KERO YA USAFIRI WA MELI KUPUNGUA.

Ujio wa Meli mpya ya safari za Baharini umeleta matumaini mapya kwa wasafiri wanaofanya safari za Dar es salaam na Zanzibar Meli hiyo mpya ya Kampuni ya Sea Star, ina uwezo wa kubeba Mizigo tani 1,400 na Abiria 1,500, imewasili Bandarini Zanzibar kwa ajili ya kuongeza huduma za usafari wa Baharini katika mwambao wa Bahari ya Afrika Mashariki Hivi karibuni kumekua na ongezeko kubwa la wanaofanya safari za Baharini, hususani safari za Dar – ZNZ, ambapo awali ilikua unafika Bandarini kukata tiketi na kusafiri Siku hiyo hiyo. Hivi sasa hali…

Soma Zaidi >>

WAJUMBE WAPYA KAMISHENI YA UTUMISHI WA UMMA WAAPISHWA.

Zanzibar, Mjini. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti Wa Serikali Ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein, jana amewaapisha wajumbe wapya wa Kamisheni ya Utumishi wa Umma Zanzibar. Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu mjini Zanzibar ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Dk. Abdulhamid Yahya Mzee, Washauri wa Rais, Naibu Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Mzee Ali Haji. Wajumbe walioapishwa katika hafla hiyo ni Dk. Mohamed Seif Khatib, Mbaraka Mohammed Abdulwakil na Sheikh Hassan Othman Ngwali. Wengineo ni Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar, Sheikh…

Soma Zaidi >>

JESHI LAAMUA KULINDA VISIMA VYA MAFUTA KWA MANUFAA YA WALIBYA

Tripoli, LIBYA. Afisa mmoja wa Libya aitwaye El Manzar al Kharrtosh, ametangaza kuwa wanajeshi wametumwa katika eneo linalojulikana kama Hilali ya Mafuta huko kaskazini mwa nchi, ambalo lina visima vikubwa zaidi vya mafuta na bandari kubwa za mafuta za nchi hiyo ili kudhamini usalama wa eneo hilo. Afisa huyo anayehusika na masuala ya habari katika kikosi cha 73 cha wanajeshi watembeao kwa miguu chini ya kamanda mkuu wa vikosi vya ulinzi vya Libya, amesema kuwa brigedi ya 165 ya wanajeshi watembeao kwa miguu imetumwa katika eneo la Hilali ya Mafuta…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YACHUKIZWA NA WAFANYABIASHARA

Zanzibar, Mjini. Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 11 wa Jumuiya Ya Wafanyabiashara, Wenye Viwanda Na Wakulima Zanzibar (ZNCCIA). Uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip iliyopo Malindi mjini Zanzibar Makamu wa pili wa Rais, Balozi Seif alieleza, Serikali makini husisitiza umuhimu wa jumuiya ya Wafanyabiashara yenye kuleta manufaa na faida kwa kufungua milango ya biashara ndani na nje ya nchi Sambamba na kuongeza wigo wa pato la Taifa, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inachukizwa na kuona watu wachache wanaigeuza sekta ya biashara kuwa kichaka cha wakwepa kodi, wala…

Soma Zaidi >>

WANAFUNZI 12,399 WACHAGULIWA  KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2019 SIMIYU.

Simiyu. Jumla ya wanafunzi 12,399 mkoani Simiyu wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika shule za Serikali za kutwa na bweni kwa awamu ya kwanza. Hayo yalibainishwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu, Bw.Jumanne Sagini Desemba 14, 2019 wakati akitoa taarifa ya uchaguzi wa wanafunzi wa Kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 Mjini Bariadi. Sagini amesema jumla ya wanafunzi waliofaulu Mtihani wa Darasa la Saba ni 24,983 sawa na asilimia70.68 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani, ambapo amebainisha kuwa wanafunzi 12, 584 kati ya 24,983 waliofaulu hawajachaguliwa…

Soma Zaidi >>

SALUM MWALIM:OLENASHA ALIOMBE RADHI TAIFA.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Zanzibar Salum Mwalimu amemtaka naibu waziri wa elimu William Olenasha kujitokeza na kuliomba taifa radhi kutokana na kauli yake ya kuwa mawaziri hawaendi kwenye majimbo ya wapinzani(wahuni) Mwalimu ameyasema hayo mkoani Njombe wakati akizungumza na viongozi wa chama hicho mjini Njombe. “Juzi nimeona naibu waziri mmoja bila aibu anazungumza mambo ya ajabu eti pale nilikuwa siji mlikuwa mnanialika kwasababu mbunge wenu hapa alikuwa ni CHADEMA,Olenasha atoke aliombe taifa radhi unaibu waziri sio wakwake wala sio wa baba yake ni wa watanzania…

Soma Zaidi >>

FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO KUTUMIKA KATIKA MIRADI YA AFYA ELIMU NA UTAWALA MKOANI NJOMBE.

Na Emily Kilagalila,Njombe. Mbunge wa jimbo la Njombe kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM,Edward Mwalongo amesema fedha za mfuko wa jimbo kiasi cha shilingi milioni arobaini(40) zinaenda kuchangia miradi ya afya ,elimu na utawala jimboni humo. Akizungumza wakati wa ziara ya kamati ya mfuko wa jimbo iliyofanywa kwa lengo la kukagua na kupitisha miradi itakayosaidiwa na mfuko huo,Mwalongo amesema kuwa kiasi cha shilingi milioni 40 kitatumika kununulia vifaa vya ujenzi kulingana na mahitaji ya mradi husika na vitagawiwa kwenye Kata 13 za jimbo hilo ili kuweza kuchochea na kuchangia kasi…

Soma Zaidi >>

UFARANSA YAIKABIDHI JAMHURI YA AFRIKA YA KATI SILAHA ZA KIVITA ZAIDI YA 1,400

Bangui, AFRIKA YA KATI. Serikali ya Ufaransa juma hili imekabidhi bunduki zaidi ya elfu 1,400 aina ya AK-47 kwa vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Afrika ya Kati vinavyokabiliana na mashambulizi yanayofanywa na makundi yenye silaha. Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Florence Parly, alishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika kwenye kambi ya jeshi ya M’Polo iliyoko mjini Bangui. Msaada huu wa kijeshi ni sehemu ya ahadi ya Serikali ya Ufaransa iliyoitoa mwezi Novemba jijini Paris, sambamba na euro milioni 24 kama msaada wa kibinadamu. Maelfu ya raia wa Jamhuri ya Afrika ya…

Soma Zaidi >>

MAGAIDI 27 WAUAWA NA VIKOSI VYA ULINZI VYA MISRI HUKO SINAI

Cairo, MISRI. Vikosi vya ulinzi vya jeshi la Misri vimewauwa magaidi wapatao ishirini na saba (27) katika oparesheni maalumu iliyofanyika katika eneo la Sinai la Kaskazini mwa nchi hiyo. Kamanda mkuu ya vikosi vya ulinzi vya Misri jana alitangaza kuwa wanajeshi pamoja na wahandisi wa kijeshi walinasa na kuripua mabomu 344 ambayo magaidi walikuwa wameyatega ili kuwalenga askari jeshi na wale wa usalama wa nchi hiyo, na walifanikiwa kuangamiza maficho 342 ya magaidi huko kaskazini na katikati mwa eneo la Sinai. Idadi kubwa ya miripuko na silaha mbalimbali zilinaswa pia…

Soma Zaidi >>

MANISPAA YA UBUNGO KUJENGA OFISI ZA KISASA

Halmashauri ya manispaa ya Ubungo imesaini mkataba wa ujenzi wa ofisi za halmashauri hiyo za kisasa na wakala wa majengo nchini (TBA). Kutoka kushoto ni meneja wa TBA Dar es salaam Edwin Godfrey (katikati) meya wa manispaa ya Ubungo Boniface Jacob na kulia ni mkurugenzi manispaa ya Ubungo Beatrice Kwai wakisaini mkataba wa ujenzi wa ofisi za kisasa za manispaa hiyo. Ujenzi huo wa ofisi za kisasa ambao utagharimu jumla ya shilingi bilioni 6.2 utachukua muda wa mwaka mmoja hadi kukamilika kulingana na mkataba waliosaini leo kati ya manispaa ya…

Soma Zaidi >>