WANANCHI IRINGA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA YA VIWANJA NDULI

Na Francis Godwin,Iringa. Mstahiki Meya wa Manispaa ya Iringa Alex Kimbe amesema halmashauri ya Manispaa ya Iringa imejipanga kuuza viwanja eneo la Nduli katika mji huo na kuwataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo. Kimbe amesema hayo katika mkutano wa mbunge wa jimbo la Iringa mjini mchungaji Peter Msigwa unaoendelea uwanja wa Mwembetogwa. Aidha amewataka machinga kulipa ushuru kwa ajili ya kuufanya mji kuwa katika hali ya usafi . Kuhusu mikopo kwa vijana na wanawake amesema zaidi ya milioni 144 zimetolewa na halmashauri kwa makundi hayo kupitia mapato ya ndani. Hata hivyo…

Soma Zaidi >>

ZIARA YA JPM TARIME YAZAA MATUNDA, MHE. MATIKO AMMWAGIA SIFA MAGUFULI

Tarime, MARA. Ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dakta John Pombe Magufuli, aliyoifanya mnamo Septemba 07 mwaka huu, mkoani Mara hususani wilayani Tarime, imezaa matunda mara baada ya kupatikana kwa utatuzi wa migogoro kadhaa ya ardhi, ukiwemo wa eneo la shule ya msingi Mturu na mwekezaji wa eneo hilo. Mapema wiki hii Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, alianza ziara wilayani Tarime, ambapo kulioneka kuwepo migogoro ya ardhi, baada ya mbunge wa jimbo hilo, Ester Matiko (Chadema), kuwasilisha kwa Rais Magufuli alipokuwa ziara…

Soma Zaidi >>

KALANGA AAPA KUTEKELEZA AHADI ZOTE JIMBO LA MONDULI

  Monduli,Arusha. Muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi katika kinyang’anyiro cha ubunge jimbo la Monduli,mbunge mteule Julius Kalanga, ccm,amewashukuru wananchi wote waliompigia kura na kumpa ushindi huo,huku akiahidi kuyafanyia kazi mambo yote ya msingi waliyokubaliana wakati wa kampeni. Akizungumza na waandishi wa habari,Kalanga amesema kuna mambo mengi atakayoyatekeleza lakini vipaumbele vyake kwanza ni maji ambapo amesema atahakikisha anashirikiana na serikali ili kuhakikisha jimbo hilo linapatiwa maji ya uhakika na kuondoa kero ambayo ni ya muda mrefu kwa wananchi hao. Aidha suala la migogoro ya ardhi,ni miongoni mwa mambo yanayowasumbua wananchi…

Soma Zaidi >>

KAMPUNI YA GREEN MILES YAAGIZWA KUINGIA MIKATABA NA VIJIJI VILIVYOPO KWENYE KITALU CHAKE.

Longido,Arusha. Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Longido limeaiagiza kampuni ya uwindaji ya Green Miles kuingia mikataba na wananchi waliopo katika vijiji vilivyopo katika kitalu chake. Maagizo hayo yametolewa 13 September 2018,wakati wa kikao cha kawaida cha madiwani hao. Baraza hilo la madiwani chini ya mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Sabore Molloimet na mkurugenzi mtendaji, Jumaa Mhina,limepokea Taarifa za Kamati za kudumu za halmashauri fedha,utawala na mipango, kamati ya elimu, afya na maji, Kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira na Kamati ya kudhibiti Ukimwi ambapo masuala mbalimbali yamejadiliwa ikiwemo…

Soma Zaidi >>

ALIYOYASEMA LISSU BAADA YA HOTUBA YA PROF KABUDI BUNGENI JUU YA RAIS KUTUNGA SHERIA

Leuven, UBELGIJI. Hotuba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamaganda Kabudi, aliyotolewa bungeni juu ya masuala mbali mbali ya kisheria na kikatiba, imemuibua Rais mstaafu wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) Mheshimiwa Tundu Lissu ambaye yuko Ubelgiji kwa matibabu. Mh Lisu amesema kuwa, amevutiwa na alichokisema juu ya mamlaka ya Rais ya kutunga sheria na hicho ndicho hasa kimemfanya azungumze kwa ufupi na hiki ndicho alichosema. “Profesa Kabudi ni bingwa wa kuchapia, hasa kwa watu wasiomuelewa au walio wavivu wa kusoma au wenye uelewa wa juu juu, hasa wa…

Soma Zaidi >>

RC CHALAMILA: WATUMISHI ACHENI SIASA MNAPOTEKELEZA MAJUKUMU YENU

Na Prakseda Mbulu, Mbeya. Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amewataka watumishi wa umma kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi na kutokuwa sehemu ya washabiki wa kisiasa kwa kupotosha jamii. Kauli hiyo, ameitoa wilayani Kyela 10 September 2018 wakati akizungumza na watumishi mbalimbali wa halmashauri hiyo na taasisi za umma kwenye ziara ya kujitambulisha. Amesema kuwa, mtumishi wa umma hatakiwi kuwa sehemu ya vyama vya siasa kutokana na kuwa anaongozwa na kanuni, Sheria na taratibu ambavyo vimemnyang’anya uwezo wa kuipinga Serikali badala yake kuwa mshauri wa Serikali katika shughuli za…

Soma Zaidi >>

RAIS BASHIR AVUNJA BARAZA LA MAWAZIRI ILI KUIKOMBOA SUDAN KIUCHUMI

  Khartoum, SUDAN. Sudan imempata waziri mkuu mpya, baada Rais Omar la Bashir kuvunja Baraza lake la Mawaziri kama hatua ya kukabiliana na mzozo wa kiuchumi uliokumba nchi yake katika miezi ya hivi karibuni. Hali hiyo ilisababishwa na hatua ya serikali ya kuondoa ruzuku ya chakula, pamoja na kushuka kwa Sarafu ya Sudan ambako kumesababisha ugumu katika kununua ngano nje ya nchi na bidhaa nyingine. Motazz Moussa, ambaye alikuwa Waziri anayeshughulikia masuala ya umeme na umwagiliaji, ameteuliwa kushika nafasi ya Bakri Hassan Saleh, aliyechaguliwa kuongoza nafasi ya waziri mkuu tangu…

Soma Zaidi >>

DC MURO AMALIZA MGOGORO WA ARDHI KATA YA AMBURENI

  Arumeru. MKUU wa Wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro amemaliza Mgogoro wa Ardhi wa Kata ya Ambureni,uliosababishwa na wanakijiji cha Shangarai waliotaka ardhi kwaajili ya kuweka huduma za jamii waliyopewa na mwekezaji Machumba Coffee estate kuona wenzao wamevamia eneo hilo na kufanya shughuri zao za kilimo kwa kupanda migomba na mazao mengine, Awali baadhi ya wananchi wasiozidi kumi (10) wa Kijiji cha Shangarai walikuwa wakilitumia eneo hilo kwa maslahi binafsi kwa kupanda migomba hatua iliyowakera wananchi zaidi ya elfu kumi (10,000) wa kata nzima ya Ambureni ambao baadhi yao waliamua…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI AMNG’OA PROF. MWANDOSYA, WASIRA ACHUKUA NAFASI YAKE

Ikulu Mdogo Bariadi. Siku ya leo Septemba 9, 2018, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli amefanya teuzi mbili ambazo zinawahusu kada wa muda mrefu wa CCM, Stephen Masato Wasira, na aliyewahi kuwa mbunge wa Magu Dkt. Festus Bulugu Limbu. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, ndugu Gerson Msigwa, Rais Magufuli amemteua Stephen Masato Wasira kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, ambapo anachukua nafasi ya Prof. Mark James Mwandosya. Kwa upande wake Dkt. Festus Bulungu…

Soma Zaidi >>