BENARD MEMBE AGEUKA KUWA TISHIO KWENYE URAIS 2020,UVCCM WAIBUKA NA KUMKINGIA KIFUA JPM

NA KAROLI VINSENT
NI wazi Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Benard Membe ni kama amekitikisa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuhusu mikakati yake ya kuwania Urais kupitia chama hicho kwenye uchaguzi wa mwaka 2020 ndivyo naweza kusema,baada ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuibuka na kutaka Rais John Magufuli apewa nafasi tena ya Urais 2020.

Katibu wa idara ya uhamasishaji na chipukizi waUmoja huo Hassan Bomboko, amesema kuelekea uchaguzi wa mwaka 2020 umoja huo utaenda Dodoma kuhakikisha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa sasa Rais John Pombe Magufuli, anapewa nafasi ya kuwania tena Urais.

Kauli ya Bomboko inakuja ikiwa teyari kumekuwa na minong’ono ndani ya Chama hicho kuwa Membe ambaye alikuwa mgombea wa Urais wa ndani ya chama hicho,Mwaka 2015 ni wazi anataka kuchukua nafasi ya Urais 2020 na kumweka kando Rais Magufuli .

Kwa mujibu wa Bomboko kwenye kikao kitakachofanyka Dodoma Umoja huo hautakuwa na lengo jingine zaidi ya kumpitisha Rais Magufuli kuwania tena nafasi hiyo ya kukiongoza chama hicho kwenye uchaguzi wa awamu ya pili.

“Kama msemaji rasmi wa UVCCM, msimamo wa taasisi yetu ni kwamba hatuna na hatutakuwa na mchakato wa kumtafuta mgombea Urais 2020 mwingine zaidi ya Magufuli ambaye ndiyo Mwenyekiti wa CCM” amesema Hassan Bomboko na kuongeza;

“Mwaka 2020 tutakwenda Dodoma kwenye mchakato wa kidemokrasia Kukamilisha desturi yetu ya CCM ya kumbariki mgombea wetu kwa muhula wa pili, uchaguzi wa mgombea wa CCM tulishamaliza mwaka 2015.

“Kwa wenye nia ya kugombea Urais 2020 kupitia CCM watafute biashara nyingine ya kufanya kwani CCM hakuna Urais wa kupeana kiushemeji” ameongeza Hassan Bomboko.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.