KAMATI YA MAADILI YA BUNGE YAMHOJI CAG

Kamati ya Maadili, Haki na Madaraka ya Bunge imemhoji Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad kuhusu kauli yake ya “udhaifu wa Bunge.” CAG amehojiwa mapema leo Januari 21, 2019 ambapo mara baada ya mahojiano hayo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Emmanuel  Mwakasaka amesema atawaeleza waandishi wa habari kilichojiri katika kikao hicho. Prof. Assad ameitwa mbele ya kamati hiyo kujieleza kuhusu kauli aliyoitoa wakati akijibu swali la mwandishi wa televisheni ya UN, Anord Kayanda kuhusu kutoshughulikiwa ipasavyo kwa ripoti zake zinazoonyesha ufisadi. “Kama tunatoa ripoti na…

Soma Zaidi >>

DKT SHEIN AWATAKA WAHITIMU WA CHUO KUTUMIA UJUZI WAO KUJIAJIRI

RAIS wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Mhe.Dk Ali Mohamed Shein amewataka wahitimu wa Chuo cha Abdul Rahman Al Sumait kutumia ujuzi walioupata chuoni hapo kwa kujiajiri wenyewe bila ya kusubiri ajira kutoka Serikalini. Akisoma hotuba kwa niaba yake huko Chukwani, katika mahafali ya 18 ya chuo hicho, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Riziki Pembe Juma amesema tatizo la upungufu wa ajira si la Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pekee bali ni kilio cha dunia nzima. Aidha Dk. Shein ameupongeza uongozi wa chuo cha Alsumait…

Soma Zaidi >>

MBUNGE ZANZIBAR AMKINGIA KIFUA NDUGAI

NA DANSON KAIJAGE,DODOMA MBUNGE wa Viti Maalum kutoka Zanzibar Tahuida Nyimbo (CCM) amesema kuwa siku zote maamuzi ya Spika Job Ndugai hayajawahi kuwa ya kukurupuka. Nyimbo alisema kutokana na hilo ni jambo la aibu kuona baadhi ya wanasiasa kumkebei na kumdhalilisha huku wakiwa wanatamani kukwanisha utendaji wake wa kazi. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya sakata la Spika Ndugai kutoa agizo la CAG kufika mbele ya kamati ya Bunge ili kuhojiwa kwa madai ya kutoa kauli ya kulidhalilisha Bunge alipokuwa akihojiwa na kituo…

Soma Zaidi >>

KIKUNDI CHA VYAMA VYA SIASA CHAJITOSA KUSAIDIA DAMU HOSPITAL YA NYERERE

Na,Naomi Milton Serengeti Kikundi cha ujamaa na ujirani mwema Serengeti (KICHAUMWESE) kinachoundwa na vyama vitano vya siasa kimejitokeza na kuchangia unit 18 za damu kusaidia wahitaji mbalimbali katika Hospitali Teule ya Nyerere ddh Hospital hiyo bado ina changamoto kubwa ya uhitaji wa damu hasa kwa makundi maalum kama vile mama wajawazito na watoto lakini pia kwa watu majeruhi ambao hupata ajali Katika mkutano wao mkuu uliofanyika wilayani Serengeti wanakikundi walikabidhi hati ya usajili kwa katibu Tawala wilaya Cosmas Qamara aliyemwakilisha Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu na kuahidi kuendeleza…

Soma Zaidi >>

WABUNGE WA CCM WAJIPANGA KUMDHIBITI ZITTO

Na DANSON KAIJAGE, DODOMA WABUNGE wote wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wameazimia kwa pamoja kuhakikisha wanakabiliana na mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) kwa madai kuwa amekuwa kinara wa upotoshaji Umma pamoja na kuwa mstari wa mbele kupinga Mamlaka ya Spika kufanya kazi. Mbali na kujipanga kukabiliana na Zitto pia wamesema kuwa watahakikisha wanajibu hoja za Zitto na wapinzania kwa njia yoyote na kutoruhusu hoja za Zitto na wapinzania kwa ujumla kuendelea kusikilizwa na kusambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kama ilivyo sasa. Kamati ya wabunge…

Soma Zaidi >>

WATENDAJI KATA NJOMBE WAKALIA KUTI KAVU, DC APIGILIA MSUMALI MZAZI ALIYECHANGISHWA DAWATI AKALICHUKUE

Na Amiri kilagalila Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri ameapa kupambana na kiongozi yeyote atakayediriki kumchangisha mzazi fedha ya dawati kama walivyochangishwa baadhi ya wazazi katika shule ya secondari Maheve pamoja na shule ya Secondari Mabati zilizopo katika halmashauri ya mji wa Njombe. Akizungumza na waandishi wa habari mapema hii leo ofisini kwake mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa utaratibu wa kufuata waraka wa elimu bure uko pale pale, hivyo swala la kumchangisha mzazi dawati ni kinyume na maagizo ya serikali na endapo kutakuwa na ulazima wa kuchangisha mchango…

Soma Zaidi >>

WAZIRI BITEKO, PROF.MSANJILA WAUTAKA MGODI WA NORTH MARA KUTII MAMLAKA ZA SERIKALI

Waziri wa Madini Doto Biteko pamoja katibu Mkuu Wizara ya Madini Prof.Simon Msanjila wakutana na uongozi wa mgodi wa North Mara na kuutaka kulipa fidia ya ardhi kwa wananchi wanaozunguka mgodi huo. Akizungumza katika kikao kilichofanyika tarehe 17 Januari, 2019 katika Ofisi ya Waziri jijini Dodoma, Biteko aliwaeleza wajumbe hao kuwa walipaswa kuwa wamechukua hatua kadhaa kuonesha kua wanatii maagizo ya Serikali lakini kutokana na wao kuhisi serikali haina cha kufanya wakaamua kutulia kwa miezi mine ambapo wamefika Ofisini kueleza masuala ambayo hayajafanyiwa kazi. Hatuwezi kuwa tunakaa, tunafikia maamuzi ninyi…

Soma Zaidi >>

WAFANYABIASHARA DODOMA HATARINI KUPATA MAGONJWA

Wafanyabiashara na watumiaji wa soko la sabasaba lililopo jiji la  Dodoma wapo katika hatari ya kupata maambukizi ya magonjwa ya mlipuko kutokana na mlundikano wa uchafu uliopo ndani ya soko hilo. Akizungumza kwenye eneo hilo la dampo na waandishi wa habari mjumbe wa uogozi wa mpito soko hilo,Mabewo Daudi alisema kuwa mlundikano huo unatokana na jiji kutoondoa uchafu huo kwa wakati na kusababisha kuwepo pia kwa harufu kali. Aidha alisema kuwa kuwepo kwa uchafu huo kunaweza kuhatarisha mlipuko wa magonjwa ya tumbo kwa wafanyabishara wenyewe na hata kwa watumiaji wa…

Soma Zaidi >>

WAZAZI NGARA WAPEWA SIKU 14 KUWAPELEKA SHULE WATOTO WALIOCHAGULIWA KIDATO CHA KWANZA

Na Mwandishi wetu Ngara Mkuu wa wilaya ya Ngara Mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele ametoa muda wa siku 14 kwa wazazi na walezi wilayani humo kuhakikisha wanawapeleka shule wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kabla ya kuanza msako wa nyumba kwa nyumba. Mntenjele ametoa muda huo hii leo baada ya kizindua ujenzi wa vyoo vyenye jumla ya matundu 12 na tanki moja la Maji katika shule ya sekondari ya Kabanga wilayani Ngara vilivyojengwa na shirika la Tumaini fund chini ya kanisa la Anglikana dayosisi ya Kagera kupitia kwa…

Soma Zaidi >>

OPARESHENI YA UKUSANYAJI MAPATO JIJI LA ARUSHA YAANZA UPYA

Na.Fatuma S Ibrahimu – Arusha Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt. Maulid Suleiman Madeni amesema kuwa ifikapo kesho Tarehe 18 Januari, 2019 operesheni ya ukusanyaji wa mapato inatarajiwa kuanza upya baada ya kupumzika kwa muda mfupi kupisha msimu wa mapumziko na sikukuu. Ameyasema hayo wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari akiwa ofisini kwake leo Taehe 17 Januari, 2019 ambapo ameitambulisha timu mpya katika awamu hii ambayo ni Wakuu wa Idara zote zilizoko Halamshauri ya Jiji la Arusha na kila mmoja ataambatana na watumishi walio chini yake na watapangiwa maeneo…

Soma Zaidi >>