BUNGE SPORTS CLUB YAFANYA MAKUBWA BUJUMBURA.

 

Bujumbura,Burundi.

Bunge Sports Club yatikisa Bujumbura, soka yawaduwaza EALA mabao 2-0, mpira wavu ( wanawake ) wamewazabua EALA seti 3-0, wakati netball Bunge Queens yawasambaratisha Kenya magoli 52-29

Timu za Bunge Sports Club za soka, mpira wa wavu ( wanawake ) na Netball zimekuwa gumzo katika jiji la Bujumbura baada ya kushinda michezo yote mitatu iliyoshiriki leo disemba 6, 2018.

Katika michezo ya tisa ya Mabunge ya Afrika Mashariki, walikuwa ni Bunge Queens walioanza kusafisha njia ya Ushindi baada ya kuwapoteza kabisa Kenya kwa kuwalaza magoli 52-29 kwenye mchezo uliofanyika kwenye viwanja vya Chuo cha Taifa cha Ualimu cha Burundi.

Nayo timu ya mpira wa wavu ( wanawake ) ikafuata nyayo kwa kuwagaragaza EALA seti 3-0.

Kama vile haitoshi, Ndugai Boyz wakawa cha bangalore EALA kwa magoli 2-0 katika mchezo ambao mashabiki walibaki wakijiuliza ilikuwaje Bunge SC ilipoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya mabingwa watetezi Bunge la Uganda kutokana na mchezo wa hali ya juu wa pasi za kuvutia..

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.