya elimu zinafananafanana na zile zinazozikabili sekta zingine,Changamoto yeboyebo kama uhaba wa watumishi,Nyumba za walimu,Maslahi Zimetawala katika maeneo mengi ingawa juhudi za Serekali katika kuzitafutia ufumbuzi ni kubwa. Ukiachiliambali changamoto hizo,Elimu katika sehemu za vijijini imegubikwa…

Soma Zaidi >>

ZIFAHAMU FAIDA ZA KITUNGUU SWAUMU

Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba. Kitunguu swaumu kimetajwa kwenye vitabu mbalimbali vya dini vikielezea faida zake katika kutibu maradhi mbalimbali yasababishwayo na bakteria, matatizo katika mapafu, matatizo katika mfumo wa umen’genyaji chakula, na matatizo ya kuishiwa nguvu. Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi…

Soma Zaidi >>

FAHAMU UMUHIMU WA TANGAWIZI KATIKA MWILI WA BINADAMU.

  Tangawizi ni nini? Tangawizi ni kiungo ambacho kinatokana na mizizi ya mmea wa Tangawizi. Mmea huu unafanana sana na Binzari ikiwa bado haijamenywa maganda yake. Pia  bidhaa hii inapatikana nchi nzima kwa bei nafuu kabisa na kila mtu mwenye uwezo wowote wa kiuchumi anaweza kununua aidha kwa kipande kimoja, fungu au kwa kilo pia. Zifahamu faida/umuhimu wa Tangawizi. Husaidia kupunguza kama si kuondoa kichefuchefu ni nzuri haswa kwa wale wanawake wenye mimba changa ambao husumbuliwa kutapika. Husaidia wale wenye matatizo ya gauti yaani sehemu ya viungo kuuma na kusikia…

Soma Zaidi >>

GENERAL LAURENT NKUNDABATWARE MIHIGO NA HARAKATI ZA KIJESHI CONGO.

Na Mpoki Buyarapah Kaminah Mwandagasya. General Laurent Nkundabatware Mihigo ni moja ya watu wenye historia tata na ngumu,amefanya mengi na mazito akiwa katika ubora wake, namuingiza katika listi ya vizazi vya chuma vilivyowahi kuwepo Afrika,namchukilia kama udongo wa zamani udongo mgumu usiokubali jembe la mkono,akiwa katika umri mdogo sana miaka ya 1994-1998 alitoka congo na kwemda kumsaidia POUL KAGAME katika vita kati ya TUTS (Watutsi) na HUTU (Wahutu) uko RWANDA,Miaka ya 1998 baada vita kuisha  na RWANDA kuwa chini ya TUTS General LAURENT NKUNDABATWARE alirudi CONGO Kuendeleza mapambano ya kijeshi…

Soma Zaidi >>

YAFAHAMU MAISHA YA MTATA HUGO CHAVEZ; MJAMAA HASWA, MUUZA UNGA, MGONJWA WA TOTOZI.

Hugo Chavez ni shujaa wa itikadi ya Ujamaa mpaka kifo kilipomchukua Machi 5, 2013. Watu wenye imani isiyoyumba ya falsafa zote za Mrengo wa Kushoto (Left-Wing), kwao Chavez alikuwa jemedari kinara dhidi ya Ubepari.Chavez aliuchukia ubepari na aliijenga Venezuela kuwa taifa la Kijamaa kupitia vyama vya Movement for the Fifth Republic kati ya mwaka 1997 mpaka 2007 kisha United Socialist Party kuanzia mwaka 2007 hadi roho yake ilipotengana na mwili wake. Hata sasa, mwili wake ukiwa umepumzishwa kwenye makaburi ya Cuartel de la Montana, yaliyopo Caracas, Venezuala. Chavez anakumbukwa kama…

Soma Zaidi >>

HEBU WATANZANIA TUTAFAKARI KWA KINA NA KUKIHURUMIA KIZAZI CHETU KIJACHO

Na.  Japhet Matarra Kuna watu wengi sana siku hizi za rafu za kuhama vyama vya siasa kutoka upinzani kwenda chama tawala (CCM), Wamekuwa wakifurahia sana. Lakini WENGI Hamjui madhara yake licha ya gharama za Uchaguzi katika marudio, eti mnatamani nchi yetu iwe chini ya chama kimoja. MPO SERIOUS KWELI..?? Hebu Vuta Picha kwa mfano, Vyama vyote vikafutwa katika kipindi hiki kikabaki CCM tu chama Ulichonacho wewe unayefurahia sasa hivi. Baadae hao uliokua Unawaona hawafai akina Mbowe, Mdee, Heche, Nassary, Lema, Bulaya, Zitto, n.k, wakaona ni Ujinga Kufa Unatetea watu wasiojua…

Soma Zaidi >>

WANATAKA KUABUDIWA WANASAHAU KWAMBA BINADAMU HAWEZI KUWA MUNGU, RODRIGO DUTERTE AMECHELEWA KUFUATA NYAYO ZA MBABE NAPOLEON BONAPARTE.

Toleo la II. Vituko vya Rodrigo Roa Duterte mapema sana tarehe 10/6/2018 akiwa yupo Korea ya Kusini akiwahutubiaa wafilipino waishio Korea Kusini alifanya jambo ambalo liliwashangaza wengi sana duniani kotoe, Rodrigo Roa Durtete amewahi kushutumiwa na mashirika yanayotetea haki za binadamu katika kuwanyanyasa na jinsi anavyo wachukuliaa wanawake huko Ufilipino, akiwa Korea Kusini alimwita msichana mmoja wa kifilipino na kumwambia amkumbatie na baadae kumshawishi ampige busu la mdomoni mbele ya umati wa watu bila kujali alikuwa mke wa mtu au lah, lakini mwanamke yule akawa anasita sita na baadae akakubali…

Soma Zaidi >>