BENJAMIN MKAPA AAHIRISHA MAZUNGUMZO YA AMANI YA BURUNDI

 

 

Arusha.

Shughuli za ufunguzi wa mazungumzo ya amani nchini Burundi zilizokuwa zifanyike siku ya Jumatano jana jijini Arusha zililazimika kusogezwa mbele ingawaje mwezeshaji wa mazungumzo hayo Rais wa zamani wa Tanzania Benjamin Mkapa hakueleza sababu.

Hata hivyo taarifa za ndani zimedai kuwa Mkapa ametuma ujumbe wake kwa serikali ya Rais Pierre Nkurunziza kuitaka, itume wawakilishi katika mazungumzo hayo.

Awali,serikali ya Burundi iliomba kusogezwa mbele kwa mazungumzo hayo ikidai kuwa nchi hiyo iko kwenye maombolezo ya mwezi mzima wa Oktoba.

Wajumbe wa upinzani waishio nje ya Burundi wanaojumuika katika muungano (Cenared) pamoja na Wajumbe wa upinzani wa ndani wa muungano (Amizero yabarundi) wakiongozwa na Agathon Rwasa wapo Arusha tayari kwa mazungumzo hayo.

Mazungumzo ya amani yalianza baada jaribio la mapinduzi mwaka 2015, wakati Rais Nkurunziza alipoamua kuwania urais kwa muhula wa tatu kinyume cha katiba.

Mazungumzo haya yalitarajiwa kuwa ya mwisho, kuleta amani nchini Burundi kuelekea Uchaguzi wa mwaka 2020.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.