RAIS AL BASHIR ATISHIA KUWAKATA MIKONO WAANDAMANAJI

Khartoum, SUDAN.

Rais Hassan al Bashir wa Sudan amekemea vikali maandamano ya mkate yanayoendelea kwa zaidi ya wiki moja sasa nchini humo dhidi ya serikali yake na kusema kuwa atakata mikono ya waandamanaji hao.

Rais Al Bashir amesema kuwa atakandamiza vikali maandamano hayo na kwamba jeshi la Sudan litaharibu maisha ya waandamanaji na kukata mikono yao.

Aidha, kiongozi huyo amesisitiza waziwazi kwamba, hatasalimu amri mbele ya matakwa ya taifa la Sudan au matakwa ya wasaliti. Vilevile amewatahadharisha Wasudani kuhusu kile alichokiita uvumi na kusema kuwa, mwenendo wa marekebisho umeshika njia yake nchini Sudan.

Matamshi hayo makali ya Rais Omar al Bashir wa Sudan yametolewa kufuatia maandamano yanayoendelea kushuhudiwa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo dhidi ya hali mbaya ya uchumi na ughali wa bidhaa muhimu hususan mkate ambao ndio chakula kikuu cha Wasudani.

Maandamano ya Wasudani yaliyoanza kulalamikia hali mbaya ya kiuchumi yamepata sura nyingine na sasa waandamanaji wanataka kuondolewa madarakani serikali ya Omar al Bashir.

Hadi sasa watu wasiopungua 38 wameuawa katika maandamano hayo.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.