MAAJABU YA BENZEMA, LIGI YA MABINGWA ULAYA

Na Shabani Rapwi. Mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid, Karim Benzema jana usiku amefunga goli moja katika ushindi wa magoli 2-1 iliopata timu yake ya Real Madrid dhidi ya Ajax katika mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ( UEFA Champions League) katika hatua ya 16 bora. Goli hilo alilofunga dakika ya 60′ na kuwa goli lake la 60 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, akishika nafasi ya nne ya wafungaji bora wa muda wote huku Cristiano Ronaldo akiwa ndiyo kinara wa ufungaji akiwa na magoli 121 nyuma ya Lionel…

Soma Zaidi >>

WIZARA YA AFYA YATOA MSAADA WA KISAIKOLOJIA KWA FAMILIA ZILIZO ATHIRIKA NA MATUKIO YA MAUAJI NJOMBE

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Idara Ustawi wa Jamii imetembelea kuwapa pole na kutoa msaada wa kisaikoloji na kijamii kwa Familia zilizoathirikana mauaji ya Watoto yalitokea mkoani Njombe. Timu hiyo imetembelea  Familia ya Bw. Gorden Mfugale inayoishi Mtaa wa Joshoni Kata ya Mji Mwema Halmashauri ya Mji Njombe Wilayani Njombe iliyopoteza Mtoto mmoja wa kiume Gidrack Mfugale (5) aliyepotea tarehe 04/02/2019 na kupatika tarehe 10/02/2019 akiwa amefariki dunia huku kiganja cha mkono kikiwa  na  mwili wake ulikutwa na majeraha kichwani katika  eneo la Shule…

Soma Zaidi >>

SERIKALI KUENDELEA KUJENGA MAZINGIRA WEZESHI NA ENDELEVU KATIKA SEKTA YA KILIMO

Na mwandishi wetu Dodoma Serikali imedhamiria kuendelea kujenga mazingira wezeshi na endelevu katika Sekta ya Kilimo kupitia sera imara na zenye kutekelezeka. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki wakati akifungua Kongamano la Tano la Wadau wa Sekta ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu Sera Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa tarehe 13Februari, 2019. Waziri alieleza kuwa, dhamira ya Serikali inaenda sambamba na mchango wa sekta ya Kilimo katika uzalishaji pamoja na ukuaji wa…

Soma Zaidi >>

WODI YA WAZAZI HOSPITAL YA MPWAPWA YAZIDIWA NA WAGONJWA

Na Stephen Noel -Mpwapwa Akina mama wanaojifungua Katika wodi ya wazazi Hospital ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma wanalazimika kulala wazazi wawili kwenye kitanda kimoja kutokana na uchache wa vitanda pamoja na udogo wa wodi hiyo Kauli hiyo imetolewa na Mganga mfawidhi wa hospital hiyo Dkt, Hamza Mkingule alipo kuwa akitoa taarifa mbele ya mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha Mapinduzi Bi Laula Ngozi katika ziara yake aliyo ifanya wilayani hapa kwa lengo la kuadhimisha miaka 42 ya kuzaliwa kwa chama hicho. Dkt Mkingule amesema Hospital Hiyo iliyojengwa miaka…

Soma Zaidi >>

WANANCHI MAKAMBAKO WAISHUKIA HALMASHAURI KUHUSU FIDIA

Na Amiri kilagalila Baadhi ya Wakazi wa mtaa wa Makatani Kata ya Lyamkena halmashauri ya Mji wa Makambako wameitupia lawama halmashauri ya mji huo kwa kuchelewa kulipa fidia ya eneo lililochukuliwa na serikali tangu mwaka 2014 kwa ajili ya ujenzi wa soko la mazao hali ambayo imetajwa kukwamisha shughuli za uzalishaji na maendeleo ya kudumu katika eneo hilo. Wakizungumzia kusuasua kwa utekelezaji wa mradi huo wakazi wa mtaa huo wamesema serikali imesababisha kuongezeka kwa ugumu wa maisha kwa wakazi wa mtaa huo ambao wameathiriwa na mpango wa ujenzi wa soko…

Soma Zaidi >>

TULIA TRUST YAKABIDHI VIFAA VYA UJENZI SHULE YA SEKONDARI KINYALA

Mbeya Taasisi ya Tulia Trust inayoongozwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Tulia Ackson,imekabidhi vifaa vya ujenzi kwa shule ya sekondari ya Kinyala wilayani Rungwe nkoani Mbeya. Akikabidhi vifaa hivyo meneja Tulia Trust Bi.Jacqueline Boaz amesema vifaa vya ujenzi vilivyokabidhiwa ni pamoja na mabati bando 13 yenye thamani ya shilingi milioni tano kwa shule ya sekondari Kinyala ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyo itoa Naibu Spika Dr.Tulia Ackson wakati wa harambee iliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa mwaka jana. BibJacqueline ameongeza kuwa katika harambee ile naibu…

Soma Zaidi >>

WATUHUMIWA WATATU WA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE WAFIKISHWA MAHAKAMANI

Na.Amiri kilagalila Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe imesikiliza kesi ya mauaji namba moja ya mwaka 2019 dhidi ya jamhuri na watuhumiwa watatu waliohusioka na mauaji ya watoto watatu katika kijiji cha ikando kata ya kichiwa wilayani Njombe. Akisoma kesi hiyo mbele ya mahakama wakili mwandamizi wa serikali Ahmed Seif,alisema kuwa mtuhumiwa namba moja Joel joseph Nziku mbena (35)dreva anaisha Magegere mjini Makambako,mshatakiwa namba mbili Nasson Alfredo kaduma (39) mkulima anaishi kijiji cha Ibumila na mtuhumiwa namba tatu Alphonce Edward Danda (51)naye anaishi katika kijiji cha Ibumila wote wanashtakiwa…

Soma Zaidi >>

WATENDAJI SEGEREA WAKOSA UAMINIFU KWENYE FEDHA ZA SERIKALI

Na Heri Shaban MBUNGE wa Segerea Bonah Ladislaus(CCM) amewalalamikia Watendaji kwa kukosa uaminifu katika fedha za Serikali. Bonah aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara Kata ya Vingunguti Jimboni Segerea Dar es salaam uliofanyika katika kata hiyo hii leo. Aidha alisema Rais wa awamu ya tano John Magufuli ametoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya miundombinu ya afya hivyo ni vema watendaji kushirikiana kikamilifu katika kuzisimamia ili miradi ikatekelezeke sawa sawa na ilivyopangwa. “Serikali imeleta fedha za kutosha shilingi bilioni 2 Jimbo la Segerea changamoto kubwa iliyokuwepo tuna watendaji wasio waminifu…

Soma Zaidi >>

SIMBA YAWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE, KUELEKEA KWENYE MCHEZO DHIDI YA AL AHLY

Na Shabani Rapwi. Klabu ya Simba SC imewaomba radhi mashabiki wake kuelekea kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa siku ya kesho Jumanne kwenye dimba la Taifa, Jijini Dar es Salaam, Saa 10:00 Jioni, kuwa tiketi za Platinum hazitakuwepo kwenye mchezo huo. Taarifa iliyotolewa hii leo Jumatatu na klabu hiyo kupitia mtandao wa Twitter kuwa tiketi za Platinum hazitakuwepo kwenye mchezo wa hapo kesho dhidi ya Al Ahly kama awali ilivyo tangazwa, huku walikuwa wameshanunua tiketi hizo watarudishiwa pesa zao na…

Soma Zaidi >>

MKUU WA MAJESHI NCHINI ATUA MKOANI NJOMBE

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo amefanya kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo kuhusu matukio ya mauaji ya watoto yaliyoanza Novemba mwaka jana. Jenerali Mabeyo ambaye ni Mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama amesema kuwa yuko mkoani humo kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya zoezi la kukabiliana na matukio hayo kwakuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinashirikiana. “Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana ikiwa ni pamoja na jeshi. Na mimi kama Mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi…

Soma Zaidi >>