CAF YAWEKA HADHARANI VIPENGELE 9 VYA ‘CAF AWARDS 2018’

Shirikisho la Soka Barani Afrika ( CAF ) limeweka hadharani vipengele 9 vya tuzo za ‘CAF Awards 2018’ vitakavyowaniwa mwaka huu Kwa Mashindano Mbalimbali yaliyofanyik.

vipengele vilivyotajwa
1. African Player of the Year (Mchezaji Bora Afrika wa Mwaka)

2. Women’s Player of the Year (Mchezaji Bora wa mwaka kwa Wanawake Afrika)

3. Youth Player of the Year (Mchezaji Bora Kijana wa Mwaka Afrika)

4. Men’s Coach of the Year (Kocha Bora wa mwaka Afrika wa Kiume)

5. Women’s Coach of the Year (Kocha Bora wa mwaka Afrika wa kike)

6. Men’s National Team of the Year (Timu Bora ya Taifa Kwa Wanaume ya mwaka)

7. Women’s National Team of the Year (Timu bora ya Taifa Kwa Wanawake ya mwaka)

8. Goal of the Year (Goli Bora la Mwaka)

9. Africa Finest XI (Kikosi Bora Afrika Cha Mwaka)

Kipengele cha Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa kiume na wa Kike, kura zake zitapigwa na Kamati ya Ufundi ya CAF na Waandishi wa Habari za Michezo Wachezaji wakongwe wa Afrika,Makocha wa Vilabu waliozifikisha timu Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho na Klabu Bingwa Afrika, Makocha wa timu za Taifa zote 54 wanachama wa CAF na Manahodha wake

Kipengele Cha Tuzo ya Mchezaji Bora kijana, Kocha Bora wa kiume wa Mwaka, Kocha Bora wa kike wa mwaka, timu ya taifa bora ya mwaka ya Kiume na ya Kike, kura zake zitapigwa na Kamati ya Ufundi ya CAF na Waandishi wa Habari za Michezo,Wachezaji wakongwe wa Afrika, makocha ambao wamevifikisha vilabu hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na Klabu Bingwa Afrika

Goli bora la mwaka litapigiwa kura, lenye kura nyingi ndio litatangazwa kuwa bora

Sherehe ya kutangaza washindi wa tuzo hizo zitafanyika January 08,2019 nchini Senegal katika jiji la Dakar.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.