SIASA ZAKWAMISHA UJENZI WA KITUO CHA AFYA HAMAI

Na,mwandishi Wetu Jumla ya milion 600 zilizotengwa kwenye  Mradi wa  ujenzi wa kituo cha afya Hamai wilayani chemba mkoani Dodoma  zimeshindwa kutumika ipasavyo kufuatia halimashauri kukosa wahandisi pamoja na kuchelewa kwa manunuzi ya vifaa vya ujezi na ufuatiliaji hafifu huku siasa zikichangia kwa kiasi kikubwa.   Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la ujenzi wa kituo hicho, Mganga Mkuu wa Wilaya ya chemba  Dk Olden Ngassa amesema moja ya changamoto imechangiwa na halimashauri kukosa wahandisi wa ujenzi kwa muda mrefu ambao ndio wasimamizi wakuu wa kazi za ujenzi pamoja na ushiriki…

Soma Zaidi >>

BILLIONI 5.4 KUJENGA MAGHALA MAKUBWA YA KISASA WILAYANI RUANGWA.

Na Bakari Chijumba, Mtwara. Utiaji wa saini kati ya Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa na Mkandarasi Tendar International Construction company limited, watakaotelekeza kandarasi yote ya ujenzi wa maghala ya kisasa wilayani Ruangwa Mkoani Lindi, umefanyika leo Jumatatu, 21 Januari 2019. Halfa fupi ya kusaini kandarasi hiyo imefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ambapo jumla ya majengo nane muhimu yatajengwa, likiwemo jengo la utawala, maghala mawili, Kantini, Majengo ya kupimia uzito, Mnara wa kuwekea matanki ya maji na jengo kuhifadhia vitu vya umeme, ambayo yote kwa pamoja yanatarajiwa kukamilika ndani ya…

Soma Zaidi >>

BARAZA LA MAWAZIRI LARIDHIA KUIFUTIA ZECO DENI LA VAT LA BILIONI 22.9

Baraza la Mawaziri limeridhia utozwaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa kiwango cha asilimia sifuri kwenye umeme unaouzwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa Shirika la Umeme la Zanzibar (ZECO) na kufuta malimbikizo ya deni la kodi ya VAT lililofikia shilingi Bilioni 22.9 kwa TANESCO kwenye umeme uliouzwa ZECO. Baraza la Mawaziri limefanya uamuzi huo leo tarehe 21 Januari, 2019 Ikulu Jijini Dar es Salaam, katika kikao kilichoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais…

Soma Zaidi >>

MIEZI MITATU MICHUNGU KWA TAKUKURU NJOMBE SASA IMEKWISHA.

Na Amiri kilagalila Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Njombe imefanikiwa kufuatilia na kukagua miradi mikubwa mitano ya maendeleo ukiwemo mradi wa maji wa Lugenge wenye thamani ya Tshs 3,642,817 355 bilioni. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kaimu Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Njombe Charles Mulebya Alisema Kuwa Takukuru mkoa ndani ya kipindi cha miezi mitatu ya Octoba hadi Disemba 2018 waliweza kufuatilia na kukagua miradi mikubwa mitano ya maendeleo kwa lengo la kuhakiki ubora na thamani ya fedha za umma. Mulebya alisema licha…

Soma Zaidi >>

VIONGOZI WA DINI WAPEWA SOMO.

Na,Danson Kaijage-Dodoma ASKOFU wa Jimbo la Dodoma kanisa la Mlima wa Moto,Silvanusi Komba amewataka viongozi wadini kuhakikisha wanawafundisha waumini wao juu ya kufanya kazi kwa bidii badala ya kufundisha masomo ya utoaji tu. Akihubiri katika ibada ya Jumapili askofu Komba alisema mwaka 2019 ni Mwaka pekee wa watanzania kutambua umuhimu wa kufanya kazi kwa bidii badala ya kukaa vijiweni na kuilalamikia serikali. Kiongozi huyo wa Kiroho alisema kuwa apendezwi kuona waumini wa kanisani lake kuendelea kulalamika kwa madai kuwa maisha ni magumu. Akiwahutubia maelfu ya waumini kanisani hapo alisema kuwa…

Soma Zaidi >>

TUNDU LISSU ADAI ANATAKA KUVULIWA UBUNGEā€¦SPIKA NDUGAI AKIRI LISSU NI MTORO NA ANAZURULA NJE YA NCHI.

Na,Mwandishi Wetu. Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, (Chadema), amedai kuwa kuna mkakati wa kutaka kumvua Ubunge kwa madai kuwa ni mtoro bungeni. Akizungumzia kwa undani mkakati wa kutaka kumvua Ubunge, kupitia waraka wake alioutoa, Lissu amedai kuwa kuna hoja inajengwa kuwa Mbunge huyo ni mtoro kwani hajaonekana Bungeni na hajamwandikia barua Katibu wa Bunge taarifa yoyote ya maandishi kuhusu kuumwa kwake wala matibabu yake. Mbunge huyo ameeleza kuwa hana sababu yoyote ya kutilia shaka taarifa hizi kwani waliomtonya ni watu wenye dhamana kubwa Bungeni na Serikalini ambao amedai hawaridhishwi…

Soma Zaidi >>

SHULE ILIYOATHIRIWA NA BOMU KAGERA YAJENGEWA MIUNDOMBINU.

Na,Mwandishi wetu-Ngara Taasisi ya Tumain Fund mkoani Kagera imetoa msaada wa vyumba viwili vya madarasa , ofisi ya walimu na madawati 30 vyenye thamani ya Sh76 milioni kwa shule ya msingi Kihinga wilayani Ngara ailiyoathiriwa na bomu Novemba 2017 na kusababisha wanafunzi watano kufariki na wengine 43 kujeruhiwa. Mratibu wa taasisi hiyo Alex Nyamkara akiambatana na Mwenyekiti wa mfuko huo Dkt Suzan Wilson kutoka nchini Uingereza wamekabidhi miundombinu hiyo leo kwa shule hiyo baada ya tukio la bomu lililoharibu madarasa manne. Nyamkara amesema licha ya vyumba hivyo, wakati wa tukio…

Soma Zaidi >>