NANE WAUAWA KATIKA MAANDAMANO YA KUPINGA HALI MBAYA YA UCHUMI

Khartoum, SUDAN. Nchini Sudan watu wasiopungua nane (08) raia wa nchi hiyo, wameuawa katika ghasia na maandamano ya wananchi ya kupinga hali mbaya ya kiuchumi, ughali wa bidhaa na maisha magumu nchini humo. Maafisa wa serikali ya Sudan wametangaza usiku wa kuamkia leo kwamba, idadi ya watu waliouawa katika maandamano ya kupinga hali mbaya ya kiuchumi katika mikoa ya al Qadharif na Nahru Nil imefikia 8. Tangu Jumatano ya juzi miji mbalimbali ya Sudan ilishuhudia ghasia na maandamano makubwa ya wananchi anaopinga hali mbaya ya kiuchumi na ughali wa bidhaa.…

Soma Zaidi >>

MARAIS WAWILI WAJITANGAZA WASHINDI WA DURU YA PILI YA UCHAGUZI MADAGASCAR

Antananarivo, MADAGASCAR. Wagombea wawili wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Madagascar, ambao wamewahi kuwa marais wa kisiwa hicho, Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina, wamejitangaza washindi wa uchaguzi huo uliofanyika jana, licha ya Tume ya Uchaguzi kusema kuwa imehesabu asilimia tano tu ya kura kufikia sasa. Kwa mujibu wa tume hiyo, matokeo kutoka asilimia tano ya vituo vya kupigia kura yanaonesha kuwa Rajoelina anaongoza kwa asilimia 57 huku mpinzani wake, Ravalomanana akipata asilimia 43. “Tumeona matokeo, sio rasmi lakini ni sehemu ya matokeo hayo na yanaonesha kuwa Papa…

Soma Zaidi >>

KWA MARA NYINGINE MKUTANO WA MARAIS WA EAC WAFUTWA TENA

Arusha. Mkutano wa wakuu wa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambao ulikuwa umepangwa kufanyika jijini Arusha hapa nchini umefutwa kwa mara ya pili ndani ya wiki tatu. Mkutano huo wa marais wa nchi wanachama wa EAC ambazo ni Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi Sudan Kusini ulitazamiwa kufanyika Desemba 27. Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Christophe Bazivamo, amesema, “Ni rasmi sasa, mkutano huo hautafanyika Desemba 27 kama ilivyokuwa imepangwa. Tarehe na mahala pa kufanyika mkutano huo wa 20 wa wakuu wa EAC itatangazwa baadaye.” Kikao cha mawaziri…

Soma Zaidi >>

MMOMONYOKO WA MAADILI WATAJWA KUWA SABABU YA KUONGEZEKA UKATILI KWA WATOTO.

Na Amiry Kilagalila,Njombe. Utafiti wa mwaka 2009 unaonyesha kuwa asilimia 60% ya watoto wamefanyiwa ukatili wa aina mbali mbali ukiwemo wa kingono,wa kimwili au wa kihisia ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ukifanywa na wazazi hali inayopelekea kuwa na watoto wasio kuwa imara katika Taifa. Hayo yamezungumzwa na mkurugenzi msaidizi idara ya watoto bi.Grace Muwangwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo kwa wawezeshaji ngazi ya jamii kuhusu kitini cha elimu ya malezi kwa familia katika kuzuia ukatili dhidi ya watoto yaliyofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe na kujumuisha…

Soma Zaidi >>

SHIGONGO AIBUKA KWENYE SAKATA LA USHOGA,AKUBALI KUMUUNGA MKONO RAIS MAGUFULI

Dar es salaam. Mkurugenzi wa kampuni ya Global Publishers, Eric Shigongo ameshukia vikali barua ya maazimio 15 ya bunge la Umoja wa Ulaya kwa serikali ya Tanzania ambayo yanaonekana kuwa masharti magumu kwa taifa hasa suala la ushoga. Kupitia chapisho lake mtandaoni Shigongo amesema Umoja wa Ulaya umeweka masharti hayo magumu kwa kuwa Rais Magufuli amekuwa na misimamo thabiti juu ya rasilimali za taifa hasa pale alipozuia kusafirishwa kwa mchanga wa dhahabu (makinikia). >>Mimi nasimama na rais wetu, Dk. John Pombe Magufuli kuyapinga maazimio hayo kwani inaonesha wazi yamekuja kutokana…

Soma Zaidi >>

MBUNGE ZUNGU AWATAKA WANAWAKE ILALA KUCHANGAMKIA MIKOPO

Na Heri Shaban Dar es salaam Mbunge wa jimbo la Ilala Mussa Zungu,amewataka wanawake wa jimbo la Ilala kuchangamkia mikopo ya serikali isiyo na riba ambayo inatolewa na halmashauri ya manispaa ya Ilala. Zungu aliyasema hayo jijini Dar es Salam jana wakati wa kikao cha kufunga mwaka kinachoelezea maendeleo ya kata ya Upanga mashariki kilichoandaliwa na diwani wa kata hiyo Sultan Salim. “Serikali inatoa mikopo isiyo na riba,kwa watu watano watano na vikundi vilivyosajiliwa kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu”alisema Zungu. Aidha Zungu aliwaagiza maofisa maendeleo wa kata zote jimboni…

Soma Zaidi >>

DIWANI MNEMELE:MICHEZO ITUMIKE KUTOA MAFUNZO KWA VIJANA.

Na Stephen Noel,Mpwapwa. Jamii imeombwa kutumia njia za michezo katika kutoa mafunzo rika kwa vijana ili kuweza kuwafikia vijana wengi. Rai Hiyo imetolewa hii Leo na Pamela Mnemele diwani wa viti maluum tarafa ya Kubakwe wakati akifungua bonanza la michezo lililoandaliwa na shirika lisilo kuwa la kiserikali la TAYOA (Tanzania Youth Alliance) Jimbon Kibakwe. Bi Mnemele alisema kwa kutumia michezo kunaweza kuwavuta mabinti wengi kupata Elimu iliyo andaliwa kutokana na vijana wengi kuvutiwa na mchezo hivyo hurahisisha ujumbe kufika kwa kundi kubwa na kwa urahisi zaid tofauti na njia za…

Soma Zaidi >>

ASKOFU MENGELE:TUNGETENGENEZA KIZAZI CHA AJABU KUTOIMBA WIMBO WA TAIFA MASHULENI.

Na Amiry Kilagalila,Njombe. Askofu mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)jimbo la kusini Isaya Mengele amemshukuru Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli, kwa kutoa marekebisho juu ya matumizi ya wimbo wa taifa pamoja na rangi za bendera ya taifa. Askofu huyo ametoa shukrani hizo mbele ya mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri wakati wa mahafali ya kwanza ya chuo cha tumaini mkoani Njombe yaliyofanyika katika katika chuo hicho mkoani Njombe huku akimtaka mkuu huyo wa wilaya kuzipeleka shukrani za kanisa hilo kwa Rais.…

Soma Zaidi >>

NAIBU WAZIRI NISHATI ACHANGIA MIFUKO 50 YA SARUJI KUUNGA MKONO UJENZI KITUO CHA AFYA MSANGANI.

Pwani. Naibu waziri wa nishati ambaye pia ni mbunge wa viti maalumu mkoa wa Pwani Subira Mgalu amechangia mifuko hamsini ya saruji katika ujenzi wa kituo cha afya Msangani ikiwa ni kutimiza ahadi yake. Akiwa kwenye ziara ya ufuatiliaji wa miradi ya kimkakati katika halmashauri ya Kibaha amekabidhi mifuko hiyo ya saruji kwa uongozi wa Msangani ambao ndiyo unaosimamia ujenzi huo mbele ya mbunge wa Kibaha Mjini Silyvestry Koka, Mhe.Mgalu amepongeza wananchi wa maeneo hayo kwa kujitolea kwenye shughuli za kimaendeleo hasa kwa ujenzi wa kituo cha afya ambapo ukikamilika…

Soma Zaidi >>

MWANASHERIA MKUU KUKATA RUFAA DHIDI YA KUACHILIWA HURU DIANE RWIGARA

Kigali, RWANDA. Mwanasheria Mkuu wa Rwanda, Jean Bosco Mutangana, ametangaza mbele ya waandishi wa habari kwamba atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa Desemba 6 ulio muachilia huru mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame, Diane Rwigara na mama yake. Watuhumiwa hao wawili walikuwa wanakabiliwa na kifungo cha miaka 22 kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi pamoja na kughushi nyaraka. “Upande wa Mashitaka hauridhishwi na uamuzi wa mahakama, kwahiyo tumeamua kukata rufaa katika siku zijazo. Tulisoma kwa makini uamuzi wa Mahakama Kuu…

Soma Zaidi >>