RAIS MAGUFULI AKUTANA NA ROSTAM AZIZ, MBATIA,CHEYO NA SHIBUDA IKULU

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Novemba, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na wanasiasa Mhe. John Cheyo, Mhe. James Mbatia na Mhe. John Shibuda, na mfanyabiashara Bw. Rostam Aziz Ikulu Jijini Dar es Salaam. Baada ya mazungumzo hayo Bw. Rostam Aziz amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa uongozi bora ambapo amesema anatengeneza misingi imara ya uchumi unaokua kwa uhakika zaidi kwa kujenga miundombinu ikiwemo barabara, reli na bandari ambayo ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi na kuzalisha ajira. Bw. Rostam Aziz amesema…

Soma Zaidi >>

DKT. MPOKI AELEZA UCHOVU SABABU ZA AJALI BARABARANI NCHINI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa moja ya sababu za ajali barabarani, ni uchovu wa madereva. Dkt. Mpoki ameyasema leo Novemba 13,2018 wakati wa kufungua mafunzo ya watoa huduma za tiba, uokoaji na usafirishaji wa majeruhi wa ajali na wagonjwa wenye dharura mbalimbali nje ya Hospitali nchini. Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Dkt. Mpoki amelitaka jeshi la Polisi nchini kuangalia namna ya kuweka utaratibu wa madereva kubadilishana kwani suala la uchovu linachangia kwa kiasi kikubwa ajali za…

Soma Zaidi >>

RAIS MAGUFULI ATOA MAAMUZI MAGUMU UNUNUZI WA KOROSHO ZOTE ZA WAKULIMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Novemba, 2018 ametangaza uamuzi wa Serikali kununua korosho zote za wakulima msimu huu kwa bei ya shilingi 3,300 kwa kilo baada ya wanunuzi binafsi kushindwa kutimiza maagizo ya Serikali kwa kuanza kununua kwa kusuasua na kwa bei isiyoridhisha. Mhe. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo leo Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kuwaapisha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Joseph George Kakunda, Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Ngailonga Hasunga, Naibu Waziri Ofisi…

Soma Zaidi >>

ZIARA YA MAKAMU WA RAIS WILAYANI SAME NA MWANGA LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema hakuna Maendeleo pasipo Utawala bora. Makamu wa Rais amesema hayo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mwanga mkoani Kilimanjaro. “Viongozi wa Halmashauri, Viongozi wa Wilaya wasipokuwa na Utawala bora, wasiposhirikiana, Chama, Serikali, Wilaya, Halmashauri tusitegemee kuwa na maendeleo tutalalamika siku zote” alisema Makamu wa Rais. Leo katika ziara yake ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo Makamu wa Rais alitembelea miradi mbali mbali katika Wilaya ya Same na Mwanga. Akiwa Wilayani Same, Makamu…

Soma Zaidi >>

WANARIADHA WA TANZANIA LYMO, MAKULA KIBARUANI BEIRUT MARATHON

WANARIADHA wa Tanzania, Samson Lyimo na Gloria Makula, Novemba 11, wanatarajiwa kupeperusha bendera ya Tanzania katika mbio za Blom Bank Beirut Marathon zitakazorindima jijini Beirut, Lebanon. Mbio hizo zitaanzia eneo la Beirut WaterFront na kumalizikia Martyrs’ Square. Nyota hao, wamepata nafasi hiyo chini ya ufadhili wa Kampuni ya SBC Tanzania, baada ya kufanya vema katika mbio za Dar Rotary Marathon zilizofanyika Oktoba 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Wanariadha hao, waliondoka nchini Novemba 8 wakiongozana na Mkuu wa Mahusiano wa SBC Tanzania, Alexander Nyirenda. Akizungumza katika hafla ya kuwaaga,…

Soma Zaidi >>

KOROSHO ZAMTUMBUA WAZIRI CHARLES TIZEBA RAIS ATENGUA UTEUZI WAKE

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu Jijini Dar e Salaam iliyotoka jioni ya leo Novemba 10,2018 imeeleza kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Kilimo Dkt. Charles John Tizeba ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mhe. Josephet Ngailonga Hassunga. Hii imeashiria kwa namna moja ama nyingine hali ya mambo ndani ya Nchi katika suala la korosho ambalo limepamba moto kwa wanunuzi kufanya mgomo baridi huku mamlaka za juu akiwemo Waziri Mkuu Mhe.Kasim Majaliwa Majaliwa kutoa tamko la siku nne pekee lililoanza  jana…

Soma Zaidi >>

EMMANUEL OKWI WA SIMBA ACHAGULIWA MCHEZAJI BORA WA MWEZI OKTOBA (TPL) 2018/2019

MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, Emmanuel Okwi amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Oktoba wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.  Okwi anayecheza nafasi ya ushambuliaji, alitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Yahya Zayd wa Azam na Eliud Ambokile wa Mbeya City alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu…

Soma Zaidi >>

MAGUFULI AKUTANA NA MADAKTARI BINGWA WA MOYO KUTOKA ISRAEL,MAREKANI NA CANADA

Uamuzi wa Serikali ya Awamu ya Tano kufungua Ubalozi wa Tanzania nchini Israel umeanza kuzaa matunda baada ya timu ya madaktari na wataalamu wa matibabu ya moyo 30 kutoka nchini Israel kuja hapa nchini kwa ajili ya kuokoa maisha ya watoto 51 wanaopatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam. Timu ya Madaktari na wataalamu hao wakiwemo 2 kutoka Marekani na Canada wanatoka shirika la Save a Child’s Heartla Israel wamekutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,  Ikulu…

Soma Zaidi >>

DKT.KIGWANGALLA: “RELI YA TAZARA INAONGEZA FURSA ZA UCHUMI KUPITIA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla amesema kuwa kupitia reli ya TAZARA inayounganisha nchi za Zambia na Tanzania ni kielelezo cha uchumi na kimkakati ikiwemo shughuli za Utalii Nchini. Waziri Dkt. Kigwangalla amesema hayo kwa nyakati tofauti Jijini Dar es Salaam na Matambwe Mkoani Mkoani Morogoro katika eneo la kiutalii la Selous mwishoni mwa wiki wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya miaka 42 ya reli hiyo iliyojengwa na Serikali ya China. Awali akizungumza katika stesheni ya TAZARA Jijini Dar e s Salaam, Dkt. Kigwangalla amesema tukio hilo ni…

Soma Zaidi >>