MA- RPC WALIOTUMBULIWA NA LUGOLA BADO WANAENDELEA KUCHAPA KAZIā€¦WANASHERIA WASEMA WAZIRI HANA MAMLAKA KUWATENGUA.

Na,Mwandishi wetu. Licha ya kutangazwa kuondolewa kwenye nafasi yake na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha Ramadhani Ng’anzi ameendelea kufanya majukumu yake kama kamanda wa Mkoa wa huo. kupitia Mkutano wake na waandishi wa habari jana January 18,2019, RPC Ng’anzi alitangaza jeshi lake mkoani Arusha kuwakamata baadhi ya watuhumiwa kumiliki mitambo ya kujengea fedha bandia, hali ambayo imezua sintofahamu hasa kwenye mitandao ya kijamii. Ng’anzi alisema watuhumiwa wanne ambao hakuwataja majina yao kwa sababu za kipelelezi wanajihusisha na utengenezaji wa fedha…

Soma Zaidi >>

WAJASIRIAMALI NJOMBE WAPEWA DARASA KUFIKIA MAFANIKIO.

Na, Amiri kilagalila Wajasiriamali Mkoani Njombe wametakiwa kuzingatia kanuni za Kibiashara ikiwemo kulinda Mitaji yao ili kuhakikisha Mitaji inabaki salama bila kufilisika kutokana na Wajasiliamari wengi kufanya kazi Bila kuzingatia kanuni za Kibiashara na Mwisho hujikuta wamefilisika. Rai hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la General Bussness Company Limited Alexander Malya jana januari 17 alipokuwa akitoa Mafunzo ya Ujasiriamali katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe kwa baadhi ya wakazi Mjini Njombe ambapo amesema kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakishindwa kukua kutokana na Kutofuata kanuni za Kibiashara. Pamoja…

Soma Zaidi >>

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAKAA YA MAWE NA CHUMA LIGANGA KUANZA RASMI.

Na, Mwandishi wetu Wizara ya Madini imesema itashirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) kuweka msukumo ili kuhakikisha kwamba miradi ya Makaa ya Mawe Mchuchuma na ule wa Chuma Linganga inaanza kutekelezwa. Kauli hiyo ilitolewa Januari 16 na Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za madini mkoani Njombe na kuona namna ya kutatua changamoto zinazohusu Wizara ya Madini katika utekelezaji wa miradi hiyo. Alisema miradi hiyo ni moja ya miradi ya kimkakati ambayo Taifa linatarajiwa…

Soma Zaidi >>

SUALA LA POLISI KUWAVIZIA NA KUWAFUKUZA BODABODA KAGERA SASA BASI.

Na: Mwandishi wetu-Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti aweka wazi mikakati yake ya kuwafanya Waedesha Pikipiki maarufu kama Bodaboda Mkoani Kagera hasa katika Manispaa ya Bukoba kuwa mojawapo ya Utalii katika Mji wa Bukoba na bodaboda hao kufanya kazi zao kiueledi na kwa kuinua vipato vyao huku wakijishughulisha na ujasiliamali katika vikundi vyao. Ni baada ya Mkuu wa Mkoa Gaguti kukutana na Bodaboda katika Ukumbi wa Linas Night Club Manispaa ya Bukoba Januari 17, 2019 na kuongea nao ambapo aliweka wazi ni jinsi gani atahakikisha…

Soma Zaidi >>

WAJASIRIAMALI KATA YA MWANGATA IRINGA WAUNGA MKONO JITIHADA ZA JPM WACHANGIA MILIONI 2.

NA Francis Godwin,Iringa WAJASIRIAMALI wa kata ya Mwangata katika manispaa ya Iringa wamechanga jumla ya shilingi milioni 2 kwa ajili ya kumuunga mkono Rais Dkt John Magufuli kwa ajili ya uendelezaji wa sekta ya elimu nchini. Wajasiriamali hao ambao walitumia pesa hizo kununua mifuko ya saruji 130 walikabidhi msaada huo kwa naibu meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Lyata kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi Jana. Akizungumza kwa niaba ya wajasiriamali hao Diwani wa kata ya Mwangata Edward Chengula mara baada ya kongamano la wajasiriamali alisema…

Soma Zaidi >>

BABA MZAZI WA MSANII ALI KIBA AFARIKI DUNIA.

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Baba mzazi wa msanii wa Bongo Fleva, Alikiba Mzee Saleh amefariki dunia alfajiri ya leo Januari 17, 2019 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.. Inaelezwa kuwa, Mzee Kiba ambaye pia ni baba mzazi wa msanii Abdu Kiba na Zabibu Kiba amekua akiugua kwa muda sasa huku akiendelea kutibiwa. Msiba upo nyumbani kwa marehemu Kariakoo mtaa wa Muheza jijini Dar es salaam (unaingilia China Plaza) ambapo mipango ya mazishi inafanywa. Kwa mujibu wa Ndg wa Marehemu, ratiba ya Mazishi ni kwamba, Maiti itaswaliwa katika…

Soma Zaidi >>

MWANAFUNZI ALIYEBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI MWENZIE AKANA MAELEZO YA AWALI.

Na,Naomi Milton Serengeti Mathayo Songalaeli (21) mkazi wa kijiji cha Natambiso Wilaya ya Serengeti, amekana maelezo ya awali mara baada ya kusomewa maelezo hayo katika kesi yake ya Jinai namba 94/2018. Kabla ya kusomewa maelezo ya awali Hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya Ismael Ngaile alimtaka mwendesha mashtaka wa Jamhuri Faru Mayengela kumkumbusha mshitakiwa mashtaka yake. Akisoma mashtaka Faru alisema makosa yanayomkabili mshitakiwa ni mawili kosa la kwanza ni kubaka kinyume na kifungu 130(1)(2)(e) na 131(1)cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 Kosa la pili ni…

Soma Zaidi >>