DKT. BASHIRU ASHAURI WAKUU WA MIKOA KUJIFUNZA SIMIYU

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa CCM Taifa, Dkt. Bashiru Ally amewashauri Wakuu wa Mikoa hapa nchini kwenda(kuja) kujifunza namna ya kufanya kazi kwa umoja na mshikamano kati ya Chama na Serikali sambamba na ubunifu na uchapakazi wa viongozi wa mkoa huo.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali, Mjini Bariadi wakati akiwa katika ziara yake mkoani Simiyu.   Dkt. Bashiru amewapongeza Viongozi wa Serikali wakingozwa na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,…

Soma Zaidi >>

DKT. BASHIRU AWAONYA VIONGOZI WALIOANZA KUTAFUTA UBUNGE KABLA YA WAKATI.

  Na Stella Kalinga, Simiyu Katibu Mkuu wa Chama cha Mpinduzi (CCM) Taifa Dkt. Bashiru Ally amewaonya baadhi ya Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Wakuu wa Taasisi na Mashirika ya Umma, ambao wameanza kukaa vikao kwa ajili ya kutafuta majimbo kabla ya wakati wa Chama hicho kutangaza mchakato wa kutafuta wagombea wapya wa ubunge na udiwani.   Dkt. Bashiru ameyasema hayo Januari 05, 2019 wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM pamoja na Viongozi na watendaji wa Serikali katika wilaya…

Soma Zaidi >>

MATINGA: UTAFITI KUONGEZA TIJA NA UZALISHAJI WA MADINI KWA WACHIMBAJI WADOGO

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Lilian Matinga amewataka wachimbaji wadogo kuachana na kutafuta na kuchimba madini kimazoea badala yake wafuate njia ya kisayansi katika kutafuta, kuchimba na kuchenjua madini katika maeneo yao ili kuongeza tija, pato lao na Taifa kwa ujumla. Aliyasema hayo Disemba 4 wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wachimbaji wadogo eneo la D reef na Kapanda Mkaoni Katavi, na kuongeza kuwa, masuala ya madini ni ya kisayansi na hivyo kuwataka wachimbaji wadogo kuondoa dhana mbaya iliyojengeka kwa…

Soma Zaidi >>

WATOTO WAOKOTWA UFUKWENI MTWARA WAKIWA WAMEFARIKI.

  Watoto wawili wakazi wa kijiji cha Mgao, Mkoni Mtwara wameokotwa wakiwa wamefariki Dunia pembezoni mwa mwambao wa Bahari ya Hindi. Uchunguzi wa Daktari imebainisha kuwa vifo hivyo vimetokana na watoto hao kukosa hewa baada ya kuzama kwenye maji. Kamanda wa Polisi mkoani Mtwara, Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi Blasius Chatanda amesema hii leo kuwa, tukio hilo la kuzama majini limetokea Januari Mosi katika kijiji cha Mgao ambapo uchunguzi wa awali unaonesha watoto hao hawakuwa na wasimamizi walipokwenda kuogelea. “Watoto hao tumeweza kuwatambua, wa kwanza alikuwa anaitwa Rajab Athman mwenye…

Soma Zaidi >>

MHE. MABULA ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA TENK NNE ZA MAJI ZENYE UWEZO WA KUHIFADHI LITA 3,300,000 NYAMAGANA.

  Haya yanebainishwa na Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula katika ziara yake MWAUWASA Mwanza Urbun Water Supply Supply and Sanitation Authority, Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Jijini Mwanza katika ukaguzi wa ujenzi wa tank nne za kuhifadhia maji zenye uwezo wa kuhifadhi Lita 3,300,000 zitakazo hudumia wakazi takribani 105,649. Mhe. Mabula amesema ukamilishwaji wa ujenzi tank hizi zilizopo Kata tatu za Halmashauri ya Jiji la Mwanza ikiwemo Kata ya Isamiro lilipo tank la Mji la Mwema lenye uwezo wa kubeba maji Lita 1,200,000, tank la maji…

Soma Zaidi >>

WANAWAKE TUMUOGOPE MUNGU,KUZAA MTOTO NA KUMTELEKEZA NI KUHATARISHA MAISHA YAKE.

  NGARA. Na Mwandishi wetu, Wanawake wameshauriwa kumuogopa mungu na sheria za nchi kwa kuepuka vitendo vya ukatili dhidi ya watoto baada ya kuwapata kwa kuwazaa kisha kuwaua au kuwatelekeza wakiwaacha mazingira hatarishi. Ushauri huo umetolewa na mmoja wa wafanyakazi wa benki ya NMB tawi la Ngara mkoani Kagera Witness Mwanga baada ya kuungana na wenzake kutembelea watoto yatima wa kituo ANGEL’S HOME kilichopo Kanisa katoliki la Rulenge wilayani Ngara. Witness Mwanga amesema kuzaa mtoto ni baraka hivyo mtoto anahitaji malezi, matunzo na kupewa haki zake za msingi kuliko kutupa…

Soma Zaidi >>

LUGOLA – ASKARI WANAOCHAFUA JESHI LA POLISI, WAKATAFUTE KAZI NYINGINE.

  Na Allawi Kaboyo – Bukoba Kagera. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Kangi Lugola, ameanza Rasmi ziara yake Mkoani Kagera ambapo amekutana na idara pamoja na taasisi zilizopo chini ya wizara hiyo, na kisha kufanya Mkutano wa hadhara katika viwanja vya mayunga mjini Bukoba sambamba na kusikiliza kero za wananchi. Mhe.Lugola katika hotuba yake iliyojaa ufafanuzi wa Utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya ccm unaofanywa na Mh. Rais John Pombe Magufuli, katika Kusimamia amani ya nchi na watanzania kwa ujumla, na kuwa Mh. Rais hapendi kusikia mwananchi…

Soma Zaidi >>

CCM YAITAKA AFRIKA IKATAE KUBURUZWA NA WAKOLONI WAPYA.

  Morogoro Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Morogoro kimesema vyama vya siasa katika mataifa yalioendelea havifanyi mikutano ya hadhara wala maandamano bila vibali mara baada ya chaguzi kuu kumalizika lakini inashashangaza mikutano hiyo ikishinikizwa ifanyike Barani Afrika. Kimeeleza maendeleo yaliopatikana Marekani na ulaya yangekawia mno iwapo wananchi wake wangepuuzia kazi za uzalishaji mali,kujiendeleza kielimu na kundekeza siasa kama inavyotakiwa ifanyike katika nchi za ulimwengu wa tatu . Msimamo huo ulitolewa jana na katibu wa CCM mkoa wa Morogoro Shaka Hamdu Shaka,kwa nyakati tofauti akiwa ameambatana na secretarieti ya CCM mkoa…

Soma Zaidi >>

DKT.BASHIRU ALLY ATOA SIKU TATU KWA UONGOZI WA KCU, WAWE WAMEWALIPA WAKULIMA WA KAHAWA FEDHA ZAO.

  Na, Mwandishi wetu, Kagera. Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi taifa Dkt Bashiru Ally amewapa muda wa siku tatu viongozi wa chama kikuu cha ushirika KCU (T)199 LTD Mkoani Kagera, kuhakikisha kinawalipa wakulima wa zao la kahawa fedha za awali kabla hawajachukuliwa hatua. Dkt Bashiru Ally ametoa maagizo hayo wakati akizungumza na wajumbe wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi kwenye kikao utendaji kazi kilichowahusisha wajumbe kutoka halmashauri za Biharamulo na Muleba. Amesema kuwa wapo baadhi ya wakulima wanadai fedha zao tangu msimu uanze Mwezi Mei mwaka huu hadi…

Soma Zaidi >>

OLE WAO WANAOHUJUMU MIUNDOMBINU YA UMEME – WAZIRI KALEMANI

  Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani jana (Desemba 29, 2018) amefanya ziara wilayani Kwimba, Mkoa wa Mwanza na kutoa onyo kali kwa watu wenye tabia ya kuhujumu miundombinu ya umeme pamoja na vishoka. Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vijiji vya Ngulla na Ibindo, akiwa katika ziara ya kazi kukagua utekelezaji wa miradi ya umeme, kuwasha umeme na kuzungumza na wananchi; Waziri Kalemani alitahadharisha kuwa serikali haitamvumilia yeyote atakayebainika kufanya hayo. “Mtu atakayebainika akikata nguzo, akiiba nyaya, akichezea transfoma kiasi cha kukosesha umeme wananchi, Mkuu wa Wilaya wa eneo husika…

Soma Zaidi >>