BACHELET AWAONYA CHINA, MAREKANI, SAUDI ARABIA NA UMOJA WA ULAYA

New York. Mkuu wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Michelle Bachelet, ameitolea wito China kuruhusu waangalizi kuingia nchini humo kufuatia taarifa za kutisha kuhusu watu kutoka jamii ya Wawghur wanaozuiliwa katika kambi zisizojulikana katika mkoa wa Xinjiang. Rais huyo wa zamani wa Chile, ametoa wito huo alipokuwa akitoa hutuba yake ya kwanza mbele ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, na kutangaza kuwa kuna timu ambazo zinatarajiwa kutumwa nchini Austria na Italia kuhusu kwalinda wahamiaji. Bi Bachelet amesema pia ana wasiwasi kwamba watoto…

Soma Zaidi >>

RAIS MUSEVENI AKANUSHA KUWATESA WANASIASA WA UPINZANI

Kampala, UGANDA. Nchini Uganda Rais wa Yoweri Museveni amekanuusha madai ya kuwatesa na kuwapiga wanasiasa na wapinzani na wafuasi wao katika operesehi ya kiusalama hivi karibuni, baada ya kuzuka kwa machafuko Kaskazini mwa nchi hiyo. Museveni amesema hayo alipokuwa akihutubia taifa kwa zaidi ya saa nne siku ya jana Jumapili Septemba 09 majira ya usiku. Kiongozi huyo ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1986, amevilaumu vyombo vya Habari nchini humo kwa kuripoti taarifa za uongo na kuwapotosha raia. Amewaelezea wanasiasa wa upinzani, Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, kama wanasiasa waliokosa…

Soma Zaidi >>

GESI BADO INA NAFASI KUBWA KATIKA KUCHANGIA PATO LA TAIFA – NAIBU WAZIRI

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, amesema kuwa gesi asilia inayopatikana nchini, ingali na nafasi kubwa ya kuchangia katika pato la taifa, tofauti na hofu ya baadhi ya watu kuwa Serikali haiipi tena kipaumbele sekta hiyo. Mhe. Mgalu alitoa kauli hiyo jana, Septemba 9, 2018 jijini Dodoma, wakati akijibu hoja za wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, walizoziwasilisha katika semina maalum iliyoandaliwa na wizara kuhusu masuala ya umeme, mafuta na gesi asilia. Awali, wakitoa maoni na hoja mbalimbali wakati wa semina hiyo, baadhi ya wajumbe…

Soma Zaidi >>

GAZETI LA TANZANITE LAMCHEFUA ZITTO, AAPA KUTOA FUNZO KWA WAHUSIKA

Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo ndugu Zitto Kabwe, ameonesha kukerwa na habari ya uongo na uzushi iliyochapishwa na gazeti la Tanzanite toleo la leo Septemba 10, 2018. Mbunge Zitto ametumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea masikitiko yake kufuatia habari katika gazeti hilo kusema ana mahusiano ya kimapenzi na aliyekuwa mke wa marehemu Deo Filikunjombe, habari ambayo amekanusha vikali na kusema marehe Filikunjombe alikuwa ni zaidi ya rafiki kwake. “Deo alikuwa zaidi ya rafiki yangu, tangu hajafa uzushi wa gazeti la Tanzanite, kama…

Soma Zaidi >>

DC MURO APIGA MARUFUKU MGAMBO KUNYANYASA WAFANYABIASHARA NDOGO NDOGO WILAYANI ARUMERU

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhe Jerry Muro amewaondoa askari wa jeshi la akiba (mgambo) waliokuwa katika soko la Tengeru kutokana na mgambo hao kutuhumiwa kunyanyasa wafanyabiashara  ndogo ndogo wakiwemo kina mama wanaouza bidhaa mbalimbali sokoni hapo. Dc Muro ambae alifanya ziara ya kustukiza sokoni hapo amesikiliza kero mbalimbali zikiwemo za kuporwa bidhaa zao na kuvunjiwa mbao wanazotumia kupanga bidhaa zao jambo linalowapa wakati mgumu wa kufanya biashara zao ambazo wamekuwa wakizitumia kuongeza vipato na kuhudumia familia zao. Kutokana na malalamiko hayo DC Muro amelazimika kuwaondoa mgambo hao kupisha uchunguzi…

Soma Zaidi >>

MANISPAA YA UBUNGO YAPATA NAIBU MEYA, MKURUGENZI ATOA SOMO.

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo iliyopo mkoani Dar es Salaam, siku ya jana Septemba 6, 2018 imefanya uchaguzi wa Naibu Meya wa Manispaa kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2018/2019. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Habari na Uhusiano, Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, uchaguzi huo umefanyika katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo uliopo Kibamba CCM, ambapo wagombea wawili, Mhe. Paschal Manota ambaye ni diwani kata ya Kimara kupitia CCM na Mhe. Ramadhan Kwangaya ambaye ni diwani wa Manzese kupitia CUF walijitokeza…

Soma Zaidi >>

DC MWAIMU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA KATA, VIJIJI NA VITONGOJI.

Mkuu wa wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, Bw. Rashid Mohamed Mwaimu amefanya kikao cha pamoja na viongozi wa kata zote, vijiji pamoja na vitongoji ndani ya wilaya yake. Mheshimiwa Mwaimu amekutana na viongozi hao mapema siku ya jana Septemba 5, 2018, ambapo alitumia fursa hiyo kusikiliza kero mbalimbali pamoja na changamoto zinazokwamisha kukamilika kwa miradi mbalimbali wilayani humo. Kikao hicho kimefanyika baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea katika kata hizo ili kujiridhisha na hatua zinazochukuliwa katika utekelezaji wa miradi hiyo sambamba na thamani ya pesa (value of money)…

Soma Zaidi >>

DC MWAIMU AKAGUA UJENZI WA ZAHANATI KATA YA KAMULI – KYERWA.

Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa, Bw. Rashid Mohamed Mwaimu amefanya ukaguzi katika mradi mkubwa wa ujenzi wa zahanati unaoendelea katika Kata ya Kamuli. Mheshimiwa Mwaimu amefanya ziara hiyo mapema siku ya jana Septemba 5, 2018, ambapo ameonekana kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo. Aidha, Mheshimiwa Mwaimu ametaka jitihada za ziada kufanyika ili kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili kusaidia kupunguza changamoto za afya katika wilaya hiyo. Mradi wa ujenzi wa zahanati ya Kamuli ni kati ya miradi mikubwa inayoendelea katika wilaya ya Kyerwa, ambapo endapo utakamilika thamani…

Soma Zaidi >>