MJUMBE WA UN KUMALIZA MZOZO BAINA YA YEMEN NA SAUDI ARABIA

Huko mashariki ya mbali mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Yemen, Martin Griffiths anatarajiwa kufanya zaira rasmi nchini Saudi Arabia na Yemen kufuatia mzozo uliopo baina ya matafa hayo mawili. Griffiths Katika zaira yake hiyo, nchini Yemen anatarajiwa kukutana na Rais Abd Rabbo Mansour Hadi, baada ya kufanya mazungumzo na viongozi tofauti nchini Saudi Arabia. Baada ya ziara yake nchini Saudi Arabia, atajielekeza nchini Yemen ambapo pia anatarajiwa kukutana na viongozi tofauti wa taifa hilo. Saudi Arabia inaongoza jeshi la ushirika ambalo lilianzisha operesheni nchini Yemen mnamo…

Soma Zaidi >>

POLISI 06 WAUAWA KATIKA SHAMBULIZI LA BOMU HUKO TUNISIA

Maafisa sita wa vikosi vya usalama wameuawa katika shambulizi la bomu kaskazini magharibi mwa Tunisia, shambulizi lililodaiwa kutekelezwa na kundi la Aqmi lenye mafungamano na Al Qaeda. Mazishi ya polisi hao yamefanyika hapo jan Jumatatu mapema asubuhi karibu na mji wa Tunis. Mashambulizi hayo, ambayo yamesababisha vifo vingi tangu miaka miwili iliyopita, wakati ambapo Tunisia inayokabiliwa na mgogoro wa kisiasa huku ikiwa n matumaini mazuri mwaka huu kwa kuwapokea watalii wengi baada ya kuboresha hali usalama. “Maafisa sita wa kikosi cha ulinzi wa Taifa waliuawa na watatu walijeruhiwa wakati gari…

Soma Zaidi >>

UINGEREZA HALI TETE, WAZIRI MWINGINE WA TATU AJIUZURU KUFUATIA SAKATA LA BREXIT

Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Uingereza Borris Johnson amejiuzulu. Boris amejiuzulu leo baada ya waziri aliyesimamia mchakato wa Uingereza kujitenga na Umoja wa Ulaya, David Davis, na naibu wake pia kujiuzulu. Mawaziri hao wamejiuzulu siku chache tu baada ya Waziri Mkuu Theresa May kutangaza kupata maridhiano na mawaziri wa serikali yake kuhusu mkakati wa kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya. Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari, Borris amesema Waziri Mkuu Theresa May amekubali kujiuzulu kwake na kwamba atakayechukua wadhifa wake atatangazwa hivi karibuni. Awali Bi Theresa May alisisitiza…

Soma Zaidi >>

ISRAEL YAKAMATA WAPALESTINA 10 KATIKA ENEO LA WEST BANK

Wapalestina kumi wameripotiwa kukamatwa na wanajeshi wa Israel katika eneo la West Bank kwa madai ya  shutuma za kujihusiha na ugaidi. Wapalestina hao waliokamatwa mwishoni mwa juma lililopita wamewekwa rumande mpaka pale uchunguzi utakapokamilika. Jeshi la Israel limekuwa likifanya uvamizi na kuwakamata wapalestina mara kwa mara, huku wanajeshi wa nchi hiyo wamekuwa wakisema kuwa ukamataji huo unafanyika kwa lengo la kuwatafuta wapalestina wenye makosa. Kulingana na ripoti zilizotolewa na Palestina, inasemekana Wapalestina zaidi 6500 wapo katika magereza ya Israel na kati ya wafungwa hao 62 ni wanawake na 350 ni…

Soma Zaidi >>

KIKUNDI CHA GROUP LA WHATSAPP KINACHOTOA HUDUMA ZA KIJAMII

Imezoeleka kwamba magroup mengi ya mitandao hasa mtandao wa Whatsap ni kwa ajili ya kuchati kwa kubadilishana mawazo, kupashana habari, kukutanisha marafiki wapya na mengine mengi, ila hii imekuwa ni tofauti kabisa na kundi (group) hili. Group la Whatsap hilo linalojulikana kwa jina la Vijana wa Yesu jana tarehe 7 Julai, 2018 lilipeleka furaha kwa kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalum cha Salvatory Army kilichopo maeneo ya sabasaba Wilaya ya Temeke jijin Dar es salaam na kuwapa baadhi ya mahitaji ambayo ni muhimu hapo kituoni. Wanagroup hao walifika kituoni…

Soma Zaidi >>