ATOROKA KIFUNGO BAADA YA USHAHIDI KUMMBANA

Na Stephen Noel Mpwapwa -Dodoma.

Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Julias Lwagila (51)aliyekuwa anakabiliwa na tuhuma za kulima zao la Bangi Heka tatu atoroka kifungo.

Mtuhumiwa huyo hakuonekana mahakamani wakati wa kusomewa hukumu hiyo kitu kinachopelekea kuaminika kuwa ametoroka hukumu Hiyo baada ya kuona kesi inamwendea vibaya.

Pamoja na kutokuwapo mahakamani lakini Mahakama ya Hakimu mkazi ya wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma imewahukumu watuhumiwa wengine kifungo cha miaka thelathini (30) bwana Julius Lwagila mkazi wa kijiji cha Wota, Kata Lwihomelo na wilaya ya Mpwapwa.

Kesi hizo zilikuwa zinasikilizwa na hakimu mkazi bwana Pascal Mayumba wa mahakama Hiyo ya wilaya ambapo aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa Bwana Julias Lwagila alikamatwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya aliyo kuwa imeambatana na mkuu wa Polisi mkoa wa Dodoma bwana Gireti Mroto Machi 29 mwaka huu Katika kijiji cha Wota.

Aidha Hakimu Mayumba alisema bila halali mtuhumiwa alitenda kosa hilo kinyume na sheria namba 11 kifungu kidogo cha 1(D) sura 5 ya mwaka 2015 ambapo alilima shamba la Bangi lenye ukubwa wa heka (3)tatu.

Katika utetezi wake Mtuhumiwa huyo alipoulizwa juu ya tuhuma zinazomkabili aliamua kukiri kosa hilo mbele ya kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na mbele ya RPC baada ya kusulubishwa, kupigwa na kuteswa ndipo aliposema bangi Hiyo alirithishwa kutoka kwa baba yake na inamsaidia kumuingizia kipato cha kusomeshea watoto wake.

Wakati huo huo mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha mwaka mmoja Bi Joyce Malagu (51) kwa kupatikana na hatia ya kupika pombe ya Moshi (gongo) .

Hakimu huyo Pascal aliiambia mahakama kuwa mtuhumiwa Bi.Joyce Malagu kuwa bila halali alikuwa akijihusisha na upikaji wa Pombe haramu aina ya Pombe Gongo kinyume na kifungu namba 225 kanuni ya adhabu .

Hakimu Mayumba alisema kuwa serikali na Taasisi zisizo kuwa za kiserikali zinajikita kupambana na madawa ya kulevya na serikali imekuwa ikitumia Pesa nyingi na kupambana na madawa ya kulevya lakini baadhi yao wamekuwa hawasikii maonyo hayo mithili ya kupigia mbuzi gitaa aliiambia Mahakama.

Pia alisema kesi hiyo iliyo pewa Nguvu na mashahidi watano na vielelezo vilivyopelekwa mahakamani bila Shaka yeyote na mtuhumiwa kupatikana na hatia .

Mwendesha mashtaka wa polisi bwana Wilson Mwita aliiomba mahakama itoe adhabu Kali kwa mtuhumiwa kutokana na madhara ya madawa ya kulevya yanayoweza kuathiri nguvu kazi ya Taifa Pamoja na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano Katika vita dhidi ya madawa ya kulevya.

Pia alisema fundisho hilo litakuwa kwa Wakazi wa mkoa wa Dodoma kiwemo wilaya ya Mpwapwa na nchi nzima kwa ujumla ili iwe fundisho kwa watu wanaoendeleza vitendo vya ulimaji wa zao la Bangi na madawa ya kulevya.

Hakimu Mayumba aliiambia mahakama kuwa watuhumiwa watafungwa kifungo cha miaka 30 Jela kutokana na kupatikana na hatia na kutokana na ushahidi na vielelezo vilivyo wasilishwa mahakamani.

Aidha hakimu huyo alitoa amri kuwa mtuhumiwa aliyetoroka atafutwe popote alipo ili aanze kutumikia kifungo chake Mara baada ya kukamatwa.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.