MAUZO DSE YAPOROMOKA

Mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka kutoka Sh bilioni 1.11 wiki iliyopita hadi Sh milioni 676.26 wiki hii. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko, Emanuel Nyalali, amesema mauzo hayo yametokana na kuuzwa kwa mihamala 166. “Wakati huo thamani ya Soko la Hisa imeongezeka hadi kufikia Sh trilioni 22.18 kutoka Sh 21.99 wiki iliyopita,” amesema Nyalali. Aidha amesema katika kipindi hicho, hatifungani za serikali na makampuni zenye thamani ya Sh bilioni 1.96 ziliuzwa kwenye mihamala…

Soma Zaidi >>

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUTUNZA KUMBUKUMBU MIAMALA MALIPO YA KODI KWA MIAKA 5 MFULULIZO

Serikali imewashauri wafanyabiashara wote nchini kutunza kumbukumbu zao za miamala ya ulipaji kodi katika kipindi cha miaka mitano mfululizo kama sheria ya usimamizi kodi ya mwaka 2015 kifungu cha 35 kinavyoelekeza. Ushauri huo umetolewa leo Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akijibu swali la Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo aliyehoji iwapo serikali itapokea kumbukumbu ya namba ya malipo iwapo mfanyabiashara atapoteza taarifa za miala zilizopo katika simu. “Walipa kodi wajitahidi kuwa na kumbukumbu kama kifungu cha 35 cha sheria usimamizi kodi ya…

Soma Zaidi >>

SERIKALI KUTOA MASHINE ZA EFD KWA WAFANYABIASHARA WADOGO KUANZIA JULAI MOSI

Serikali imesema kuanzia Julai mosi mwaka huu, kupitia Mamlaka ya Mapato nchini- TRA itaanza kutoa mashine za risiti za kielektroniki-EFD kwa wafanyabiashara wadogo nchi nzima. Hayo yamesemwa leo Bungeni jijini Dodoma katika kipindi cha maswali na majibu na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji wakati akijibu hoja ya Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo aliyeishauri serikali kutoa mashine za EFD bure kwa wafanyabiashara wadogo. “Tumeanza utaratibu wa kufikia wafanyabiashara wote, na hata kwanza mashine hizo hazikutolewa bure wafanyabiashara wakubwa walipewa kwa mkopo, kwa hivyo tuna mpango kupitia TRA…

Soma Zaidi >>

TRA YASAJILI WAFANYABIASHARA WAPYA 600

Mamlaka ya Mapato nchini-TRA imesajili wafanyabiashara wapya 600 kupitia kampeni maalumu ya utoaji huduma na elimu kwa mlipa kodi iliyofanyika mkoani Geita. Akizngumza baada ya kukamilika kwa kampeni hiyo mwishoni mwa wiki, Meneja wa TRA mkoani Geita, James Jilala ameishukuru Idara ya Huduma kwa Mlipa Kodi kwa kuwafikia wafanyabiashara hao walioko kwenye maeneo yasiyokuwa na ofisi za mamlaka hiyo. Jilala alisema wafanyabiashara wengi walishindwa kusajiliwa na kupatiwa huduma ya Utambulisho wa Mlipakodi-TIN kwa wakati kutokana na umbali wa ofisi za TRA ambapo walitakiwa kusafiri umbali wa zaidi ya kilomita 100.…

Soma Zaidi >>

MAZINGIRA MAZURI YA UWEKEZAJI YAWAVUTIA WAWEKEZAJI UFARANSA, WAAHIDI KUWEKEZA NCHINI

Chama cha Waajiri nchini Ufaransa-MEDEF kinachowakilisha asilimia 75 ya sekta binafsi nchini humo, chenye kampuni wanachama takribani 750,000, kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi nchini-TPSF, Ubalozi wa Tanzania Paris na Ubalozi wa Ufaransa Dar es Salaam. Kimeandaa  Jukwaa la Kimataifa la Biashara linalojulikana kwa jina la TPSF-MEDEF International Business Forum, litafanyika Jumatano ya Aprili 18 mwaka huuu katika Hoteli ya Serena iliyoko Jijini Dar es Salaam. Jukwaa hilo litatanguliwa na ujio wa Ujumbe wa viongozi wa wafanyabiashara kutoka nchini Ufaransa utakaotembelea Tanzania kwa muda wa siku tatu kuanzia Aprili…

Soma Zaidi >>

MITAJI, MAUZO YA DSE YAPUNGUA KUTOKANA NA KUSHUKA KWA BEI ZA HISA

Mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kuanzia Machi 2 hadi 9, 2018 yameshuka kutoka Shilingi bilioni 2.9 hadi kufikia milioni 518, vile vile idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa katika soko hilo imeshuka kutoka hisa milioni 2.4 hadi hisa laki 6.9. Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Masoko Mwandamizi DSE, Marry Kinabo wakati akitoa taarifa ya kila wiki ya mauzo ya soko hilo kwa wanahabari. Pia, taarifa hiyo inaonyesha kupungua kwa ukubwa wa mtaji wa kwa Sh. Bilioni 417 kutoka Trilioni…

Soma Zaidi >>

POLISI KENYA YATANGAZA DAU LA MILLION MOJA KWA YEYOTE ATAKAYESAIDIA KUKAMATWA KWA KIONGOZI WA KIGAIDI ANAYEFANYA UHALIFU MLIMA ELGON.

NAIROBI. Nchini Kenya Jeshi la polisi nchini humo limezindua msako mkali dhidi ya kiongozi wa kikundi cha kigaidi kinachowauwa na kuwahangaisha wakazi wa mlima Elgon. Idara ya polisi imeweka wazi picha ya mtu mmoja ajulikanaye kama Timothy Kiptanui Kitai alimaarufu “Cheparkach” huku ikitangaza dau la shilingi milioni moja za kikenya kwa yeyote yule atakayesaidia kukamatwa kwa bwana huyo. Mnamo jumanne,Machi 6 hapo jana waziri wa usalama na maswala ya ndani Fred Matiang`i alitanganza amri ya kutotoka nje (curfew) kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi saa kumi na mbili asubuhi…

Soma Zaidi >>

Viwanda 3,500 vyajengwa nchini,ndani ya miaka miwili

Rais John Magufuli amesema utekelezaji wa azma ya kujenga viwanfda nchini unaelendelea vizuri ambapo katika kipindi cha miaka miiwili viwanda takribani 3,500 vimejengwa na vingine vingi vinaendelea kujengwa. Dkt. Magufuli amebainisha hayo jana katika hafla yam waka mpya aliyowaandalia mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam. Rais Magufuli aliwahakikishia Mabalozi pamoja na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa walipo hapa nchini, kwamba katika mwaka 2018 serikali yake itaendeleza juhudi za kuboresha mazingira ya uwekezaji ikiwemo mapambano dhidi ya rushwa, kuboresha miundombinu ya barabara, reli na usafiri…

Soma Zaidi >>

TAARIFA KUHUSU HALI YA UCHUMI NA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI 2017/2018

UTANGULIZI Nashukuru sana kupata fursa nyingine ya kuzungumza nanyi leo tunapokaribia mwisho wa mwaka 2017. Lengo la Serikali ni kuwapatia Watanzania taarifa rasmi kuhusu (i) mwenendo wa uchumi wa Taifa kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2017 na kwa miezi ya hivi karibuni pale ambapo tunazo takwimu, (ii) utekelezaji wa bajeti ya Serikali 2017/18 hadi sasa, (iii) changamoto zilizopo mbele yetu na matarajio mpaka Juni 2018. Aidha, nitatoa ufafanuzi kwa lugha nyepesi katika baadhi ya maeneo ambayo yamekuwa hayaelezwi ipasavyo au yanapotoshwa hususan katika mitandao ya kijamii na baadhi ya…

Soma Zaidi >>