“BENKI YA NMB KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MAENDELEO KISARAWE”

MKUU WA WILAYA YA KISARAWE NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KISARAWE WAPANGA MKAKATI WA MAENDELEO WILAYA YA KISARAWE KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA NMB.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Bi. Jokate Mwegelo, pamoja na Mussa Gama, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe, wamefanya kikao muhimu cha ushirikiano katika Maendeleo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji (Managing Director & CEO) wa Benki ya NMB Tanzania, Bi. Ineke Bussemaker, akiongozana na Kiongozi wa Mahusiano ya Kibenki na Serikali (Head of Government Banking), Bibi Vicky P. Bishubo.

Kikao kiliangazia maeneo makubwa matatu ambayo ni Elimu, Afya na uwezeshaji wa kiuchumi.

1. Elimu
Kisarawe itashirikiana na Benki ya NMB kutoa elimu ya Masuala ya fedha na usimamizi wake ( Financial Literacy) kwa makundi mbalimbali tukianza na watoto na vijana, ili kuwajengea uwezo wa kusimamia fedha kuanzia umri mdogo.

Pia, NMB imekubali kuwa mdau mkubwa wa kujenga mazingira bora ya ufundishaji na kujifunza katika Shule za Wilaya ya Kisarawe.

2. Afya
Benki ya NMB ipo tayari kusaidia jitihada za jamii kwa mfumo wa fursa na vikwazo vya maendeleo ulioboreshwa

3.Uwezeshaji wa kiuchumi.

Kisarawe itashirikiana na Benki ya NMB kuwawezesha wananchi, hasa vijana na wanawake, na makundi maalumu kiuchumi, ikilenga sekta ya kilimo, kwa mambo manne(4)

Mosi; Kisarawe na NBM tutashirikiana kuwatuma mawakala maalumu watakao kutana na makundi ya Vijana na Wanawake, kutambua namna bora ya wawawezesha na kuwajengea uwezo, Wale waliofaidika na mikopo na kufanya vizuri kuweza “kumaliza mafunzo ” kwa kupewa mikopo mikubwa zaidi itakayowawezesha kuinua biashara zao na kufikia watu wengi zaidi.

Pili; Kisarawe itashirikiana na NMB kujenga ghala la  Mfumo wa Stakabadhi wa mazao hasa kwenye zao la Korosho ambapo kwa Kisarawe uzalishaji umekuwa ukiongeza msimu mpaka msimu kutoka tani 54 msimu 2015, tani 193 msimu 2016, tani 583 msimu 2017, na malengo kwa msimu wa 2018 ni kufikia  tani 1000.

Tatu; Kisarawe itashirikiana na NMB katika ujenzi wa kiwanda cha usindikaji wa wanga wa muhogo ili kuwezesha wakulima wetu kuhamasika kupanda zao la mihogo kwa malengo ya kibiashara lakini pia kuweza kuhudumia soko linalokua kwa hivi sasa.

Serikali imeialika NMB kuhudhuria harambee ya uzinduaji wa kampeni ya Tokomeza Zero, Jumamosi ya Tar. 22/08/2018.Hivyo Kikao cha leo ni zao la wito wetu kwa wadau mbali mbali wanaopenda kushirikiana nasi katika kuijenga Kisarawe Mpya.

Mkuu wa Wilaya, Bi. Jokate Mwegelo, amewapongeza benki ya NMB kwa kuonesha moyo wa dhati kufanya kazi pamoja na Serikali katika kuleta maendeleo, Wilaya ya kisarawe, na ametoa wito kwa wadau wengi zaidi katika sekta za fedha, kilimo na viwanda kuwekeza katika kuinua na kuwawezesha kiuchumi wananchi wa Wilaya ya Kisarawe.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.