HAKUNA MJASIRIAMALI MWENYE SIFA ATAKAYEKOSA KITAMBULISHO-DC NJOMBE

Na Amiri kilagalila

Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth msafiri amezindua zoezi la ugawaji wa vitambulisho kwa wajasiriamali wadogo kiwilaya na kuwahakikishia wote wanao stahili kupata vitambulisho kabla ya mwezi kumalizika.

Akizungumza baada ya kuzindua zoezi hilo lililofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe amesema kuwa mala baada ya kusajiliwa na kupata kitambulisho hicho hategemei kuona mjasiriamali yeyote akifanya shughuli zake katika maeneo yasiyokuwa rasmi.

“zoezi hili linaendeshwa kwa maagizo ya muheshimiwa Raisi na leo sisi tunazindua sio mwisho lakini hatutalifanya kwa mda mrefu na tunatamani kufika mwisho wa mwezi huu wote ambao wanastahili wawe wamechukua vitambulisho hivi na wamekwisha kusajiliwa,na baada ya zoezi hili hakuna mtu yeyote atakayeruhusiwa kufanya biashara bila kitambulisho” alisema Ruth msafiri

Nao baadhi ya wajasiriamali wadogo kutoka halmashauri hiyo akiwemo Wille Kilasi ambaye ni mlemavu wa miguu wamesema kuwa vtambulisho hivyo vitawasaidia kwa kuwapa unaafuu kwa kuwa awali walikuwa wakilipa kodi kubwa kwa mwaka ukilinganisha na mitaji yao.

“kitambulisho hiki mimi naona kitatupatia unaafuu kwa kutupunguzia kiwango cha kodi sisi wafanyabiashara wadogo lakini pia kitatusaidia kupata mikopo na hata kutambulika popote tutakapohitaji kufanya biashara zetu”alisema Wille mmoja wa wajasiliamali

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.