ALIYEWATAPELI WATALII DOLA 5000 AKAMATWA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam inamshikilia Omwailimu Sosthenes ambaye ni mmiliki wa kampuni ya Utalii ya  Arise Special Sunrise,kwa tuhuma za kuwatapeli watalii wawili Dola za kimalekani 5000. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum, DCP Liberatus Sabas, amesema mtuhumiwa huyo aliwatapeli watalii hao ambaye mmoja anaishi Marekani na mwingine nchini India kwa makubaliano kwamba angewapeleka safari ambazo walizipanga. Amesema baada ya mtuhumiwa huyo kuwatapeli wageni hao aliwatelekeza katika nyumba ya wageni maeneo ya Sinza na walipojaribu…

Soma Zaidi >>

RIEK MACHAR MBIONI KUREJESHEWA WADHIFA WAKE

Kiongozi wa kisiasa maarufu nchini Sudan Kusini na aliyekuwa Makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo, Riek Machar, atarejeshwa katika wadhifa wake kama sehemu ya makubaliano ya amani ya kuvifikisha mwisho vita vya karibu miaka mitano ambavyo vimewaua maelfu ya watu na kuliharibu kabisa taifa hilo changa barani Afrika. Makubaliano hayo yaliafikiwa katika mazungumzo ya mjini Entebbe, na yalisimamiwa na Rais Yoweri Museveni wa Uganda na kuhudhuriwa na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, Rais wa Sudan Omar al-Bashir na Machar. Taarifa ya ofisi ya rais ya Sudan Kusini…

Soma Zaidi >>

MAUZO DSE YAPOROMOKA

Mauzo ya Hisa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) yameshuka kutoka Sh bilioni 1.11 wiki iliyopita hadi Sh milioni 676.26 wiki hii. Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Biashara na Masoko, Emanuel Nyalali, amesema mauzo hayo yametokana na kuuzwa kwa mihamala 166. “Wakati huo thamani ya Soko la Hisa imeongezeka hadi kufikia Sh trilioni 22.18 kutoka Sh 21.99 wiki iliyopita,” amesema Nyalali. Aidha amesema katika kipindi hicho, hatifungani za serikali na makampuni zenye thamani ya Sh bilioni 1.96 ziliuzwa kwenye mihamala…

Soma Zaidi >>

Tundu Lissu atoa ujumbe mzito kuhusu afya yake

Kupitia ukurasa wake wa mtandao, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye anapatiwa matibabu nchini Ubeligiji aliandika; “Wapendwa wangu natumaini wote hamjambo asubuhi hii (angalau kwangu ni saa 12 kasoro ya asubuhi). Nawaomba msamaha kwa kuwaweka roho juu jana halafu sikuonekana. Nilipata wageni na by the time nimemalizana nao muda ulishaenda sana. Naomba nianze kwa kuwapa briefing ya afya yangu. Wengi wenu mtakuwa mmeona video clips nikifanya mazoezi ya kutembea. Clip hizo zinaonyesha naendelea vizuri na ni kweli. Operesheni ya mwezi uliopita imepona, angalau kwenye muscles. Mfupa bado una kazi…

Soma Zaidi >>

Kangi Lugola alivyomzuia Kamishina wa Magereza kuingia kwenye mkutano wake

Kamishina wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa amezuiwa kuingia kwenye mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola baada ya kuchelewa kwa dakika mbili kuingia kwenye ukumbi ambako mkutano huo ulifanyika. Waziri huyo ambaye aliingia kwenye ukumbi majira ya saa 4:51 asubuhi ambapo mara baada ya kuingia aliagiza kwamba ikifika saa 5:00 mtu ambaye atakuwa hajaingia ukumbuni hataruhusiwa kuhudhulia kikao chake isipokuwa waandishi wa habari. Ilipofika saa 5:00 aliagiza mlango ufungwe na usifunguliwe kwa mtumishi yoyote wa wizara wala Kamanda yoyote kuingia labda awe mwanahabari. Ambapo…

Soma Zaidi >>