BREAKING NEWS: MFANYABIASHARA MWINGINE WA KIHINDI ATEKWA TABORA

 

 

TABORA:
Mfanyabiashara mwingine mwenye asili ya Kihindi aliyefahamika kwa jina la Kishori ametekwa na watu wasiojulikana usiku wa Oktoba 25, 2018 na kisha kuondoka nae sehemu isiyojulikana.

Kwa mujibu wa mashuhuda ambao wameongea na mwandishi wa mtandao wa Dar Mpya mapema leo mjini hapa, wameeleza kuwa, tukio hilo limetokea eneo la katikati ya mji wa Tabora karibu na Golden Eagle hotel eneo ambalo ni jirani na ofisi na makazi yake.

Shuhuda hao wameongeza kuwa, wakati tukio hilo limetokea lilikuwa ni la ghafla na walimchukua na kisha kukimbia na gari na kutokomea huko kusiko julikana.

Hata hivyo imeelezwa kuwa watu hao walimtaka awape fedha ili wamuachie, lakini mfanyabiashara huyo aliwaomba warudi nyumbani ndio wape hizo fedha na watu hao walimkubalia baadae kwenda nae nyumbani kwa lengo la kuzichukua fedha ili wamuachie.

“Wakati usiku wanafika kuchukua hizo fedha alizoahidi angewapa ili wamuachie, tayari jeshi la Polisi walitaarifiwa na walifika baada ya mmoja wa wafanyakazi wa muhindi huyo na wengine kushuhudia tukio hilo. Lakini watu hao walishtukia mchezo huo na kukimbia na mfanyabiashara huyo”.

Habari zaidi zinaeleza kuwa, baada ya watu hao kukimbia na mfanyabiashara huyo walikuja kupata ajali katika barabara ya Ujenzi eneo la hoteli ya Wilca baada ya kugonga mti.

Mtandao wa Dar Mpya ulipowasiliana na Kamanda wa Polisi wa Tabora RPC Emmanuela Nyeli amesema ndio kwanza amezisikia habari hizo kutoka kwa mwandishi na atazifanyia kazi kama nikweli ama si kweli.

Mtandao huu unaendelea kufuatilia tukio hilo.

Related posts

One Thought to “BREAKING NEWS: MFANYABIASHARA MWINGINE WA KIHINDI ATEKWA TABORA”

  1. Benedicto

    Emungu utunuduru

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.