ALIYEPASWA KUWA SHAHIDI UPANDE WA JAMHURI AMTETEA NONDO MAHAKAMANI LEO

    Na Francis Godwin,Darmpya Iringa SHAHIDI wa Mwisho upande wa utetezi wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania (TSNP) Bw Abdul Nondo iliyofunguliwa katika mahakama ya Iringa imefungwa kwa shahidi wa Nondo , Alphose Lusako  (29) ambae ni mwanafunzi wa sheria mwaka wa Kwanza chuo kikuu cha Dar es salaam mkazi wa Tabata Kimanga jijini Dar es Salaam kutoa ushahidi wa kumtetea Nondo mahakamani hapo . Shahidi Lusako ambae amepata kuwa katibu mtendaji wa TSNP amehitimisha kutoa ushahidi wake Leo (jumatano) mbele ya Hakimu wa mfawidhi wa…

Soma Zaidi >>

ZIARA YA DC WA UBUNGO KUTATUA KERO YA WAFANYABIASHARA UBUNGO-MATAA.

    Ubungo Dar es Salaam. Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mhe. Kisare Makori leo aliambatana na Mkurugenzi wa Halimashauri hiyo ndugu,Beatrice Kwayi na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wadogo wadogo wanaofanya biashara zao pembezoni mwa barabara iliyopo eneo la Ubungo Mataa. Mazungumzo yalilenga kufikia mustabali na wafanyabiashara hao kuweza kuhama kutoka eneo hilo kwenda eneo la SIMU 2000(Mawasiliano) ambapo ndipo soko lilipojengwa na halmashauri kwa ajili ya wafanya biashara wadogo wadogo. Katika majadiliano hayo Mkuu wa wilaya Mh Kisare Makori amewaomba wananchi hususani wafanyabiashara wadogowadogo kuhama kutoka eneo hilo kwenda…

Soma Zaidi >>

KAMPENI YA TOKOMEZA ZERO KISARAWE KUJA NA MATOKEO BORA KWA WANAFUNZI

  Kisarawe Pwani. Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi. Jokate Mwegelo leo tarehe 19/09/2018 amezindua rasmi kampeni ya TOKOMEZA ZERO Kisarawe tukio lililofanyika katika shule ya sekondari Chazinge Wilayani humo akizungumza na waandishi wa habari Mkuu wa wilaya hiyo amesema ; “Nimedhamiria kwa dhati kuanzisha kampeni hii kwa lengo la kuboresha na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wetu katika wilaya hii ili tuwape watoto wetu urithi wa maisha ya badae.” Akiwa katika uzinduzi wa kampeni hiyo Mkuu huyo wa wilaya amesisitiza uhusiano na ushirikiano baina ya ya watendaji wote wa serikali…

Soma Zaidi >>

“BENKI YA NMB KUUNGA MKONO JITIHADA ZA MAENDELEO KISARAWE”

MKUU WA WILAYA YA KISARAWE NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KISARAWE WAPANGA MKAKATI WA MAENDELEO WILAYA YA KISARAWE KWA KUSHIRIKIANA NA BENKI YA NMB.   Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Bi. Jokate Mwegelo, pamoja na Mussa Gama, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kisarawe, wamefanya kikao muhimu cha ushirikiano katika Maendeleo pamoja na Mkurugenzi Mtendaji (Managing Director & CEO) wa Benki ya NMB Tanzania, Bi. Ineke Bussemaker, akiongozana na Kiongozi wa Mahusiano ya Kibenki na Serikali (Head of Government Banking), Bibi Vicky P. Bishubo. Kikao kiliangazia maeneo makubwa matatu ambayo ni Elimu,…

Soma Zaidi >>

ALIYEKUWA MWENYEKITI CCM MKOA IRINGA AACHIWA HURU NA MAHAKAMA

Mahakama ya Hakimu Mfawidhi Mkoa wa Iringa imemwachia  huru aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Iringa, Dokta Jesca Msambatavangu (41), na mwenzake Ismaili Mlenga,  ambao walishitakiwa kwa kesi jinai namba 65 ya mwaka  2017 baada ya kesi hiyo kukosa ushahidi kamili. Akitoa maamuzi madogo ya kesi hiyo leo Agosti 29 mahakamani hapo Hakimu mfawidhi Liad Chamshama amesema washitakiwa hao hawana kesi ya kujibu na hivyo mahakama  inawaachia huru . Akizungumza na wanahabari  mara baada ya kuachiwa huru kwa  washitakiwahao, wakili aliyekuwa akiwasimamia kesi (Dk.Msambatavangu na Mlenga) Alfredy Kingwe amesema uamuzi huo wa mahakama wameupokea kwa  mikono miwili maana awali kesi ya msingi ilikuwa shambulio la kawaida lakini baadae upande wa Jamhuri ukaja na mashtaka mengine ya ubakaji,dawa za kulevya pamoja na shambulio la kudhuru…

Soma Zaidi >>

“MKUU WA WILAYA YA KISARAWE MH. JOKATE MWEGELO KUJA NA MBINU MPYA ZA KUINUA ELIMU KISARAWE. “

Na.. Mwalimu Richard Augustine Baruapepe: augustinerichard629@gmail.com +255754728801. Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Bi JOKATE MWEGELO leo tarehe 23/08/2018 amefanya kikao wilaya Kisarawe katika ukumbi wa mikutano uliopo wilayani hapo chenye lengo la kuinua Elimu katika wilaya ya Kisarawe. Akifungua kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe alianza kwa kuwatambulisha wadau mbalimbali walioamua kuunga mkono jitihada zake na jitihada za serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wake Dr JOHN POMBE MAGUFULI ,alipongeza na kuwashukuru kwa kazi kubwa ambayo wameifanya ya kuamua kuleta baadhi ya vifaa mbalimbali ikiwemo Mashine ya…

Soma Zaidi >>

WAZIRI MPANGO AIBUKIA BANDARI AIKINGIA KIFUA SERIKALI KUHUSU KUKWEPA KODI.

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, amefanya ziara ya kushitukiza katika eneo la kuhifadhia makontena-Bandari Kavu Dar es Salaam (DICD), na kukagua makontena 20 yaliyoingizwa nchini na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na kuiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA kuendelea na mnada wa makontena hayo ili kupata kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia shilingi bilioni 1.2. Dkt. Mpango amesema kuwa kodi hiyo inadaiwa kwa mujibu wa sheria za nchi baada ya mwenye mali kushindwa kulipa kodi na kwamba amesikitishwa na vitisho vinavyotolewa na Mkuu huyo…

Soma Zaidi >>