ALLY SONSO AFUNGUKA KUTUA YANGA.

 

Na Shabani Rapwi, Dar es Salaam

Beki wa klabu ya Lipuli FC ya Iringa, Ally Sonso leo Disemba 02, 2018 amefunguka na kukiri kufanya mazungumzo na viongozi wa klabu ya Yanga SC.

Sonso amesema kama viongozi wa Yanga watafata taratibu zinazo takiwa na uongozi wake ukikubali yupo tayari kujiunga na klabu hiyo huku akiahidi kupambana ili aweze kucheza, kwa sasa yeye bado ni mchezaji wa Lipuli FC.

“Mimi bado mchezaji wa Lipuli na hizo taarifa nazisikia kwenye magezeti na sina taarifa zozote”

“Kama wenzangu Yanga watafatisha taratibu ambazo viongozi watakazo kubaliana nazo basi naamini ntaungana nao” alisema Sonso

“Maongezi ni yapo, naamini kwa sababu yasemwayo yapo, mi naamini hivyo hivyo ” alisema Sonso

Mwisho amemalizia kwa kusema, anauwezo wa kuichezea timu kubwa kama Yanga bila ya kukosa namba.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.