POCHETTINO, ZIDANE WANAONGOZA MBIO ZA KUMRITHI MOURINHO

Klabu ya Manchester  Utd imeendelea kufanya vibaya kwenye michezo ya hivi karibuni tetesi za Mourinho kuondoka klabuni hapo zimezidi kupata uzito katika vyombo vya habari licha ya Jose Mourinho mwenyewe kusema bado ana mahusiano mazuri na mabosi wa klabu hiyo na wala hafikiri kuondoka klabuni hapo kwa sasa labda ingekua klabu nyingine. Watu ambao wamekua wakipewa nafasi kubwa sana kumrithi Jose ni Pochettino, Zidane, Conte, Carrick na Wenger. MAURICIO POCHETTINO. Huyu ni kocha wa Tottenham kwa sasa ambae anapewa nafasi ya kwanza kabisa. Pochettino aliiongoza klabu yake usiku wa jana ilipoipa…

Soma Zaidi >>

MOURINHO HALI TETE MANCHESTER UNITED.

  Jana katika dimba la Oldtraford klabu ya Manchester united walikuwa wenyeji wa klabu ya Tottenham katika mwendelezo wa ligi kuu nchini Uingereza . Manchester united wakajikuta wanapoteza mchezo mwingine ,wapili mfululizo baada ya juma lilipita kupoteza kwa idadi ya mabao 3-2 dhidi ya klabu ya Brighton ,Jana Manchester walijikuta wanapoteza mchezo mwingine kwa mabao 3-0 dhidi ya klabu kutokea jiji la London Tottenham . Manchester walianza mchezo kwa kasi kubwa wakionyesha matumaini ya kushinda mchezo lakini jitihada hazikuzaa matunda kwani walishindwa kufunga magoli licha ya kutengeneza nafasi kadhaa Kipindi…

Soma Zaidi >>

WCB WAITAWALA KENYA

Wasanii wanaotamba kwasasa kwenye tasnia ya muziki nchini Tanzania kutokea Wcb, wazidi kukumbiza tasnia hiyo kwa upande wa Afrika mashariki na kati ,Wcb  ambayo Iko chini ya msanii Diamond Platinumz  ,wakiwa na nyimbo yao mpya ambayo inajulikana kama Jibebe ,ndani yake wako Wasanii wote kutokea Wcb ,Diamond, Mbosso na Lavalava  imeshika nafasi ya kwanza kwenye nyimbo bora 20 zinazotamba nchini Kenya ,huku Jumla ya nyimbo tatu kutokea Wcb zikiingia 10 bora .

Soma Zaidi >>

SAMATA KAWASHA MOTO LIGI KUU NCHINI UBELGIJI

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samata ambaye anakipiga kunako klabu ya Genk nchini Ubelgiji jana ameisaidi klabu yake ya Genk kupata alama 3 na kujikita kileleni wakiwa na alama 13 baada ya michezo 5. Mbwana Samata alingia kipindi cha pili cha mchezo akitokea kwenye wachezaji wa akiba. Samata alitumia dakika chache kuisawazishia klabu yake bao na kufanya mchezo kuwa 2-2 ndani ya dakika ya 78 ya mchezo ulioikutanisha klabu ya Genk dhidi ya Klabu ya Beveren. Genk ndio walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya Ishirini kupitia kwa…

Soma Zaidi >>

MZIMU WA SARE WAITAWALA KLABU YA KMC .

  Ligi kuu Tanzania Bara imendelea Leo kwa michezo kadhaa katika viwanja vinne tofauti huku matokeo ya Sare yakiendelea kuitawala klabu ya Manispaa ya Kinondoni maarufu kama Kmc. Klabu ya Kmc ambayo inamilikiwa na halimashauri ya manispaa ya Kinondoni ,leo ilikuwa katika dimba la Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani ilikutana na klabu ya Ruvu Shooting ,mchezo ulimalizika kwa sare Pacha ya 1-1, huku klabu ya Kmc ikisawazisha bao lake kupitia kwa Mshambuliaji wao hatari Hassan Kabunda . Hii ni Sare ya pili kwa klabu hiyo wageni wa Ligi ya Tanzania Bara ,kwani…

Soma Zaidi >>

CHELSEA WAPATA USHINDI WA TATU MFULIZO LIGI KUU NCHINI UINGEREZA.

Klabu ya Chelsea leo jioni ilikuwa  kunako dimba la St James park kuwakabili wenyeji Newcastle united kwenye mwendelezo wa ligi kuu nchini Uingereza . Chelsea wakiwa na Mkufunzi mpya ,kwa mara ya kwanza wanafanikiwa kupata ushindi kwenye uwanja huo wa klabu ya Newcastle united. Chelsea walifanikiwa kutawala mchezo kwa vipindi vyote kwa kupiga Pasi nyingi ambazo Newcastle united walishindwa kuzuia,Chelsea walitumia  dakika 17 tu kupiga jumla ya Pasi 184 huku kiungo wao mpya Jorginho akipiga jumla ya Pasi zilikamilika 86 Ndani ya kipindi cha dakika 45 za Mwanzo . Chelsea walikuwa…

Soma Zaidi >>

HAZARD KUTUA MADRID?

Mabingwa wa Ulaya klabu ya Real Madrid imejipanga kutuma dau la mwisho kunako Klabu ya Chelsea  kuangalia uwezekano wa kukamilisha dili la uhamisho wa kiungo Mshambuliaji wa klabu ya Chelsea Eden Hazard . Awali klabu ya Madrid ilitenga jumla ya paundi Million 115 kupata  saini ya mbelgiji huyo. Eden Hazard bado ana mkataba wa miaka miwili na klabu ya Chelsea,huku mkufunzi wa klabu ya Chelsea muitaliano  Maurcsio Sarri akionyesha shahuku ya kumbakiza  Eden Hazard Chelsea. Klabu ya Chelsea imepanga kumpa Hazard kandarasi mpya ambayo atakuwa analipwa kiasi cha paundi 300k kwa…

Soma Zaidi >>

GOR MAHIA WABEBA UBINGWA KENYA

Klabu ya GOR Mahia ya nchini Kenya wametangzwa mabingwa wa ligi nchini Kenya maarufu kama Sports Pesa Premier League Gor Mahia wametangazwa kuwa mabingwa baada ya kuwafunga mahasimu wao AFC Leopards katika dimba la Karasai kwenye mchezo wa mahasimu unaojulikana kama MASHEMEJI DERBY. Mashabiki wengi wa AFC Leopards walipimga juu ya mahamuzi ya mwamuzi Felix Ekau ,kufanya fujo kipindi mchezo unaendelea na kung’oa viti ila haikusidia kuwazuia Gor Mahia kubeba kombe la ligi kuu nchini Kenya kwa mara ya 17 ,huku michezo 6 ikiwa imesalia. Baada ya mchezo kumalizika na…

Soma Zaidi >>

KOCHA WA JUVENTUS AMEOMBA MASHABIKI KUMPATIA MUDA RONALDO.

Klabu ya Juventus leo imecheza mchezo wake wa pili wa ligi kuu nchini Italia maarufu kama Sirie A na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, magoli ya Pranic  dakika ya 30 na Mario Madzukic  dakika ya 70 yalitosha kuipa ushindi klabu ya vibibi vya Turin Juventus. Wasiwasi mkubwa umetanda kwa mashabiki wa Juventus ju ya uwezo wa Ronaldo kufunga magoli kama alivyokuwa anafunga kunako klabu ya zamani ya Real Madrid kwani, tayari Ronaldo amechezea klabu Juventus jumla ya michezo miwili ya ligi kuu nchini Italia bila kufunga goli hata moja,…

Soma Zaidi >>

KOCHA NIGERIA AMTEMA JOHN OBI MIKEL

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Nigeria Maarufu kama Super Eagles ,Gernot Rorh ametangaza majina ya wachezaji ambao watajiandaa na mchezo wa kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika  mwakani. Akiwa ndani ya makoa makuu ya chama cha mpira nchini Nigeria jijini Logos  ,Rorh alitangaza majina ya wachezaji 23 ambao watakwenda nchini Shelisheli kucheza mchezo wa kufuzu kwa kombe la mataifa barani Afrika. Jina la Onyekuru likiwemo miongoni mwa majina 23, mshambuliaji wa Garatasaray ya nchini Uturuki Onyekuru hakuwemo kunapo kikosi cha timu ya Taifa ya Nigeria…

Soma Zaidi >>