TUNDU LISSU:HAKUNA MJOMBA AU SHANGAZI WA KUMLILIA, NI KUELEKEA MARUDIO YA CHAGUZI NDOGO-BUYUNGU

UBELGIJI.  Mbunge wa jimbo la Singida Mashariki mkoani Singida, Mheshimiwa Tundu Lissu, amesema kuelekea marudio ya chaguzi ndogo zinazotarajiwa kufanyika hivi karibuni ni fursa nyingine ya mlengo upinzani kuanika wazi utawala wa Rais Magufuli na hatua nyingine ya kupigania haki za Binadamu, utawala bora na demokrasia nchini Tanzania. Mh Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni(KUB), ameyasema hayo usiku wa kuamkia leo Julai 16 akiwa nchini Ubelgiji, anapoendelea kupokea matibabu baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi 38 hapo Septemba mwaka jana akiwa nyumbani…

Soma Zaidi >>

WORLD CUP-2018 FINAL:NANI ZAIDI BAINA YA UFARANSA ALIYESAHAU KIKOMBE HIKI KWA MIAKA 20 DHIDI CROATIA

MOSCOW. Leo ikiwa ni siku ya fainali za kombe la dunia kwa mwaka 2018, michuano ambayo ilikuwa ikichezwa nchini Urusi, ni watu wachache walitarajia wakati tamasha hilo kubwa la kandanda duniani lilipoanza wiki nne zilizopita. Croatia inachuana na Ufaransa mjini Moscow ikijaribu kunyakua taji la kombe la dunia kwa mara ya kwanza, huku kikosi cha kocha Didier Deschamps wa Ufaransa kinalenga kupata taji lake la pili, tangu 1998. Timu ya taifa ya Croatia imeleta furaha katika taifa hilo la Balkan ambalo lina Wakazi Milioni 04 tu kwa kwenda kinyume na…

Soma Zaidi >>

DIWANI-CHADEMA ATOA KADI ZA MATIBABU BURE KWA WAZEE KATIKA KATA YAKE

DAR-ES-SALAAM. Diwani wa kata ya Mtoni kwa tiketi ya CHADEMA na Makamu Makamu Mwemyekiti wa wa chama hicho Dar es salaam Kuu, Mheshimiwa Benard Mwakyembe, ametoa kadi za matibabu bure kwa wazee wa kata ya Mtoni. Hafla hiyo imefanyika leo Jumamosi Julai 14, 2018, akiwa na Katibu wa chama hicho wilaya Temeke, Jacob Mlay pamoja na viongozi wengine Akiongea katika hafla hiyo fupi Mhe. Mwakyembe amewaambia wazee muda kubeba makaratasi na kutumia mlolongo mrefu kupata matibabu umekwisha, na kuwahakikishia usumbufu waliokuwa wakiupata awali pia umefikia kikomo. “Kuanzia sasa matibabu nyie…

Soma Zaidi >>

RAIS SALVA KIIR WA SUDAN KUSINI AONGEZEWA MUDA KUBAKIA MADARAKANI

JUBA. Nchini Sudan Kusini Bunge la nchi hiyo, limepiga kura kurefusha muda wa Rais Salva Kiir kubakia madarakani kwa miaka mitatu zaidi hadi mwaka 2021, hatua ambayo bila shaka huenda ikatatiza juhudi za kuleta amani katika nchi hiyo changa duniani kwa kudhoofisha mazungumzo ya amani na makundi ya upinzani. Bwana Kiir amekuwa madarakani tangu Sudan Kusini ipate uhuru wake mwaka 2011 na uchaguzi wa mwaka 2015 nao ulihairishwa. Makundi ya upinzani nchini humo hivi karibuni katika siku za nyuma yalishutumu hatua kama hiyo kuwa inakwenda kinyume na sheria. “Mswada wa mabadiliko…

Soma Zaidi >>

NI ‘MNYAMA’ SIMBA ALIYESAHAU KOMBE LA KAGAME KWA MIAKA 16 AU AZAM FAINALI LEO

DAR-ES-SALAAM. Michuano ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati maarufu kombe la Kagame leo hii linafikia tamati kwa mechi mbili kupigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Lakini mechi ya fainali itakayowakutanisha Simba Sc na Azam Fc ndiyo itakayovutia zaidi kwani itakuwa ni ya historia kubwa kwa timu zote mbili. Mabingwa watetezi wa Kombe la Kagame Azam Fc watacheza mchezo wa fainali na Simba leo Ijumaa, baada ya timu hizo kushinda mechi zao za nusu fainali. Azam Fc inataka kutetea taji lake ililolitwaa mwaka 2015 hapa hapa jijini Dar…

Soma Zaidi >>

BODI YA MIKOPO -HESLB YAONGEZA MUDA WA KUTUMA MAOMBI MPAKA JULAI 31

DAR-ES-SALAAM. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB), Abdul-Razaq Badru, amesema kuwa Bodi ya Mikopo inapenda kuwataarifu waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2018/2019 kuwa imeongeza muda wa kutuma maombi kwa njia ya mtandao kwa wiki mbili kuanzia Julai 15, 2018. Hayo ameyasema leo Julai 13 katika taarifa kwa umma na waombaji na kuongezea kuwa tarehe ya mwisho ya kuwasilisha maombi kupitia mtandao wa HESLB (https://olas.heslb.go.tz ) itakuwa Jumanne, Julai 31, 2018. Vilevile ameelezea kuwa tarehe ya mwisho ya kutuma nakala ngumu kwa ‘EMS’…

Soma Zaidi >>

MWANAMKE MMOJA NA MTUHUMIWA WA KUNDI LA KIGAIDI NCHINI UJERUMANI AFUNGWA MAISHA

MUNICH. Nchini Ujerumani Mahakama moja ya mjini Munich imemhukumu kifungo cha maisha, Bibi Beate Zschaepe aliyekuwa mwanachama wa kundi la kigaidi la NSU lililokuwa linalojiita Wanazi mamboleo, ambaye ni mtuhumiwa mkuu katika kesi iliyohusu vuguvugu la chini kwa chini nchini humo. Mahakama ilitoa uamuzi huo leo hii Jumatano ambapo Bibi Zschaepe amepewa hukumu hiyo ya kifungo cha maisha. Mshtakiwa huyo amekutwa na hatia kuhusiana na maujai ya watu 10 wengi wao wakiwa ni wahamiaji wa Kituruki ambao waliuwawa kwa kupigwa risasi kati ya mwaka 2000 na 2007. “Kesi hii ilisababisha…

Soma Zaidi >>

UGANDA POLISI WATUMIA MABOMU KUWATAWANYA WAANDAMANAJI WA KUPINGA KODI YA MITANDAO YA KIJAMII

KAMPALA. Nchini Uganda Jeshi la polisi limetumia mabomu ya machozi leo kuwatawanya mamia ya waandamanaji katika mitaa mbalimbali, ambao walikuwa wanapinga tozo jipya la kodi kwa matumizi ya mitandao ya kijamii. Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti kuwa polisi pia walijaribu kumkamata kiongozi wa maandamano hayo Mwimbaji Robert Kyagulanyi, ambaye pia hujulikana kama “Bobi Wine”, Mbunge wa jimbo la Kyaddondo Mashariki kutoka wilaya ya Wakisso Mkoa Kati nchini humo lakini alifanikiwa kukimbia. Kodi hiyo iliyoanza kukatwa mwanzoni mwa mwezi huu, inamlazimu mtumiaji wa mitandao kama Facebook, WhatsApp Twitter na hata…

Soma Zaidi >>

MACHAR AGEUKWA NA WAASI WAKE, WAKATAA MAKUBALIANO YALIYOFIKIWA KUMREJESHA KATIKA WADHIFA WAKE

JUBA. Nchini Sudan Kusini kikundi cha Waasi kinachomuunga mkono aliyekuwa Makamu wa Rais wa zamani wa nchi hiyo, Riek Machar leo kimeukataa mpango wa amani ulioafikiwa wa kumrejesha kiongozi wao huyo kwenye umakamu wa rais, wakisema makubaliano hayo hayajapunguza mamlaka makubwa aliyonayo rais wa nchi hiyo, Salva Kiir. Machar alikuwa makamu wa Kiir hadi mwaka 2013, wakati tofauti za kisiasa zilipochochea vita ambavyo vimesababisha maafa makubwa nchini humo kwa miaka mitano. Makubaliano ya kumrudishia Machar wadhifa wa makamu wa rais yaliafikiwa mjini Entebbe, Uganda, mwisho wa wiki iliyopita chini ya…

Soma Zaidi >>