CCM KILOSA WAPITA BILA KUPINGWA KATA MBILI

Chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kimefanikiwa kupita bila kupingwa katika kata mbili zilizowekewa pingamizi awali . kwa mujibu wa Luciano Mbosa ambaye ni kitengo cha uchaguzi mkoa wa Morogoro ndani ya CCM ,kuwa CCM imeshinda kufuatia ushindi wa pingamizi zilizowekwa na wagombea wa chadema Mbosa amezitaja kata hizo kuwa ni Zombo na Magomeni. Hata hivyo alisema mkoa wa Morogoro ni kata tatu ndizo zilipaswa kufanya uchaguzi mdogo ila kwa sasa wamebaki na kata moja ya Namwawala wilaya ya Kilombelo ndiko uchaguzi utafanyika .

Soma Zaidi >>

ALIYEWATAPELI WATALII DOLA 5000 AKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inamshikilia Omwailimu Sosthenes ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Utalii ya  Arise Special Sunrise,kwa tuhuma za kuwatapeli watalii wawili Dola za kimalekani 5000. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, DCP Liberatus Sabas, amesema mtuhumiwa huyo aliwatapeli watalii hao ambaye mmoja anaishi Marekani na mwingine nchini India kwa makubaliano kwamba angewapeleka safari ambazo walizipanga. Amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuwatapeli wageni hao aliwatelekeza katika nyumba ya wageni maeneo ya Sinza na walipojaribu…

Soma Zaidi >>

RIEK MACHAR MBIONI KUREJESHEWA WADHIFA WAKE

Kiongozi wa kisiasa maarufu nchini Sudan Kusini na aliyekuwa Makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Riek Machar, atarejeshwa katika wadhifa wake kama sehemu ya makubaliano ya amani ya kuvifikisha mwisho vita vya karibu miaka mitano ambavyo vimewaua maelfu ya watu na kuliharibu kabisa taifa hilo changa barani Afrika. Makubaliano hayo yaliafikiwa katika mazungumzo ya mjini Entebbe, na yalisimamiwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na kuhudhuriwa na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Sudan Omar al-Bashir na Machar. Taarifa ya ofisi ya rais ya Sudan Kusini…

Soma Zaidi >>

Tundu Lissu atoa ujumbe mzito kuhusu afya yake

Kupitia ukurasa wake wa mtandao, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye anapatiwa matibabu nchini Ubeligiji aliandika; “Wapendwa wangu natumaini wote hamjambo asubuhi hii (angalau kwangu ni saa 12 kasoro ya asubuhi). Nawaomba msamaha kwa kuwaweka roho juu jana halafu sikuonekana. Nilipata wageni na by the time nimemalizana nao muda ulishaenda sana. Naomba nianze kwa kuwapa briefing ya afya yangu. Wengi wenu mtakuwa mmeona video clips nikifanya mazoezi ya kutembea. Clip hizo zinaonyesha naendelea vizuri na ni kweli. Operesheni ya mwezi uliopita imepona, angalau kwenye muscles. Mfupa bado una kazi…

Soma Zaidi >>

Kangi Lugola alivyomzuia Kamishina wa Magereza kuingia kwenye mkutano wake

Kamishina wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa amezuiwa kuingia kwenye mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola baada ya kuchelewa kwa dakika mbili kuingia kwenye ukumbi ambako mkutano huo ulifanyika. Waziri huyo ambaye aliingia kwenye ukumbi majira ya saa 4:51 asubuhi ambapo mara baada ya kuingia aliagiza kwamba ikifika saa 5:00 mtu ambaye atakuwa hajaingia ukumbuni hataruhusiwa kuhudhulia kikao chake isipokuwa waandishi wa habari. Ilipofika saa 5:00 aliagiza mlango ufungwe na usifunguliwe kwa mtumishi yoyote wa wizara wala Kamanda yoyote kuingia labda awe mwanahabari. Ambapo…

Soma Zaidi >>

DIWANI WA CCM APOTEZA MAISHA KWA AJALI ASUBUHI YA LEO.

Diwani wa CCM katika kata ya Tindabuligi wilayani Meatu mkoani Simiyu, ndugu Seleman Mahega amepoteza maisha akiwa katika Hospitali ya Mwandoya alipokuwa akipatiwa huduma ya kwanza mara baada ya kuapata ajali asubuhi ya leo. Diwani huyo ni mmoja wa wale waliokuwa kwenye msafara wa mwenyekiti wa Uvccm Taifa Kheri James, uliopata ajali asubuhi ya leo mara baada ya magari katika msafara huo kugongana baada ya moja ya gari kwenye msafara kufunga breki ya ghafla iliyosababisha kutokea vumbi lilipelekea madereva katika magari ya nyuma yake kushindwa kuona vizuri. Taarifa za msiba…

Soma Zaidi >>

HII HAPA TAARIFA YA UTEUZI KUTOKA IKULU ILIYOTOLEWA JIONI YA LEO.

Taarifa kutoka Ikulu inasema kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Prof. Siza Donald Tumbo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utawala ya Chuo Kikuu cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College – ATC). Taarifa hiyo pia inaeleza juu ya kuteuliwa kwa Mhandisi Mussa Iyombe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (Public Service Social Security Fund- PSSSF). Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa wenyeviti hao wa bodi umeanza siku ya jana Mei 13, 2018.  

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI ASEMEZANA NA MANGULA, KINANA, OFISI NDOGO ZA CCM LUMUMBA.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Ijumaa ya leo Mei 11, 2018, amefanya ziara katika ofisi ndogo za chama hicho zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Mhe. Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu mwenyekiti wa CCM –Bara, Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa Chama hicho, Abdulrahaman Kinana. Hata hivyo mpaka sasa hakuna taarifa iliyotoka kuelezea kile kilichozungumzwa na viongozi hao wa chama tawala nchini Tanzania, lakini wadadisi wa mambo wanaamini mazungumzo hayo…

Soma Zaidi >>

VIKOSI VYA SIMBA NA YANGA VINAVYOUMANA JIONI HII.

Kikosi cha Simba SC kinachoanza dhidi ya Yanga SC, mechi ya Ligi Kuu Bara jioni hii. Aishi Manula Erasto Nyoni Nicholas Gyan Yusufu Mlipili James Kotei Jonasi Mkude Asante Kwasi Shomari Kapombe John Bocco Emanuel Okwi Shiza Kichuya   Kikosi cha akiba Mohamed Nduda Paul Bukaba Said Ndemla Mzamiru Yassin Laudit Mavugo Rashid Juma Mohamed Hussein Kikosi cha Yanga SC dhidi ya Simba SC, kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara, jioni hii. Youthe Rostand Hassani Kessy Gadiel Mbaga Andrew Vicent Kelvin Yondani Saidi Juma Yusufu Mhilu Papy Tshishimbi Obrey Chirwa…

Soma Zaidi >>