Dodoma. Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu imesaini mikataba na makampuni ya vijana yatakayoanza kujenga na kutoa mafunzo ya kilimo kupitia kitalu nyumba (Green House). Hafla hiyo ya utiaji saini mikataba hiyo ilifanyika Novemba 27, 2018 katika ofisi hiyo iliyopo jijini Dodoma. Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Bw. Peter Kalonga alisema kuwa serikali imetoa fursa kwa vijana kupata mafunzo ya kilimo cha kisasa kupitia mradi huo utakao wawezesha kiuchumi na kuwaletea maendeleo katika jamii. “Malengo mahususi…
Soma Zaidi >>Category: KILIMO NA UFUGAJI
NAIBU WAZIRI STELLA MANYANYA AIPONGEZA ANSAF KWA KUCHOCHEA MAENDELEO YA KILIMO NA VIWANDA
Dar es salaam. Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Eng Stella Manyanya, amesema, endapo kutakua na ustawi wa sekta ya viwanda na kilimo nchini Tanzania, kutaokoa dola za kimarekani millioni 420 kila mwaka ambazo hutumika kuagiza chakula nje ya nchi. Kauli hiyo ameitoa mapema leo jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa wadau wa kilimo na viwanda ulioandaliwa na jukwaa huru la wadau wa kilimo lisilo la kiserikali (ANSAF ) ambao umefadhaliwa na SDC, Irish Aid na UKAID kupitia KPMG. Amesema, Tanzania imekuwa ikiagiza maziwa, ngano, kuku na…
Soma Zaidi >>KAMPUNI YA RUAHA FARM NI MKOMBOZI WA WAFUGAJI NYUKI IRINGA
KAMPUNI ya uchakataji wa asili ya Ruaha farm mkoani Iringa kupitia asali yake Ruaha Honey imeanza kuwaokoa kiuchumi wafugaji wa nyuki mkoani Iringa kwa kutoa mizinga na kuwaunganisha na soko la asali . “kampuni ya Ruaha Farm imekuja kivingine baada ya kufunga mashine za kisasa za kuchakata asali yenye ubora pasipo kutumia vifaa vya kienyeji kama moshi na vingine “ Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Ruaha Honey Fuad Abri alisema kuwa kampuni yake imeendelea kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Magufuli ya Tanzania ya viwanda . Alisema ubora wa asali ya kampuni ya Ruaha Honey ni tofauti na asali nyingine zinazouzwa mitaani kwani sifa kubwa ya asali ya Ruaha honey ni asali halisi toka katika vijiji vinavyozunga hifadhi ya Ruaha national park. Asali ya ruaha honey ni Asali bora inayozingatia usafi wa vyombo, usafi…
Soma Zaidi >>DC HOMERA AAGIZA KUPITIWA UPYA DAFTARI LA WAKULIMA WA KOROSHO
Tunduru. Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Juma Homera ameagiza wataalamu wa kilimo, Maafisa ushirika, viongozi wa AMCOS Watendaji wa vijiji na Kata pamoja na maafisa Tarafa kupitia upya orodha ya wakulima wa korosho kwenye AMCOS na Katika vijiji mbalimbali. Agizo hilo alilitoa October 4 mwaka huu katika kikao cha kazi kilichoitishwa na Bodi ya korosho Tanzania CBT, Kilichofanyika mkoani Mtwara kufuatia kuwepo kwa dalili za majina hewa katika madaftari ya wakulima wa korosho. Aidha DC Homera amesema kuna baadhi ya wananchi na viongozi wa vijiji wamejiorodhesha majina yao kama wakulima…
Soma Zaidi >>MADALALI WA KOROSHO KWA WAKULIMA WAPIGWA MARUFUKU MTWARA
Na Omary Hussein,Mtwara. Serikali wilayani Mtwara imewatahadharisha madalali wenye tabia za kuwalaghai wakulima na kununua Korosho kabla ya msimu kuanza kwa kuwataka kutafuta kazi nyingine za kufanya kwani katika msimu huu wa mwaka 2018-2019 kumewekwa utarabitu madhubuti kuhakikisha watakao ruhusiwa kuuza Korosho ni wakulima wenye mashamba yanayo tambulika katika wilaya hiyo. Kauli hiyo ya serikali imetolewa na mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda wakati akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mtimwilimbwi Halmashauri ya mji Nanyamba waliojitokeza katika ziara yake ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wananchi. Akiwa…
Soma Zaidi >>WAFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA RUNGWE WAOMBA ASAS AWAJENGEE KIWANDA.
WAFUGAJI WA NG’OMBE WA MAZIWA RUNGWE WAOMBA ASAS AWAJENGEA KIWANDA. Na Rashid msita, Mbeya. Wafugaji wa ng’ombe wa maziwa wilayani Rungwe mkoani Mbeya, wamemuomba mnunuzi wao wa maziwa namba moja wilayani humo ASAS, kuwajengea kiwanda cha maziwa ili kuongeza thamani ya bei ya maziwa yao. Mwenyekiti wa chama cha ushirika cha MUWAMARU, Bw John Mwamfupe, amesema hayo leo Septemba 07, katika mkutano wa wafugaji uliofanyika wilayani hapo, ambapo ameomba uongozi wa ASAS kuwajengea kiwanda cha maziwa wafugaji hao kwa kuwa wamekuwa wakizalisha maziwa mengi kuliko wafugaji wa wilaya nyingine yeyote…
Soma Zaidi >>WANANCHI KILUMBU WILAYA YA KILOLO WALIA NA AFISA MIFUGO NA KILIMO
WANANCHI wa kijiji cha Kilumbu kata ya Ibumu wilaya ya Kilolo mkoani Iringa wadai ofisa mifugo amekuwa si msaada kwa wafugaji wenye uhitaji wa huduma ya kupatiwa tiba ya mifugo yao ila amekuwa mwepesi kukikimbilia kwenda kupima nyama inapochinjwa ili kupewa kitoweo. Wananchi hao watoa malalamiko hayo kwenye mkutano wa asasi isiyo ya kiserikali ya Mazombe Mahenge Development Association” (MMADEA) wakati wa mkutano wa hadhara wa lengo la ushiriki wa wananchi katika usimamizi wa uwajibikaji katika wilaya ya kilolo ,kwenye kata za Idete,Ibumu ,Uhambingeto na Nyanzwa . Walisema kuwa wanaomba maofisa ugani…
Soma Zaidi >>WAKULIMA WA KARANGA MAHENGE WILAYANI KILOLO WALIA NA SOKO
Wakulima wa zao la Karanga na mtama katika kata ya Mahenge wilayani Kilolo mkoa wa Iringa wameiomba serikali kusaidia kutafuta soko la mazao hayo. Wakulima hao walimweleza Mkuu wa wilaya ya Kilolo Asia Abdalah wakati wa mkutano wa hadhara Jana kuwa wamekuwa wakirudishiwa karanga kutoka Dar es Salaam kwa madai soko hakuna. Shaban Omari alisema kuwa kutokana na kukosekana kwa soko la uhakika wakulima wa zao la Katanga na Mtama wameanza kuhofu kulima kilimo hicho hivyo kuomba serikali kuwatafutia wanunuzi wa uhakika . Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya…
Soma Zaidi >>