CHADEMA YATANGAZA MAJINA YA WAGOMBEA UBUNGE JIMBO LA MONDULI, KOROGWE NA UKONGA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Kikao Maalum cha Kamati Kuu iliyokaa kwa siku mbili, Agosti 15-16, mwaka huu, jijini Dar es Salaam baada ya kupokea na kujadili kwa kina taarifa kuhusu chaguzi za marudio za ubunge na udiwani na hali ya kisiasa nchini; Chama hicho, kimefikia maazimio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kufanya uteuzi wa wagombea ubunge katika majimbo ya Monduli, Korogwe na Ukonga, kupitia Chama hicho, kwenye uchaguzi wa marudio ambao kampeni zake zitaanza rasmi Agosti 24- hadi Septemba 15 na siku ya kupiga kura Jumapili Septemba…

Soma Zaidi >>

PAPA FRANCIS ALAAN VITENDO VYA UDHALILISHAJI DHIDI YA WATOTO

Vatican imesema kuwa inataka kusikiliza kwa kina hoja za wahanga zaidi ya 300 walioathirika na vitendo vya ukatili ili kujua nini kilichotokea dhidi yao kutoka kwa makaasisi wa kanisa hilo katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani na kuliita tukio hilo kuwa ni la kinyama. Hatua hii imekuja mara baada ya waendesha mashtaka nchini Marekani kubaini kuwa zaidi ya watoto 1,000 huko jimbo la Pennsylvania walifanyiwa ukatili huo. Askofu wa Kanisa Katolik nchini Marekani ameagiza kufanyika uchunguzi ambao utaongozwa na Vatican, Kadnal Daniel DiNardo ambaye ni Rais wa kundi la maaskofu…

Soma Zaidi >>

UN YATAKA KUACHIWA HURU MWANAHARAKATI NABEEL RAJAB

Bodi ya umoja wa mataifa UN,imetaka kuachiliwa huru kwa mwanaharakati wa haki za binadamu wa Bahraini Nabeel Rajab aliyefungwa kwa madai ya kufanya makosa ya kueneza habari za uongo na kukashifu mamlaka za kiserikali. UN inasema kuwa hukumu ya Nabeel Rajab ilifanyika kinyume cha sheria na ilikiuka uhuru wake binafsi wa kujieleza, ambapo hadi sasa Nabeel amekwisha tumia miaka mingi tu gerezani tangu alipokuwa akiongoza harakati zake za kidemokrasia mwaka 2011.Lakini serikali kwa upande wake inasema kuwa mashitaka ya Rajab yalitolewa katika mfumo wa uhuru na uwazi. Nabeel Rajab, mkuu…

Soma Zaidi >>

NYAMAGANA KUKAMILISHIWA MIRADI YA MAENDELEO AMBAYO HAIKUKAMILIKA AWAMU ILIYOPITA

Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli, imejidhatiti katika mwaka huu wa fedha 2018/19 kukamilisha miradi ya maendeleo katika sekta ya Afya ambayo haikukamilika katika awamu iliyopita ikiwemo miundombinu ya majengo pamoja na Vifaa tiba wilayani Nyamagana. Haya yamebainishwa na Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe Stanslaus Mabula alipokuwa katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Kata tatu Isamiro, Pamba pamoja na Kata ya Mahina, ambapo katika mwaka huu wa fedha 2018/19 Serikali imetenga shilingi . 261,000,000 ili kukamilisha…

Soma Zaidi >>

CHADEMA :TUMESHTUSHWA NA UPOTOSHAJWI UNAOFANYWA NA NEC

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema, kimeshtushwa na kiwango cha uongo na upotoshaji unao oneshwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kuendelea kuhalalisha vitendo vya kuharibu na kuvuruga uchaguzi vilivyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi wa marudio uliofanyika Agosti 12, mwaka huu. Katika taarifa iliotolewa na chama hicho imeeleza ,taarifa iliyotolewa jana na tume hiyo,iliyokua ikilenga kujibu moja wapo ya nchi wahisani wa maendeleo nchini ambayo ilitoa tamko la kuonesha kuguswa na matukio yaliyotokea wakati wa uchaguzi huo. Taarifa hiyo imesema, tume hiyo imeamua kutaka kuidanganya jamii ya Watanzania,…

Soma Zaidi >>

MWILI WA MWANAMAPINDUZI ALIYEJULIKANA KAMA KIBARAKA WA WAZUNGU “JONASI SAVIMBI” KUFUKULIWA NA KUPEWA HESHIMA KAMA BABA WA TAIFA HILO LA ANGOLA.

Jonas Savimbi. Ni vyema na ni heshima kubwa pale viongozi wa Afrika wanapotambua mchango wa viongozi wao mbali na tofauti zilizowahi kutokea apo mwanzo sasa sikia habari hizi njema kutoka Angola. Kiongozi wa UNITA Isaias Samakuva amedai kwamba amepewa nafasi hiyo na Rais wa Nchi hiyo Joao Laurenco kwamba Mwili wa aliyekuwa kiongozi wa waasi nchini Angola Jonas Savimbi utafukuliwa kabla ya mwisho wa mwaka huu ili apate kupewa maziko mazui, kwa mujibu wa chama chake cha Unita kilichonukuliwa na shirika la habari la AFP na pamoja na Daily Nation…

Soma Zaidi >>

DC MJEMA AMTUMBUA OFISA MASOKO ILALA

  MKUU wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemsimamisha kazi OFISA Masoko wa Manispaa ya Ilala, Solomon Mushi asiendelee kusimamia soko kuu la Kigogo fresh kwa kushindwa kusimamia majukumu yake. DC Mjema ametoa agizo hilo mapema leo alipokua katika ziara yake ya jimbo la ukonga katika kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia ufumbuzi, ambapo amepokea malalamiko mengi katika soko hilo ambalo ameshindwankulisimamia Ofisa huyo. “Mushi nakusimamisha kuanzia sasa yaani Leo marufuku kusimamia soko hili la Manispaa ya Ilala la Kigogo Fresh badala yake nakuagiza Mkurugenzi tafuta Ofisa mwingine kwa ajili…

Soma Zaidi >>

RIPOTI YA LHRC YAITAKA SERIKALI KUIKABILI VYEMA SEKTA YA MADINI

Ripoti ya Haki za Binadamu na Biashara 2017 iliyofanywa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu LHRC imeitaka Serikali kuikabili vyema Sekta ya madini nchini kuhakikisha yanalipa kodi kwa manufaa ya nchi na kuwachukulia hatua stahiki kwa wale watakaokwepa. Akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo, Mkurugenzi Mtengaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu,Wakili Anna Henga wakati akizindua Ripoti ya Haki za Binadamu na Biashara, ambapo amebainisha mapendekezo kadhaa kwa serikali juu ya kuboresha mazingira mazuri yenye haki na usawa kwa jamii. “LHRC inapendekeza serikali kupitia Mamlaka ya…

Soma Zaidi >>

CHADEMA: TUNAMTAKA DC MJEMA KUSITISHA ZIARA YAKE JIMBO LA UKONGA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Ilala kimesema kinamtaka Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema kusitisha mara moja ziara yake anayofanya hivi sasa katika kata mbalimbali za jimbo la Ukonga. Katika taarifa iliotolewa na chama hicho imeeleza kuwa, ziara hiyo ina kila dalili ya kuanza kufanyia kampeni Chama cha Mapinduzi (CCM) kabla ya muda wa kampeni kuelekea uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye Jimbo hilo utakaofanyika tarehe 16 Septemba 2018. Ratiba ya mchakato wa uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ukonga imetolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)…

Soma Zaidi >>

MAVUNDE AITAKA TUME YA USULUHISHI NA UAMUZI(CMA) KUTOCHELEWESHA MASHAURI

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Peter Mavunde amewataka wasuluhishi wa Tume ya usuluhishi na uamuzi (CMA) kufanya kazi kwa  uadilifu na kumua mashuri kwa uharaka. Pia ameitaka  Tume hiyo, kufanya kazi zao kwa uweledi na kwa kuzingatia maadili katika utoaji wa haki na pia kuhakikisha wanatoa maamuzi kwa wakati pasipo ucheleweshaji ili kusaidia kuchochea maendeleo ya Uchumi wa Viwanda. Mavunde ameyasema hayo leo asubuhi katika Uwanjanwa Jamhuri-Morogoro wakati akihitimisha ratiba ya awali ya siku 3 ya mafunzo ya Wafanyakazi wa (CMA) kutoka nchi…

Soma Zaidi >>