MEYA MANISPAA YA IRINGA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA

Na Francis Godwin,Iringa TAASISI  ya  kuzuia na kupambana na Rushwa  nchini (TAKUKURU) imemfikisha   mahakamani mstakihi   meya  wa  halmashauri ya  manispaa ya  Iringa Alex  Kimbe kupitia  chama  cha  demokrasia na maendeleo ( CHADEMA)   makosa  mawili  ya  jinai kuomba na  kupokea  rushwa . Kaimu  kamanda  wa  takukuru  mkoa  wa  Iringa  Mweli Kilimali   akizungumza leo na  vyombo  vya habari  ofisibni  kwake  alisema kuwa   meya  huyo alipokea kiasi cha  shilingi  milioni 2  kutoka kwa  mteja  wao . Alisema  kuwa  tukio  la kukamatwa meya  huyo lilitokea  Novemba  15  mwaka  huu majira ya saa 12  jioni …

Soma Zaidi >>

SHULE SUN ACADEMY ENGLISH MEDIUM IRINGA WAJIPONGEZA KUFANYA VIZURI ….

Na Francis Godwin,Iringa UONGOZI  wa    shule ya Sun Pre  & PRIMARY English Medium mkoani  Iringa  umewapongeza  wafanyakazi  wake  wakiwemo  walimu  kwa kuiwezesha shule  hiyo   kushika nafasi ya juu matokeo ya darasa la saba kitaifa. Mkurugenzi mtendaji  wa shule  hiyo  Edward  Nguvu  Chengula amesema  amelazimika kuwaandalia  sherehe maalum  ya  kuwatoa  nje ya  mji  wa Iringa wafanyakazi wake  kama sehemu ya  kuwapongeza  na  kujipongeza kwa  kuiwezesha shule hiyo  kuendelea  kufanya   vizuri . Chengula  alisema  matokeo mazuri ya  shule  hiyo  yamepelekea   wazazi  wengi  kutoka ndani ya mkoa na nje ya mkoa wa Iringa  kuhamisha …

Soma Zaidi >>

MEYA MANISPAA YA IRINGA ALEX KIMBE AWAACHA AWASHANGAZA MADIWANI ,AENDESHA BARAZA KWA DAKIKA 32

Na  Francis Godwin, Iringa KATIKA  hali  isiyoya kawaida   kikao  cha  baraza la madiwani  wa  Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa ambacho  kwa wiki  iliyopita  madiwani  wa chama  cha mapinduzi (CCM)  walisusia  kikao   hicho  leo  mstahiki  meya wa Halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa Alex Kimbe amewashangaza  wengi  baada ya  kuendesha  kikao  kwa  dakika 32  na  kugoma kusikiliza  hoja binafsi . Kikao   hicho  kilianza  saa 2.00  hadi saa 2.32  huku  madiwani  takribani 10 wa  chama  cha  demokrasia na maendeleo (Chadema)  wakiwa na ukumbini na CCM   akiwemo  diwani  mmoja pekee  na   naibu  meya  Joseph …

Soma Zaidi >>

WAZIRI KAMWELWE ATOA MAAGIZO MATANO TANROADS ,ASEMA HATAKUBALI KUTUMBULIWA NA RAIS JPM

Na Francis Godwin,Iringa WAZIRI  wa ujenzi ,uchukuzi na mawasiliano mhandisi Isack Kamwelwe  ametoa  maagizo matano kwa   mameneja  wa wakala  wa  barabara  chini  (TANROADS )   kutekeleza vinginevyo hatakubali   kutumbuliwa  na  Rais  Dkt  John  Magufuli kwa  kushindwa kazi. Akizungumza  jana  wakati wa  uzinduzi wa mkutano wa  11  wa wafanyakazi wa  TANROADS  nchini  uliofanyika   katika  ukumbi wa  kichangani  mjini  Iringa ,waziri   huyo alisema Rais Dkt  Magufuli hapendezwi  na  utendaji  uliochini ya  kiwango kwa  wateule  wake  wakiwemo  mawasili na  wengine  hivyo ili  kuepuka  yeye kama  waziri  kutumbuliwa lazima  kila mmoja afanye kazi kwa weledi…

Soma Zaidi >>

SALIM ASAS ABRI ASAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO CHUO CHA R.D.O MDABULO

Na Francis Godwin, Iringa MJUMBE  wa  halmashauri   kuu ya  chama  cha mapinduzi Taifa  (NEC)  Salim   Salim Abri  amechangia  kiasi cha  shilingi milioni 3 kwa  chuo    cha  ufundi stadi cha  R.D.O  Mdabulo  wilaya  Mufindi  mkoani Iringa  kwa ajili ya  kutatua  changamoto  mbali mbali  za  chuo   hicho. Abri   alikabidhi  msaada  huo  jana  wakati wa ma hafali ya  tatu ya  chuo   hicho  na  kuwa  pamoja na  kuunga  mkono  jitihada  kubwa  zinazofanywa na  uongozi  wa  chuo   hicho katika  kuwasaidia  watoto wasio na  uwezo  kupata  elimu  mbali mbali  ikiwemo  elimu ya  sekondari  katika  shule …

Soma Zaidi >>

KIASI CHA SHILINGI BILIONI 12 ZAHITAJIKA KUHAMISHA MAGEREZA IRINGA MJINI

Na Francis Godwin,Iringa KIASI  cha  shilingi  bilioni 12 zinahitajika kwa  ajili ya  kuhamisha  gereza  la Iringa mjini  ili  kupisha  upanuzi wa hospitali ya  rufaa ya  mkoa wa Iringa . Kamishina jenerali  wa  magereza  nchini  Phaustine  Kasike   hayo leo   wakati wa  ziara  yake  mkoani Iringa na  kuwa  tayari  mchakato wa  kuhamisha  gereza  hilo  umeanza  katika eneo la mlolo  nje ya  Manispaa ya  Iringa . Kasike  alisema  kuwa  hivi  sasa  maandalizi ya  ujenzi wa nyumba  za  watumishi  wa magereza  yanafanyika katika  eneo la  Mlolo  na  tayari  baadhi ya  vifaa vya  ujenzi kama …

Soma Zaidi >>

MADIWANI WA CCM IRINGA MJINI WASUSA BARAZA LA MADIWANI

Na Francis Godwin, Iringa KIKAO   cha  baraza la madiwani  wa halmashauri ya  Manispaa ya  Iringa  kimeshindwa  kufanyika  baada ya madiwani wa   chama  cha mapinduzi (CCM)  kususia kikao hicho   wakipinga  kile  walichodai ni ubabe wa mstahiki meya  kupitia  chama  cha Demokrasia na maendeleo  (CHADEMA) Alex  Kimbe katika  uundaji wa kamati mbali mbali na uendeshaji wa vikao hivyo. Akizunguza leo  na waandishi  wa habari katika   ofisi ya  CCM wilaya ya Iringa mjini naibu meya wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Joseph Lyata  alisema kuwa  uamuzi wa  kutoingia katika  kikao  hicho   ni kutokana na…

Soma Zaidi >>

KAMPUNI YA RUAHA FARM NI MKOMBOZI WA WAFUGAJI NYUKI IRINGA

KAMPUNI  ya  uchakataji  wa  asili  ya Ruaha farm  mkoani Iringa kupitia asali yake Ruaha  Honey  imeanza  kuwaokoa  kiuchumi  wafugaji wa  nyuki  mkoani Iringa kwa kutoa  mizinga na  kuwaunganisha na  soko la asali . “kampuni  ya Ruaha Farm  imekuja  kivingine  baada ya  kufunga mashine  za  kisasa  za  kuchakata  asali  yenye  ubora pasipo  kutumia vifaa vya  kienyeji kama moshi  na vingine “  Mkurugenzi  mtendaji wa kampuni ya Ruaha  Honey  Fuad Abri  alisema  kuwa  kampuni yake  imeendelea  kuunga mkono jitihada za  serikali  ya  awamu ya  tano  chini ya   Rais Dkt  John Magufuli ya Tanzania  ya  viwanda .  Alisema ubora wa  asali  ya kampuni ya Ruaha Honey  ni tofauti na  asali   nyingine  zinazouzwa  mitaani kwani  sifa  kubwa ya  asali  ya Ruaha honey ni asali halisi toka katika vijiji vinavyozunga hifadhi ya Ruaha national park.  Asali ya ruaha honey ni Asali bora inayozingatia usafi wa vyombo, usafi…

Soma Zaidi >>

SERIKALI YA TANZANIA YAPONGEZA USAID KUPITIA MRADI WA FEED THE FUTURE KWA KUMWAGA PESA

SERIKALI  Tanzania  imepongeza nchi ya   marekani   kupitia  Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) chini ya   mradi   unaofadhiliwa na  Feed the Future Advancing Youth Tanzania  kwa  kusaidia pesa  za ruzuku  zaidi ya  shilingi bilioni 1.2 kwa makundi ya  vijana  wajasilia mali  nchini. Akitoa  pongezi  hizo  jana katika  kijiji  cha  Mgela kata ya  Kiwere  wilaya ya  Iringa mkoani Iringa  wakati  hafla ya  kukabidhi   hundi kwa makundi ya  vijana  wanaojishughulisha na shughuli za  kilimo naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu; Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Anthony Peter Mavunde alisema  kuwa  USAID  kupitia mradi  huo wa Feed The Future  Advancing Youth Tanzania  imekuwa mkombozi  mkubwa kwa  makundi ya vijana. Hivyo  alisema  kuwa vijana  nchini  wanaowajibu  wa kuchangamkia  fursa  ya  kuwekeza katika  kilimo  na  shughuli  nyingine za  kiuchumi  huku  serikali ya Tanzania  itaendelea  kuwasaidia  vijana  hao  kwa kuraslimisha   shughuli  zao kama  za  ufundi na  nyingine   ili  kuweza  kupewa fedha  za  ruzuku kwa  ajili ya  kukuza  mitaji yao. Mavunde  alisema  kuwa  lazima  vijana  kutoka  vijiweni na  kujikita katika kilimo na  shughuli nyingine za kiuchumi kama  njia ya  kujikwamua  kiuchumi  zaidi. ‘’ Nawataka…

Soma Zaidi >>

TBA WAPONGEZA FAMARI STORE KWA KUWAPA MAFUNZO MAFUNDI RANGI IRINGA

WAKALA wa  majengo Tanzania (TBA )  mkoa wa  Iringa amepongeza  kampuni ya  Famari  Store  kwa  kutoa mafunzo kwa mafundi rangi  wa  mkoa wa Iringa na Njombe  kuwa  yatasaidia   kuongeza  ubora wa majengo mkoani hapa . Menja  wa TBA  mkoa wa Iringa  Fazes  Tarimo ametoa  pongezi hizo jana  wakati  akifunga mafunzo ya   siku  moja  yaliyoandaliwa na kampuni ya Famari  Store  ya  mkoa  Iringa na  kuendeshwa  na  kampuni ya Slkcoat Print Co.Ltd  ya  nchini  Uturuki  kupitia tawi lake la  jijini Dar es Salaam . Alisema kuwa  mafunzo hayo  ni mazuri ya  yanakwenda …

Soma Zaidi >>