AGIZO LA NAIBU WAZIRI MADINI LAWATIA KITANZINI WACHIMBAJI WADOGO NYARUGUSU

Jeshi la Polisi mkoani Geita linawashikilia wachimbaji wadogo watatu kutoka mgodi wa dhahabu uliopo katika kijiji cha Nyarugusu wilayani Geita kufuatia kukaidi agizo la Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo, linalowataka kusitisha shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.

Majina ya wachimbaji hao ni pamoja na Abdul Ramadhan ambaye pia ni Mmiliki wa Leseni, Hezron Enock na Mai Kibanda ambao ni wabia wa mgodi huo.

Wachimbaji hao wamekamatwa hii leo kufuatia agizo la Waziri Nyongo alilolitoa baada ya kufanya ziara kwenye mgodi huo ambapo amepokea malalamiko ya wananchi waliokaribu na mgodi huo  kuhusu nyumba zao kuharibika kwa mitetemo na sauti zinazotokana na ulipuaji wa baruti kwenye miamba ya mawe yenye dhahabu katika eneo hilo.

Katika hatua nyingine Nyongo ameagiza kukamatwa kwa mtumishi wa serikali aliyekaidi agizo la kusitisha shughuli za uzalishaji na kutoa tamko la mgodi huo uendelee kufanya kazi kinyume na maagizo ya wizara.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.