SASA ZAMU YA WAKUU WA WILAYA, RAIS MAGUFULI AMTUMBUA DC KAHAMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ametangaza kumfuta kazi aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, ndugu Fadhili Nkurlu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ikulu zinasema kuwa, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo hii leo Julai 15, 2018. Kufuatia hatua hiyo, Rais Magufuli amemteua Anamringi Macha kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama. Mkuu wa Wilaya, Anamringi Macha ametakiwa kuripoti katika kituo chake cha kazi mara moja. Hata hivyo taarifa hiyo haijaeleza sababu za Rais Magufuli kufikia uamuzi wake wa kumtumbua ndugu Fadhili Nkurlu.

Soma Zaidi >>

ALIYEWATAPELI WATALII DOLA 5000 AKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inamshikilia Omwailimu Sosthenes ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Utalii ya  Arise Special Sunrise,kwa tuhuma za kuwatapeli watalii wawili Dola za kimalekani 5000. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, DCP Liberatus Sabas, amesema mtuhumiwa huyo aliwatapeli watalii hao ambaye mmoja anaishi Marekani na mwingine nchini India kwa makubaliano kwamba angewapeleka safari ambazo walizipanga. Amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuwatapeli wageni hao aliwatelekeza katika nyumba ya wageni maeneo ya Sinza na walipojaribu…

Soma Zaidi >>

Tundu Lissu atoa ujumbe mzito kuhusu afya yake

Kupitia ukurasa wake wa mtandao, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye anapatiwa matibabu nchini Ubeligiji aliandika; “Wapendwa wangu natumaini wote hamjambo asubuhi hii (angalau kwangu ni saa 12 kasoro ya asubuhi). Nawaomba msamaha kwa kuwaweka roho juu jana halafu sikuonekana. Nilipata wageni na by the time nimemalizana nao muda ulishaenda sana. Naomba nianze kwa kuwapa briefing ya afya yangu. Wengi wenu mtakuwa mmeona video clips nikifanya mazoezi ya kutembea. Clip hizo zinaonyesha naendelea vizuri na ni kweli. Operesheni ya mwezi uliopita imepona, angalau kwenye muscles. Mfupa bado una kazi…

Soma Zaidi >>

Kangi Lugola alivyomzuia Kamishina wa Magereza kuingia kwenye mkutano wake

Kamishina wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa amezuiwa kuingia kwenye mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola baada ya kuchelewa kwa dakika mbili kuingia kwenye ukumbi ambako mkutano huo ulifanyika. Waziri huyo ambaye aliingia kwenye ukumbi majira ya saa 4:51 asubuhi ambapo mara baada ya kuingia aliagiza kwamba ikifika saa 5:00 mtu ambaye atakuwa hajaingia ukumbuni hataruhusiwa kuhudhulia kikao chake isipokuwa waandishi wa habari. Ilipofika saa 5:00 aliagiza mlango ufungwe na usifunguliwe kwa mtumishi yoyote wa wizara wala Kamanda yoyote kuingia labda awe mwanahabari. Ambapo…

Soma Zaidi >>

BREAKING NEWS :BASI LAIGONGA TRENI NA KUUWA WATU 7 NA MAJERUHI 27 MKOANI KIGOMA

Na Joel Silver Watu 7 wamefariki dunia na wengine 27 wamejeruhiwa vibaya, baada ya basi la Kampuni ya Hamida kugonga treni ya mizigo mkoani Kigoma. Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoani Kigoma Martin Otieno, amesema kwamba ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:15 asubuhi ya leo katika eneo la Gungu, baada ya basi hilo ambalo linafanya safari zake kutoka Mkoani Kigoma kwenda Tabora, kugonga treni ya mizigo iliyokuwa ikipita kwenye njia yake, licha ya dereva wa treni kupiga honi kumpa tahadhari dereva wa basi. Dereva wa basi…

Soma Zaidi >>

POLISI WASABABISHA TAHARUKI KUBWA, KILIMANJARO.

Shughuli katika mji wa Moshi leo zimesimama kwa muda wakati vikosi vya jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro kupita katika maeneo mbalimbali ya mji huo wakiwa na silaha za moto na kuzua hali ya taharuki kwa baadhi ya wakazi wa mji huo. Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Kamishna Msaidizi wa Polisi ,Hamis Issah amesema zoezi hilo ni la kawaida kwa askari polisi na kwamba wamekuwa wakipata mafunzo ya nadharia kwa muda mrefu sasa wameamua kuyafanya kwa vitendo.

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE ASUBUHI HII.

Asubuhi ya leo April 23, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya mabadiliko ya kiuongozi katika Benki ya Posta Tanzania (TPB). Rais Magufuli amemteua Dkt. Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Prof. Lettice Rutashobya, ambae amemaliza muda wake. Kwa mujibu wa Ikulu, uteuzi wa Dkt. Edmund Bernard Mndolwa umeanza  leo tarehe 23, April, 2018.

Soma Zaidi >>