AFGHANISTAN YAONGOZA VIFO WANATASNIA YA HABARI 16 WAUAWA 2018

Shirikisho la mashirika ya waandishi wa habari, IFJ imesema kuwa idadi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa tasnia ya habari waliouawa mwaka wa 2018 imepanda na kufika 94.

Miongoni mwa hao 84 walikuwa waandishi wa habari, wapiga picha, mafundi mitambo na madereva.

Kulingana na ripoti ya shirika hilo, nchi hatari zaidi kwa waandishi wa habari mwaka huu unaomalizika ilikuwa, Afghanistan ambako wafanyakazi 16 wa taaluma ya habari walipoteza maisha, ikifuatiwa na Mexico ambako 11 waliuawa.

Nchi zingine ni Yemen, Syria, India, Somalia, Pakistan na Marekani.

 

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.