MWAMUNYANGE ATEMBELEA MIRADI YA MAJI SAFI, AAGIZA WAKANDARASI KUTATUA KERO ZA WANANCHI

Dar es Salaam Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange ametembelea miradi ya maji safi inayotekelezwa na (DAWASA) kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake. Mwenyekiti wa Bodi ya DAWASA Jenerali Mstaafu Davis Mwamunyange akikagua miradi ya Majisafi ilipofikia  maeneo ya Salasala na Goba jijini Dar es salaam. Mwamungange ametembelea miradi hiyo iliyopo katika Manispaa ya ubungo na Kinondoni katika maeneo ya Bunju, Wazo ,Mwabepande, Goba , Changanyikeni na Kibamba Jijini Dar es salaam,. Aidha, amesema amefurahishwa na hatua ya miradi ya Majisafi ilipofikia nakuhimiza wakandarasi kuikamilisha kwa…

Soma Zaidi >>

WAJUMBE WA KAMAKA KATA YA MWANGATA WAAGIZA MBWA WANAOZAGAA MITAANI KUUWAWA.

Na Francis Godwin,Iringa KAMATI ya maendeleo la kata (KAMAKA) kata ya Mwangaka katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa kimemwagiza afisa mifugo wa kata hiyo kuendesha zoezi la kuua mbwa wote wanaozunguka mitaani ambao wamekuwa ni hatari kwa usalama wa wananchi wa kata hiyo . Agizo hilo limetolewa october 3,2018 wakati wa kikao cha kwanza cha KAMAKA kikiongozwa na diwani Edward Chengula mara ya kwanza toka ufanyike uchaguzi mdogo wa udiwani kufuatia kujiuzulu kwa madiwani watano akiwemo aliyekuwa diwani wa kata ya Mwangata kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo…

Soma Zaidi >>

MIONGONI MWA SABABU ZA UTORO NA UFAULU HAFIFU MASHULENI, WILAYA YA MPWAPWA HIZI HAPA

Mpwapwa -Dodoma Imebainishwa kuwa kutokupewa chakula cha mchana kwa wanafunzi Katika shule nyingi wilayani Mpwapwa ni miongoni mwa sababu zinazochangia utoro nmashuleni pamoja na ufaulu hafifu kwa wanafunzi. Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo kuwa la kiserikali la (MPWAGRISO) Dkt Geminisius Bahati Tungu, linaloshughulikia masuala ya maendeleo wilayani hapo walipo kuwa wakitoa taarifa ya utafiti wa masuala ya elimu. Dkt Tungu amesema kuwa, utafiti huo uliofanywa na kwa kushirikiana na shirika la Twaweza walilenga kuangazia katika mambo mkuu matano yanayohusu elimu. Aidha, amesema mambo yaliyo kuwa yanaangaziwa…

Soma Zaidi >>

RC SHINYANGA AZITAKA HALMASHAURI KUTENGA BAJETI YA UPATIKANAJI WA TAULO ZA KIKE MASHULENI.

Na Cleo : SHINYANGA. Mkuu wa mkoa wa Shinyanga  Bi. Zainab Telack  amewaomba wakurugenzi wote kwa kushirikiana na  na wenyeviti wa halmashauri zote pamoja na madiwani mkoani humo katika mwaka wa fedha kuhakikisha wanatenga bajeti kwa ajili ya kununua taulo za watoto wa kike ili kuondoa changamoto ya utoro mashuleni ambayo hujitokeza kipindi wanapokuwa katika  kipindi cha hedhi.    Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Bi: Zainab Telack akizungumza katika tamasha la jinsia ngazi ya wilaya kata ya Maganzo Wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga lililoandaliwa na Shirika la TGNP Mtandao Tanzania mwaka 2018.  Hayo yamebainishwa katika tamasha la jinsia…

Soma Zaidi >>

ACACIA KUTUMIA MILIONI 340 KUBORESHA ELIMU KANDA YA ZIWA

NA MWANDISHI WETU Kampuni ya uchimbaji wa madini Tanzania – Acacia inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi milioni 340 kwa kupitia mashindano ya mbio za baiskeli kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa elimu kwa jamii zinazozunguka migodi hiyo katika kanda ya ziwa. Meneja Uboreshaji tija kutoka Kampuni ya uchimbaji wa madini nchini Tanzania – ACACIA, Janeth Ruben (katikati), akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wa mashindano ya mbio za baiskeli zinazojulikana kwa jina la ‘Imara Pamoja Cycle Challenge’. Kulia ni Mshauri Mkuu wa Kitengo cha Jamii endelevu – ACACIA,…

Soma Zaidi >>