MILIPUKO NA MILIO YA RISASI YASIKIKA JIJINI NAIROBI, MAGARI YACHOMWA MOTO,WENGI WAJERUHIWA.

Na,Jovine Sosthenes. Taharuki iliibuka jana mjini Nairobi kufuatia shambulio la milipuko na risasi inayosadikiwa kufanywa na magaidi katika eneo la 14 Riverside Drive, katika Hoteli ya Dusit D2 jijini Nairobi, Kenya na kusababisha vifo vya watu watano na kujeruhi wengine tisa. Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, Shambulio hilo linadaiwa kutokea Januari 15,2019. Mda, saa 9 alasiri na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa huku magari manne yakichomwa moto na milio ya risasi ikidaiwa kusikika kutoka eneo la tukio. Bado wahusika wa shambulio hilo hawajajulikana lakini askari wa Kitengo cha…

Soma Zaidi >>

TRUMP KUIANGAMIZA UTURUKI

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia ‘kuiangamiza Uturuki kiuchumi’ iwapo taifa hilo litawashambuliwa vikosi vya wakurdi nchini Syria baada ya wanajeshi wa Marekani kuondoka Syria. Katika ujumbe wake alioutuma kwenye mtandaoi wa kijamii Twitter, Trump amesema hakutaka Wakurdi kwa upande wao nao pia waichokoza Uturuki. Vikosi vya Marekani vimepambana kwa ushirikiano na wanamgambo wa Kikurdi kaskazini mwa Syria dhidi ya kundi la Islamic State (IS). Rais Recep Tayyip Erdogan amezungumza kwa hasira kuhusu Marekani kuliunga mkono kundi hilo, na kuapa kuliangamiza. Kauli ya Trump Jumapili inafuata shutumza zaidi dhidi ya…

Soma Zaidi >>

UWEKEZAJI BILA SIASA UNAWEZEKANA :ISSA SAMMA

Na Mwandishi wetu -NGARA KAGERA Msemaji wa wawekezaji kutoka Korea Kusini katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera Issa Samma amesema wakazi wa wilaya hiyo na viongozi wao wanaweza kukubali au kukataa uwekezaji bila kulumbana kwa kutanguliza siasa, ukanda na ukabila. Samma ametoa kauli hiyo siku chache baada ya mbunge wa jimbo la Ngara Alex Gashaza kunusurika kupigwa na wananchi wa kijiji cha Kazingati akipinga utaratibu uliotumika wa kuwagawia ardhi wawekezaji wa Korea Kusini wilayani Ngara. Amesema wawekezaji walijitokeza kutaka ardhi ya kilimo na kujenga viwanda Kuanza katika kijiji cha Kazingati…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YA GABON YAPINDULIWA NA JESHI

Kundi la wanajeshi nchini Gabon limetangaza kwamba limetekeleza mapinduzi ya serikali katika taifa hilo la Afrika Magharibi. Wanajeshi wenye vifaru na magari ya kivita wanashika doria katika barabara za mji mkuu Libreville. Shirika la habari la AFP inasema milio ya risasi imesikika jijini humo. Tangazo kutoka kwa kundi la vijana wa umri wa makamo linatangazwa na kurudiwa katika kituo cha redio cha serikali nchini humo, ambapo wanasema kumekuwepo na wasiwasi kuhusu uwezo wa Rais Ali Bongo kuongoza nchi hiyo. Walichukua udhibiti wa kituo hicho cha redio mwendo wa saa kumi…

Soma Zaidi >>

UPEPO MKALI NA MAWIMBI YAVIKUMBA VIJIJI VYA THAILAND.

  Na. JovineĀ Sosthenes Mvua, upepo mkali na mawimbi vimelikumba eneo la kusini mwa Thailand hususani katika maeneo ya vijiji vilivyo jirani na fukwe ikiwemo maeneo ya utalii yaliyokumbwa na kimbunga kikali cha Papuk. Hakuna taarifa ya vifo lakini tayari mamlaka ya hali ya hewa nchini humo imetoa tahadhari huku ikishuhudiwa mamia ya watalii wakiondoka katika maeneo waliyokuwepo. Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini humo imesema kimbunga kingine kikubwa kinatarajiwa kupiga jioni ya leo na kitakua kina kasi ya kilomita 80 kwa saa. Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga zaidi eneo la Nakhon…

Soma Zaidi >>

RAIS AL BASHIR ABANWA VIKALI NA WASUDANI, WAAMUA KUANDAMANA KWA MAMIA MJINI KHARTOUM

Khartoum, SUDAN. Maandamano makubwa yamefanyika mwisho wa mwaka 2018 katika mji mkuu wa Sudan Khartoum yakiitikia wito wa baadhi ya vyama vya upinzani na jumuiya za kiraia kwa ajili ya kulalamikia ughali wa maisha na hali mbaya ya uchumi wa nchi hiyo. Waandamanaji hao walikuwa wakielekea katika Ikulu ya Rais mjini Khartoum wakati walipokabiliwa na vyombo vya usalama vilivyolazimika kutumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji hao waliokuwa wakipiga kelele dhidi ya serikali ya Rais Omar Hassan al-Bashir. Waandamanaji wengi walikuwa wamebeba mabango na maberamu yenye maandishi yasemayo ‘Irhal’ yaani…

Soma Zaidi >>

DRC:HUDUMA YA INTANETI NA KUTUMA SMS YAKATWA GHAFLA MPAKA MATOKEO YA UCHAGUZI YATAKAPOTANGAZWA.

Kinshasa, DRC. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imekata huduma ya intaneti na ujumbe wa mfupi wa simu za mkononi (SMS) kote nchini humo kwa siku ya tatu mfululizo hii leo wakati nchi hiyo ikisubiri kwa hamu kubwa matokeo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais. Hali hii imetokea kuanzia juzi Desemba 31 kufuatia uchaguzi wa Rais nchini humo, uliofanyika Jumapili iliyopita, huku baadhi ya mikoa ikigubikwa na ghasia na machafuko. Pande mbili za upinzani na muungano wa chama tawala hapo juzi (Desemba 31) zilieleza kuwa, zinaelekea kuibuka na…

Soma Zaidi >>

RAIS ESSEBSI ATOA SALAMU ZA MWAKA 2019 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Tunis, TUNISIA. Rais wa Tunisia, Beji Caid Essebsi, amezungumzia uchaguzi ujao wa rais na bunge nchini humo na kusema kuwa mwaka 2019 utakuwa mwaka muhimu kwa nchi hiyo. katika ujumbe wake mwaka mpya wa 2019, Rais Essebsi ameeleza kuwa jitihada kubwa zinapaswa kufanyika kuandaa mazingira bora ya kufanyika uchaguzi wa wazi, huru na wa kidemokrasia katika mwaka huu wa 2019. Aidha, Kiongozi huyo amewataka wananchi wa nchi hiyo kutumia haki yao ya kikatiba na kushiriki kwenye chaguzi hizo, ambapo amewataka Watunisia kuwachagua watu wanaofaa kwa ajili ya kushika nyadhifa za…

Soma Zaidi >>

AFGHANISTAN YAONGOZA VIFO WANATASNIA YA HABARI 16 WAUAWA 2018

Shirikisho la mashirika ya waandishi wa habari, IFJ imesema kuwa idadi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa tasnia ya habari waliouawa mwaka wa 2018 imepanda na kufika 94. Miongoni mwa hao 84 walikuwa waandishi wa habari, wapiga picha, mafundi mitambo na madereva. Kulingana na ripoti ya shirika hilo, nchi hatari zaidi kwa waandishi wa habari mwaka huu unaomalizika ilikuwa, Afghanistan ambako wafanyakazi 16 wa taaluma ya habari walipoteza maisha, ikifuatiwa na Mexico ambako 11 waliuawa. Nchi zingine ni Yemen, Syria, India, Somalia, Pakistan na Marekani.  

Soma Zaidi >>

RUSSIA:HATUKOSI USINGIZI HATA KIDOGO KWA VITISHO VYA MAREKANI

Moscow, RUSSIA. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia, Sergey Ryabkov, ametangaza kuwa nchi yake haishughulishwi na matamko na amri iliyotangazwa na Marekani kutekeleza vitisho vyake kuhusu kujitoa katika Mkataba wa Silaha za Masafa ya Wastani za Nyuklia (ANF). Waziri Ryabkov amenukuliwa na shirika la habari la RIA Novosti akisema hayo na kuongeza kuwa mkataba wa ANF uko wazi na umekuwa ukitangazwa waziwazi hadharani, hivyo, vitisho na amri zinazotolewa na Marekani kuhusu mkataba huo hazikubaliki kabisa. Marekani inaituhumu Russia kuwa inakanyaga vipengele vya mkataba wa ANF, hivyo Marekani imeamua…

Soma Zaidi >>