AZAM FC KUIVAA LIPULI HII LEO, SAMORA

Na Shabani Rapwi.

Klabu ya Azam FC leo Jumatatu, Februari 11, 2019 itakuwa ugenini kukipiga dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utakaofanyika Saa 10: 00 Jioni Uwanja wa Samora, Iringa.

Azam FC leo itakosa huduma ya mlinda mlango wake namba moja Razak Abalora ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Alliance.

Timu hizo (Azam na Lipuli) zilikutana mara nne kwenye mechi za Ligi, katika mechi tatu zilizopita Azam FC ilishinda mara moja huku mechi mbili wakienda sare, mara ya mwisho kukutana kwenye uwanja wa Samora zilitoka suluhu.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), Azam FC ikiwa nafasi ya pili kwa alama 48 huku Lipuli FC ikiwa nafasi ya nne kwa alama 36.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.