ELIMU BURE YA WAFIKIA WAADZABE NA WATATOGA.

  Na Mariam Mallya. Wizara ya elimu kupitia Maafisa elimu ngazi ya wilaya na kata mkoani Arusha wametembelea jamii ya Waadzabe na Watatoga lengo ikiwa nikutoa fursa ya elimu kwa jamii hizo. Bw.Gift Kyando ni Afisa Elimu Mkoa wa Arusha alizungumza na jamii Hiyo na kusema kuwa serikali itaendelea kuweka mazingira rafiki katika sekta ya elimu japo changamoto ni kubwa. “Lengo ni kuwaamasisha na kuwatoa watoto wote ili wapate elimu sio wazima tu waviungo hata wale wenye mahitaji maalumu, Tunashukuru wameweza kupokea kwa mtazamo chanya na kuonyesha ushirikiano japo kimsingi…

Soma Zaidi >>

LUGOLA AKABIDHIWA KIJITI NA MWIGULU

Waziri Mpya wa Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi Mhe.Kangi Lugola amekabidhiwa ofisi na Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Lameck Nchemba katika Makao Makuu ya nchi Jijiji Dodoma leo Jumanne, Julai 10, 2018. Katika ukurasa wake wa Twiter, Mwigulu ambaye pia ni Mbunge wa Iramba Magharibi ameandika; “Makabidhiano ya ofisi/kijiti hii leo Dodoma. Nimemtakia kila raheli Mh.Kangi Lugola katika utumishi wake kwa watanzania katika wizara hii.” Aidha Nchemba mara baada ya kuenguliwa nafasi hiyo alifika jimboni kwake na kuongea na wananchi wake akisema kuwa sasa…

Soma Zaidi >>

WAZIRI ALIYESIMAMIA MCHAKATO WA UINGEREZA KUJIONDOA EU (Brexit) NA NAIBU WAKE WAJIUZULU

  Waziri wa masuala ya Uingereza kujitenga na Umoja wa Ulaya maarufu kama “Brexit”, ambaye pia ni Mjumbe mkuu wa Uingereza katika mazungumzo ya nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, David Davis, amejiuzulu. Usiku wa kuamkia leo Davis alijiuzulu pamoja na Naibu wake, kwa sababu alitofautiana na msimamo wa serikali yake ambao baraza la mawaziri lilikubaliana nao siku chache zilizopita. Kwenye barua yake ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Theresa May, Davis amesema sera na mbinu zilizoko kwa sasa, zinaifanya Uingereza kuwa na nafasi ndogo au haitajitenga na umoja wa…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AREJESHA MAHUSIANO YA KIDIPLOMASIA & KIBIASHARA NA ERITREA

  Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, wiki hii aliwasili nchini Eritrea katika ziara yake ikiwa ni baada ya mwezi mmoja kuyatambua kikamilifu makubaliano yaliyomaliza vita vya mpaka baina ya nchi hizo ndugu, ambavyo vilidumu kwa miaka miwili. Kiongozi wa muda mrefu wa Eritrea Isaias Afwerki alimkaribisha Abiy katika uwanja wa ndege wa Asmara kabla ya kuelekea katika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo yaliyodumu siku nzima. Kuwasili kwake kumeonyeshwa moja kwa moja na televisheni ya taifa ya Eritrea, na kundi kubwa la watu lilionekana limevalia fulana zenye picha za viongozi…

Soma Zaidi >>

ZAIDI YA MAGARI 200 YAFANYIWA UKAGUZI ARUSHA

  Na Mariam Mallya Jeshi la polisi mkoani Arusha limefanya ukaguzi wa mabasi yaendayo mikoani na malori ikiwa ni sehemu yakupunguza ajali za barabarani. Ili kuzuia hali hiyo jeshi la polisi mkoa wa Arusha likiongozwa na kamanda wa jeshi Ramadhani Ng’azi alie ambatana na mkuu wa kikosi cha usalama barabarani arusha leo alfajiri limefanya ukaguzi wa magari kwa lengo la kutoa elimu ili kuwa chachu ya kupunguza ajali. “Tumeweza kubaini baadhi ya madereva hawana leseni ama leseni zao walishapigwa faini bado hawajazilipia na pia Magari mabovu yote tumesitisha safari zao…

Soma Zaidi >>

ACT WAZALENDO YATANGAZA MSIMAMO WAKE UCHAGUZI MDOGO UJAO

Chama cha ACT-wazalendo kimetangaza kushiriki Uchaguzi wa Marudio wa Kata 79 pamoja na uchaguzi katika Jimbo la Buyungu ambapo uchaguzi huo Utafanyika mwezi ujao. Pia Chama hicho kimetangaza kushirikiana na Vyama vya Upinzani katika marudio ya Uchaguzi ili kuhakikisha wanaibuka na ushindi. Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam,na Makamu Mwenyekiti wa Chama chama hicho upande wa Bara,Shaaban Mambo wakati akisoma msimamo wa Kamati kuu ya chama hicho iliyokutana jana ambapo pamoja na mambo mengine wamejadili jinsi ya kushiriki uchaguzi huo. Amesema Katika kamati hiyo viongozi wameamua kwa kauli moja…

Soma Zaidi >>