ZANZIBAR WAADHIMISHA KUMBUKUMBU YA SIKU YA MAPINDUZI

RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein anahutubia taifa leo katika kilele cha miaka 55 ya mapinduzi matukufu kwenye Uwanja wa Gombani uliopo mjini hapa. Hotuba yake inahitimisha sherehe za mapinduzi ambazo zilianza kuadhimishwa tangu Desemba 31 mwaka jana kwa shughuli za kufanya usafi katika Wilaya za Pemba na Unguja huku akipokea maandamano ya wananchi na paredi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Kwa mujibu wa Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed viongozi wa kitaifa na wawakilishi wa nchi mbalimbali wanahudhuria…

Soma Zaidi >>

PAMOJA NA REKODI HIZI ZA KUTISHA SIMBA SC “YES WE CAN”

Wapinzani wa Simba kwenye mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika kundi D, timu ya JS Saoura ya Algeria wanatarajiwa kutua nchini kesho Alhamis tayari kwa mchezo huo utakaopigwa Jumamosi kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam. Katika mchezo huo, Simba inatakiwa kuutumia vizuri ili kuweza kupata alama 3 muhimu ambazo si rahisi sana kuzipata kwenye mchezo wa marejeano huko mjini Méridja Algeria kutokana na rekodi nzuri ya JS Sauora kwenye uwanja wao wa nyumbani maarufu kama ‘August 20, 1955’. JS Saoura waliweka rekodi ya kucheza mechi 58 kwenye…

Soma Zaidi >>

BENKI KUU YA TANZANIA YATOA MAAGIZO

BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imetoa tangazo kwa umma kupitia tovuti yake (www.bot.go.tz) likiwataka watu na taasisi zote zinazofanya biashara ya huduma ndogo za fedha zilizoko Tanzania Bara (isipokuwa vyama vya ushirika vya akiba na mikopo – SACCOS) kutoa taarifa zitakazotumika katika utayarishaji wa Kanuni za Usimamizi wa Huduma Ndogo za Fedha. “Bali ni kukusanya taarifa za awali kuhusu huduma hizo, kama amnavyo ilivyoainishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa kupitisha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, lengo la sheria hiyo ni kuwalinda wadau…

Soma Zaidi >>

‘YABAINIKA,MC PILI KUMBE DOMO ZEGE’

‛YABAINIKA, MC PILIPILI NI DOMO ZEGE’ Mchekeshaji maarufu na MC mwenye wasifu wake ulioshiba katika tasnia ya Burudani Tanzania Emmanuel Mathias almaarufu kama MC Pilipili alipiga hatua moja kuelekea kuuaga ukapera rasmi baada ya juzi kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake ambaye ni mke mtarajiwa wa mchekeshaji huyo ambaye ameteka soko kwa sasa katika mtindo wake wa vichekesho vya jukwaani maarufu zaidi kama standup comedy. Mchekeshaji huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu na aliyewahi kufanyia kazi kituo cha luninga cha Tv1 Tanzania alikamilisha zoezi hilo mbele ya umati wa watu ambao…

Soma Zaidi >>

UKIMSHIKA HAPA AUNT EZEKIEL USHAMMALIZA

SUPASTAA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel, amesema kama unataka kumjua upande wake wa pili wa shilingi, jaribu kuyafuatilia mapenzi yake na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ambaye ni dansa wa kutegemewa katika Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), utakiona cha mtemakuni. “Hivi kwa nini uhangaike kuyajua maisha yangu na mpenzi wangu? Leo tumegombana au tumepatana au tunaelekea kuachana, inakuhusu nini wewe? Maana hata tulivyoanza uhusiano watu walishtukizia tuko kwenye uhusiano hivyo hata kama tukiachana wataona hivyohivyo,” alisema wakati akizungumza na Ijumaa hivi karibuni. Aliongeza: “Nimekuwa nikisikia minon’gono mingi kuhusu kuachana…

Soma Zaidi >>

ALIKIBA KWENYE TUHUMA NZITO ZA WIZI

Msanii mkonge wa muziki wa Bongo Fleva, Domo Kaya amesema kuwa wasanii wapya kwenye muziki huo wanatakiwa kuwa wabunifu, baada ya msanii Alikiba kutumia kidokezo ‘Yebaba’ ambacho alikuwa alikitumia yeye mwanzo. Domo Kaya amefunguka hayo kupitia FRIDAY NIGHT LIVE ya EATV, ambapo amesema kuwa Alikiba kutumia neno hilo sio vibaya lakini alitakiwa kuomba ruhusa kwanza kwake. “Nawasihi wadogo zetu kuwa wabunifu, na kuacha ujanja ujanja maana kutumia kitu hukatazwi lakini uombe kwa muhusika akupe baraka zake”, amesema Domo Kaya. Hivi karibuni msanii Alikiba ameonesha kutumia msemo huo ‘yebaba’ katika wimbo…

Soma Zaidi >>

MWANAMKE AKIKUJIBU HIVI,KIMBIA HARAKA

Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu. KWA MFANO: 1. Ukimtumia sms ”Mambo mpenzi wangu?” akikujibu ”mambo mabaya”, usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ”sina hela dear” 2. Ukimtumia sms ”Maisha yanasemaje kipenzi changu” akikujibu ”maisha magumu hubby wangu we acha tu” usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini atakwambia ”nimefulia mwenzio kama nini sijui” 3. Ukimtumia sms ”Mbona…

Soma Zaidi >>

‘KUFURU NDOA YA DIAMOND NA TANASHA’

Mwanamuziki Diamond Platnumz na mwanadada Tanasha kutoka pande za Kenya wapo katika mahaba mazito kiasi kwamba wamekuwa wakifuatana kama kumbi kumbi kila mahali.Hali hiyo inaelezwa kwamba ni kutokana na kunogewa na utamu wa penzi lao ambalo bado ni change lakini likiwa na malemgo makubwa katika maisha yao ya baadae Diamond ambaye ni baba wa watoto watatu Tiffa na Nilan ambao kawapata akiwa na Zari na Mwingine Dylan ambaye kazaa na mwanamitindo ambaye pia ni mwanamuziki Hamisa Mobetto inaonekana kukolea vilivyo kwa binti huyo mkenya ambaye pia ana uraia wa Italia.…

Soma Zaidi >>

SHEPU YA HAMISA MOBETTO YAWA GUMZO MTAANI

SHEPU YA HAMISA MOBETO GUMZO MTAANI Mwaka 2018 ulikuwa ni mwaka ambao kulikuwa na mgawanyiko mkubwa katika mafanikio ya kimaisha ambapo watu wengi walionekana kutoufurahia kwa malalamiko ya vyuma kukaza wakimaanisha ugumu wa maisha kupitiliza tofauti na miaka mingine Kwa upande wa mastaa wa kiwanda cha Burudani hapa Tanzania kuna waliofanikiwa na kuna waliofeli katika mahangaiko yao.Ukiachilia mbali waliofeli kabisa Hamisa Mobeto ni miungoni mwa wasanii ambao walipitia vipindi vyote(kipindi kigumu na kipindi cha mafanikio) Kwa upande wa matukio yaliyomuumiza na kumvunja moyo bila shaka itakuwa ni kupoteza penzi lake…

Soma Zaidi >>

DUDU BAYA KUKICHAFUA WASAFI?

Godfrey Tumaini anayefahamika kwa jina la kisanii kama Dudu Baya (Konki Masta) ni miungoni mwa wasanii maarufu na wakongwe zaidi katika muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva),pia ni msanii miungoni mwa waanzilishi na wajenzi wa muziki huu ambapo alivuma sana miaka ya 2000 na ngoma zake kali kama nakupenda tu,Mpenzi,nimeondoka na nyimbo zingine kadha wa kadha ambazo zilimuweka na zinaendelea kumuweka kwenye ramani ya muziki mpaka sasa.Lakini nje ya muziki Dudu Baya amejiweka wazi kwamba ni mpinga ushoga namba moja akifikia hatua ya kutaja watu kadhaa ambao alisema wanajihusisha na…

Soma Zaidi >>