KUCHAGULIWA KWA KEISHA SOMO NYETI KWA WASANII WANASIASA

  Na. Dady Igogo. Kumekua na wimbi la wasanii kuingia kwenye siasa. Baadhi yao wamekua wakidhani kuwa maumbile yao, uzuri wao, mwili wao au umaarufu wao unaweza kuwafanya wakafanikiwa kwenye malengo yao ya kisiasa. Wapo pengine waliofanikiwa kwa hayo lakini yamekua ni mafanikio ya muda mfupi. Msanii Keisha aliwahi kugombea ubunge wa viti maalum kundi la walemavu mkoa wa Dodoma na kushinda tarehe 26/07/2015. Lakini hakufanikiwa kwenye kundi la Taifa. Ni dhahiri kuwa ukiangalia post zake, picha zake na namna alivyo na heshima utagundua kuwa kuchaguliwa huko siyo tu kwamba…

Soma Zaidi >>

FAHAMU KUHUSU UBAGUZI WA RANGI NCHINI MAREKANI.

Maandiko matakatifu ya dini zote yanasisitiza kwamba Mungu ni mmoja na yeye ndiye baba yetu sote tuliowanadamu na jinsi vile tulivyo ni kwa mapenzi yake Mola na sifa za uumbaji wake. Hili ni suala ambalo kila mmoja analifahamu na kulikiri katika imani yake. Hakuna asiyefahamu ya kwamba binadamu sisi tumeumbwa katika muundo wa aina moja lakini kimuonekano tuko tofauti. Sifaa kuu za sisi wanadamu kwanza kabisa uhai wetu unaambatana na upumuaji, zoezi hilo likiisha basi sifa ya kuwa binadamu hupotea na kuwa maiti. Lakini pia binadamu sisi sote tuna kichwa,…

Soma Zaidi >>

LEO NI SIKU YA MATEKA WA KIPALESTINA, 17 APRIL

April 17 kila mwaka inakwenda sambamba na Siku ya Mateka wa Kipalestina, ambapo zaidi ya mateka elfu sita (6,000) wa kipalestina wapo katika magereza ya kivamizi ya Israeli. Taasisi inayoshughulikia mambo ya mateka ya kipalestina,imetilia mkazo  ya kwamba historia ya harakati za mateka wa kipalestina,zimeanza mwanzoni mwa uvamizi wa Israeli katika ardhi ya Palesttina mnamo mwaka 1948 na kwamba utawala huo wa kivamizi wa Israeli umeifanya hatua ya kuwakamata watu ndio sera,njia na chombo cha kuwakandamiza na kuwadhibiti wananchi wa Palestina,pia kueneza woga na hofu kwa wapalestina hao.Hali iliyopelekea ukamataji…

Soma Zaidi >>

ATAKAYE JARIBU KUHARIBU AMANI YETU NI HERI ATANGULIE AKATUANDALIE MAKAZI YA MILELE.

Leo ninawaletea makala fupi yenye lengo la kukufahamisha wewe Mtanzania namna mbinu chafu za Wamagharibi( Marekani & Ulaya) zinavyotumika katika nchi nyingi za Afrika, Latini Amerika na Asia kuangusha Utawala uendao kinyume na matakwa yao. Nchi za Marekani na Ulaya kwa asili yao ni nchi za Kibepari na msingi mkuu wa Ubepari ni unyonyaji katika kile kiitwacho mwenye nguvu na apate ( Suvival for the Fittest ). Kutokana na msingi huo mkuu wa Ubepari Mataifa haya hufanya kila mbinu kuhakikisha Nchi za Afrika, Asia na Latini Amerika kuwa na viongozi…

Soma Zaidi >>

LEO KATIKA KUMBUKUMBU YA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE

Tarehe kama ya Leo 12/04/1984 Taifa lilimpoteza kiongozi wake shupavu, aliyekuwa Waziri Mkuu Hayati Edward Moringe Sokoine, kufuatia ajali ya gari eneo la WAMI-DAKAWA Kilomita 35 nje kidogo ya mji wa Morogoro. Waziri Mkuu huyu alikuwa akitokea Dodoma kuelekea Dar es Salaam baada ya kufunga Kikao cha Bunge mjini Dodoma. Baada ya kuagwa kiserikali Jijini Dar, marehemu Sokoine alisafirishwa kwenda Monduli Juu Arusha kwa mazishi. Atakumbukwa kama kiongozi shupavu na ambaye alikuwa hacheleweshi utekelezaji wa jambo pale linapoonekana linatakiwa utekelezaji wa haraka na madhubuti. Alipigana kupunguza rushwa na ufujaji wa…

Soma Zaidi >>

ZIFAHAMU FAIDA ZA MATUMIZI BORA YA ASALI, MDALASINI

Katika maisha yetu ya kila siku huwa tuna tumia asali na Mdalasini kama moja ya kichocheo (kiongeza radha) katika kitu tunachotumia, ila ukweli ni kwamba Asali na mdalasini husaidia sana kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba. Uchunguzi wa kisayansi na kitabibu umebaini kuwa kuna dazani za umuhimu wa asali na mdalasini katika kujenga afya bora. Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa…

Soma Zaidi >>

BOTSWANA:KUTANA NA BINTI BOGOLO KENEWENDO,WAZIRI KIJANA MWENYE UMRI MDOGO.

GABORONE. Mheshimiwa waziri Bogolo Kenewendo amekuwa akizungumziwa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii sio tu kwa sababu ni waziri bali, waziri kijana mwenye umri mdogo zaidi kuliko mawaziri wengine katika bunge la nchini Botswana. Kenewendo kwa mara ya kwanza alijiunga na siasa mwaka 2016 juzi tu, kama mbunge wa bunge la nchi hiyo, baada ya kuchaguliwa na rais wa zamani Ian Khama, na sasa ni waziri wa uwekezaji, biashara na viwanda nchini humo. Kuchaguliwa kwake kumekuwa ngekewa kwa jinsi alivyopokelewa kwa sifa na pongezi nyingi sana, hii…

Soma Zaidi >>

MTOTO WA RAIS KUWA RAIS WA CHAMA CHA MAWAKILI TANGANYIKA ?

Na Nizzoh Afrika. Licha ya kuwa ni mjukuu wa mwanamapinduzi wa Zanzibar ambae pia ni Rais wa kwanza wa Zanzibar na muasisi wa Muungano uliozaa Tanzania ya leo Mzee Abeid Aman Karume, Bint mfalme huyu Bi. Fatma Aman Abeid Karume mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar amekuwa mkosoaji na mpingaji mkubwa wa anachokiita uonevu na ukandamizwaji wa haki za kiraia unaofanywa na serikali ya chama tawala Chama cha Baba yake mzazi (CCM), huku akiwa tayari na shauri la Kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania dhidi ya Serikali ya Dr. John…

Soma Zaidi >>

MAKALA: SABABU TATU ZA CHINA KUDHIBITI MITANDAO YA KIJAMII NA SOMO LA KUJIFUNZA TANZANIA

Anaandika ndugu Daniel Sarungi, Information Security Expert (ISO). Tovuti ambazo zimedhibitiwa nchini china. Kabla hatujaanza, embu tuangazie tovuti zipi ambazo zimedhibitiwa vikali nchini China: Google, Blogger, Flickr, MySpace, YouTube, Plurk, Wikipedia, HotMail, MSN, Live Search, Bing, Twitter, Facebook, Instagram, Snapchat n.k Tuvoti tajwa hapo juu na zingine nyingi hazifanyi Kazi katika nchi ya China. Napenda twende hatua kwa hatua ili tukimaliza uone ni kwa jinsi gani Tanzania tunaweza kufaidika na mfumo kama huo wa China. Zifuatazo ni sababu Tatu zilizopelekea nchi ya China kudhibiti mitandao ya kijamii na tuvoti nyingi…

Soma Zaidi >>

ZITTO KABWE: UKOSEFU WA MAJI UNAVYOTIA UMASKINI WATANZANIA.

Anaandika Mhe. Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini, na kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo. Changamoto ya Maji na Umaskini kwa Watanzania. Changamoto ya Maji inachangia sana kuwashikilia watu wa vijijini kwenye dimbwi la umasikini na kuongeza tofauti ya kipato Kati ya mijini na vijijini na kati ya wenye nacho na wasio nacho. Gharama za maji ni kubwa mno maeneo ya vijijini kiasi kwamba zinazidi wastani wa pato la mtu mmoja ( per capital income) kwa siku nchini Tanzania. “Pato la Taifa mwaka 2016 lilikuwa shilingi milioni 103,744,606 kwa bei…

Soma Zaidi >>