LEGAL SERVICE FACILITY (LSF) YAZINDUA KAMPENI MKOMBOZI KWA WANAWAKE NA MAKUNDI MBALIMBALI

Shirika lisilo la kiserikali la Legal Service Facility (LSF) linalofanya kazi ya kukuza upatikanaji wa haki kwa wote hasa kwa wanawake limezindua kampeni kwa jina la ‘Siyo tatizo tena’ yenye lengo la la kuongeza ufahamu kwa jamii kuhusu upatikanaji wa huduma za kisheria. Mkurugenzi mtendaji wa Legal Service Facility  (LSF) Kees Groenendijk akizungumza na waandishi wa habari juu ya kampeni ya ‘Siyo tatizo tena’ kwenye ofisi zao. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi zao zilizopo Mikocheni B mkurugenzi mtendaji wa LSF Kees Groenendijk amesema lengo kuu la kampeni ya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI DKT.KIGWANGALLA APASUA ANGA, ANADI VIVUTIO VYA UTALII NA UTAMADUNI VYA TANZANIA NCHINI UTURUKI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla (MB) ameongoza ujumbe maalum wa Tanzania kwenye mkutano wa tatu wa Dunia wa Utalii na Utamaduni, ambao ni mkutano wa juu zaidi wa sera za utalii unaofanyika kila mwaka. Katika mkutano huo wa siku tatu, Desemba 3-5, 2018,umeandaliwa kwa pamoja na mashirika ya Umoja wa Mataifa ya likiwemo Shirika linalosimamia Utalii (UNWTO) na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) ambapo Mawaziri na watunga sera zaidi ya 300 wanakutana jijini Istanbul, Uturuki, kuzungumzia mambo mbali mbali yanayohusu utalii wa utamaduni. Waziri Dkt.…

Soma Zaidi >>

RADI YAUA MKAZI MMOJA MKOANI LINDI

  Na Mwandae Mchungulike,Lindi Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Salima Ali Kolela (45) amefariki dunia jana desemba 3 baada ya kupigwa na radi akiwa nyumbani kwake katika kijiji cha Mbuli kata ya Kichonda wilayani Liwale mkoa Lindi. Jabili Mpako ambaye mume wa marehemu amesimulia jinsi tukio lilivyotokea amesema kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10 jioni wakati yeye anatengeza msala mara baada ya mvua kunyesha waliingia ndani aliporudi tena mlangoni mke wake ambaye marehemu alikuwa amembeba mtoto ndipo radi ilipompiga na kumtupa nje na kuanguka na kupoteza fahamu.…

Soma Zaidi >>

SUMA JKT YAAGIZWA KUKABIDHI JENGO LA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI DESEMBA 30

Na. Edward Kondela Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amemtaka mkandarasi SUMA JKT, aliyepewa kazi ya kujenga jengo la ofisi ya wizara hiyo katika mji wa serikali eneo la Ihumwa, Jijini Dodoma, kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati ifikapo Desema 30 mwaka huu. Akizungumza mara baada ya kufika katika eneo hilo, kukagua hatua za awali za ujenzi wa jengo la ofisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi, akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulika Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel pamoja na Katibu Mkuu Wizara…

Soma Zaidi >>

KAMPENI ZA UCHAGUZI MKUU NCHINI DRC ZAPAMBA MOTO, HALI NI PATASHIKA

Kinshasa, DRC. Kampeni za uchaguzi zinaendelea kushika kasi nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo ikiwa zimesalia wiki tatu kabla ya Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 23. Mgombea wa chama tawala, Bw Emmanuel Ramazani Shadary, anatarajia kujielekeza magharibi mwa nchi hiyo baada ya kufanya kampeni zake mashariki mwa nchi hiyo, huku upinzani nao ukipanga kuanza kampeni zake mashariki mwa nchi Aidha, wagombea wengi wa kiti cha urais wanaendelea kujiuzulu na kuwaunga mkono wagombea wa upinzani Felix Tchisekedi na Martin Fayulu. Jean Philibert Mabaya mgombea kiti cha urais kwa tiketi ya chama…

Soma Zaidi >>

PALESTINA:WANAUME WATANO NA MWANAMKE MMOJA WAHUKUMIWA KIFO KWA KUSHIRIKIANA NA ISRAEL

Gaza, PALESTINA. Mahakama ya kijeshi ya Gaza imewahukumu kifo wanaume watano na mwanamke mmoja kwa kushirikiana na nchi ya Israeli, mamlaka katika eneo hilo la Palestina linaloongozwa na kundi la Hamas imesema. Mwanamke huyo aliyehukumiwa kifo anaishi nchini Israeli na hakuwepo wakati wa kutolewa hukumu hiyo, hiyo ni kwa mujibu wa mamlaka huko Gaza. Mahakama ilitoa jumla ya hukumu 14 kwa ushirikiano na Israeli, na watu wengine nane wamehukumiwa kufanya kazi ngumu. Mamlaka inawashtaki kuhusika katika mlipuko ambao uliua maafisa sita wa Hamas mwezi Mei 2018 na kundi la Hamas…

Soma Zaidi >>

MAZUNGUMZO KUHUSU MZOZO WA KIVITA YEMEN KUANZA KESHO HUKO NCHINI SWEDEN

Stockholm, SWEDEN. Wajumbe wa waasi wa Houthi wanatarajiwa hivi karibuni kwenda huko Sweden, ambapo mazungumzo yanatarajiwa kuanza, kuanzia Jumatano ya kesho wiki hii, ili kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoikumba nchi ya Yemen. Afisa mmoja wa Houthi ameliambia shirika la Habari la Reuters kwamba, ujumbe wa waasi ulikuwa unatarajiwa kuondoka mji mkuu Sanaa juzi Jumatatu usiku au Jumanne ya jana asubuhi. Kwa upande wa Waasi wa Kishia wale wanaoungwa mkono na Iran, ambao wamekuwa wanadai kuwa baadhi ya wapiganaji wao waliojeruhiwa wasafirishwe kwenda nchini Oman ili waweze kushiriki mazungumzo,…

Soma Zaidi >>

DC LUOGA AANZISHA MICHEZO ILI KUTETEA UHURU WA MTOTO WA KIKE

Na Frankius Cleophace Tarime Mkuu wa wilaya ya Tarime  Glorious Luoga ameanzisha bonanza la Michezo mbalimbali huku kauli mbiu ikiwa ni kutetea na kulinda haki za mtoto wa kike ambapo timu 12 za mpira wa miguu kwa wanaume zinashiriki pia na timu Nne za Wanawake zinashiriki mpira wa miguu katika viwanja vya Chuo cha Ualimu TTC Mjini Tarime. Luoaga amesema kuwa katika wilaya ya Tarime mwanamke amekuwa hakinyimwa uhuru pamoja na mtoto wa kike hivyo kupitia michezo hiyo mashirika na wadau mbalimbali wa kupinga ukatili wa kijinsia watatumia michezo hiyo…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YAOMBWA KUWEKA JICHO LA PEKEE KUNUSURU ZAO LA NGOZI

Umoja wa Wataalam Wasaidizi Tanzania (TAVEPA), umeiomba Serikali kuweka mkakati wa makusudi wa kunusuru zao la ngozi kwa kuwa sasa hivi hakuna soko la uhakika la zao hilo. Mwenyekiti wa (TAVEPA) Bw. Salim Msellem, alisema hayo leo (03.12.2018) Jijini Arusha wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 14 wa wataalam wasaidizi wa afya ya mifugo nchini. “Ngozi nyingi hutupwa, kitu ambacho kinaletea hasara taifa kwa kukosa fedha za kigeni, pia kudhoofisha uchumi wa mfanyabiashara mmoja mmoja wa ngozi hapa nchini,” alisema Bw. Msellem. Alisema pia lazima kuwe na mkakati wa dhati…

Soma Zaidi >>

ACT WAZALENDO WAIBUA MAPYA SAKATA LA KIKOKOTOO KIPYA CHA MAFAO

Sakata la kikokotoo kipya cha mafao limeendelea kuchukua sura mpya baada ya Chama cha ACT Wazalendo kuitaka serikali kurudisha kikokotoo cha zamani. Hayo yamesemwa leo wakati mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo Yeremia Maganja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho Kijitonyama na kuitaka serikali kutumia kanuni ya kikokotoo cha mafao ya zamani ili wastaafu waweze kujikimu kimaisha na kupata mikopo kupitia akiba ya mafao yao. “Kuyapunguza mafao yao ya mkupuo mpaka asilimia 25 ni kuwaondolea haki hii ya kuweza kuwa na mikopo ya nyumba,…

Soma Zaidi >>