ALIKIBA ATOA DONGO BAADA YA MWALIKO WA DIAMOND WASAFI FESTIVAL.

Jana Novemba 5, Diamond Platnumz alitangaza kuwa anatamani sana kumuona msanii mwenzake pia akiwa kama kaka yake kwenye muziki Alikiba awepo kwenye tamasha lake la Wasafi Festival ..video yake inapatikana DarMpyaTv

Lakini baada ya Diamond kuongea hayo watu walianza kuzungumza mitandaoni na kuanza kusema Alikiba hawezi kukubali huku wengine wakisema Alikiba akubali tu, na hadi kufikia wengine kusema Alikiba atatoa jibu lake baya au la kizarau sana.

Sasa bila shaka taarifa hizo zimemfikia Alikiba ambapo muimbaji huyo ameposti picha ya mchekeshaji Mr. Bean ikiwa na maneno yanayosomeka; ‘Thank you for listening, To my presentation’, halafu chini ya post hiyo akaandika “Your welcome”

Hii ndio Picha ya Mr Bean aliyoposti Alikiba leo

Mashabiki wengi wamechukulia kwamba hilo ndio jibu la Alikiba kwa Diamond kuhusu suala la yeye kushiriki Wasafi Festival ambayo itaanza November 24, 2018 mkoani Mtwara kisha kwenda Iringa na Morogoro.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.