JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU WATATU KWA TUHUMA ZA KUMUUA MZEE WA MIAKA 60.

  Na Allawi Kaboyo,Kagera. Watu watatu wakiwamo mgambo wawili, wanashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Kagera kwa tuhuma za kumpiga na kumuua mzee mmoja aitwaye Daud Rwenyagira (60) mkazi wa kijiji Nyakahita wilayani Karagwe, baada ya kumtuhumu kuwazuia kufanya kazi yao ya kumkamata mtu aliyekula fedha za manunuzi ya kahawa. Akizungumzia tukio hilo kamanda wa polisi mkoani Kagera,Revocatus Malimi amesema kuwa mgambo hao walitumwa na mtendaji wa kijiji Nyakahita, kwenda kumkamata Theophil Pima, baada ya kulalamikiwa na mama aitwaye Mali Byamanyirwohi aliyemtuhumu kula hela zake za kununulia kahawa (BUTURA) na…

Soma Zaidi >>

DC MJEMA”WAZAZI WANYONYESHENI WATOTO ILI KUBORESHA LISHE”

  Na Heri Shaaban Ilala, MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewashauri Wazazi Wilayani Ilala kunyonyesha watoto wao ili wawe na lishe bora. Mjema aliyasema hayo Dar es Salaam leo wakati wa kumsainisha mkataba Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala katika kutekeleza afua za lishe Manispaa Ilala. “Wazazi nawaomba pindi mnapojifungua wanyonyesheni watoto wenu maziwa mpaka mda ufike msiwakatishe ni halali yao kwa ajili ya afya bora ya mtoto”alisema Mjema. Aidha pia aliwaka wananchi wake kula mro kamili na vyakula vya zamani kuachana na vyakula vya kisasa. Alisema katika nchi…

Soma Zaidi >>

GAMBOSI KIJIJI KILICHOSIFIKA KWA UCHAWI CHAFANYA MAPINDUZI YA MAENDELEO

  Na Dinna Maningo,Bariadi. Ukifika Kijiji cha Gambosi Kata ya Gambosi maarufu (Gamboshi)kilichopo km 50 Magharibi mwa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu utakutana na madhari nzuri yenye kuvutia iliyo sheheni miti ya kijani ya asili. Pia kuna hewa safi na maeneo mengi yaliyowazi huku maeneo mengine zikionekana  Nyumba za wananchi,mazao ya Pamba Mpunga,Mahindi na Viazi,Njegere,Choroko na Mbaazi. Kijiji hiki kwa miaka mingi Watanzania walio wengi wamekuwa wakiwa na hofu wakiamini kukithiri kwa imani za ushirikina na uchawi jambo ambalo linaelezwa kuwa kwa sasa hakuna uchawi imebaki tu historia au hadhithi…

Soma Zaidi >>

MAOFISA WATENDAJI UBUNGO,WATOA MSAADA KWA WATOTO YATIMA.

Na Mwandishi wetu, Dar es salaam. Maofisa watendaji wa mitaa ya Wilaya ya Ubungo, wametoa msaada wa vyakula, mchele kg 135, sukari, mafuta ya kula, uga wa ngano, unga wa mahindi,maharage na baadhi ya vifaa vya darasani katika Kituo cha kulelea watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi (Watoto wetu Tanzania). Maofisa hao wametoa msaada huo wakiwa wanaadhimisha mwaka mmoja toka walipoajiriwa na serikalika kuwa maofisa watendaji wa mitaa katika wilaya hiyo. Wakikabidhi msaada huo mbele ya mwanzilishi na Mkurugenzi mtendaji wa kituo hicho,Ndugu Evans Tegete,mwenyekiti wa maandalizi ya maadhimisho…

Soma Zaidi >>

MKOA WA KAGERA WAZINDU MKAKATI WA NYUMBA KUMI BORA ZA KIUSALAMA KUKOMESHA MAUAJI UHALIFU MAGENDO NA UHAMIAJI HARAMU.

  Na: Mwandishi wetu Karagwe Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti azindua rasmi mkakati wa kuimarisha usalama katika Mkoa wa Kagera uliopewa jina la “Nyumba Kumi Bora za Kiusalama”. Mkakati huo ukilenga kuimarsha Ulinzi na Usalama wa mkoa kuanzia ngazi ya chini katika jamii kwa kila nyumba kumi kuwa na kiongozi ambaye atakuwa na jukumu la kutambua wanafamilia wanaoishi katika kila nyumba anayoiongoza. Mkuu wa Mkoa Gaguti ambaye ni Mhasisi na Mwanzilishi wa Mkakati huo wa kukomesha uhalifu, ujambazi na vitendo vya uvunjifu wa amani katika…

Soma Zaidi >>

UJIO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI KAGERA, WENYE MATATIZO MBALIMBALI WAOMBWA KUJITOKEZA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UJIO WA MADAKTARI BINGWA NA KLINIKI TEMBEZI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA KUANZIA TAREHE O5 HADI 11 NOVEMBA, 2018 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti anapenda kuwataarifu Wananchi wa Mkoa wa Kagera na nje ya Mkoa kuwa Uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wameandaa Kliniki tembezi ya Madaktari Bingwa wa fani mbalimbali itakayofanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa (Government) kuanzia tarehe 05 – 11 Novemba, 2018. Ikiwa…

Soma Zaidi >>

BEI YA ZAO LA KOROSHO BADO PASUA KICHWA MINADA YAKWAMA

  Na Bakari Chijumba, Mtwara Wakulima wa zao la korosho katika mikoa ya kusini ya Lindi na Mtwara wamegoma kuuza Korosho zao kwa kile walichodai ni kuporomoka kwa bei ya zao hilo ukilinganisha na misimu iliyopita, kiasi ambacho wamesema hakuna maslahi kulinganisha na gharama zilizotumika katika kuzalisha zao hilo. Katika minada yote mitatu iliyofanyika kwa ajili ya kuanza msimu wa mauzo ya zao hilo wakulima walijikuta wakikataa kuuza korosho zao kwa kile walichodai wanunuzi walikuwa hawajafika bei ambayo ni tegemewa hivyo kupelekea minada yote mitatu kushindwa kufanikiwa. Katika Mnada wa…

Soma Zaidi >>