BODI YA FILAMU YAENDELEA KUMPIGA “PINI” WEMA SEPETU

NA KAROLI VINSENT

Katibu mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fissoo amesema msanii wa filamu, Wema Sepetu hajafunguliwa kujihusisha na masuala ya uigizaji kama inavyovumishwa mitandaoni.

Bi Fisso ameyasema hayo  leo Jumatano Januari 9 Jijini Dar es Salaam,wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika ofisi za Bodi hiyo wakati wa kujadili Tasmini ya Tamasha la “KATAA MIHADARATI” lililofanyika katika viwanja vya Mburahati Barafu jijini Dar es Salaam. 

Amesema endapo msanii huyo atafunguliwa Baraza hilo litaitisha mkutano na waandishi wa habari kwa ajili ya kulieleza jambo hilo na si kama inavyoelezwa kwenye mitandano ya kijamii.

“Jamani naombeni muachane na stori za mitandaoni, Wema bado yupo kifungoni na endapo itatokea akaruhusiwa kujihusisha na masuala ya uigizaji bodi itaitisha mkutano na wandishi wa habari na kila mtu atajua,” ameeleza Joyce

Wema Sepetu amefungiwa na bodi hiyo Oktoba 26 mwaka jana kwa kosa la kusambaa mitandanoni kwa video yake chafu.

Katika hatua nyingine Baraza hilo limewakanya wasanii wanaotumia scene za kuonyesha madawa ya kulevya kwenye filamu zao, na kusema kuwa wawe makini sana na watumia scene hizo kwa lengo la kuelimisha na sio kuhamasisha matumizi ya madawa hayo.

Kwa Upande wao wasanii walioshiriki kwenye tamasha hilo wamesema limesaidia kutoa elimu kwa wananchi kujua madhara ya madawa ya kulevya.

Tamasha hilo lilikuwa na lengo la kutoa Elimu kuhusu madhara ya Dawa za Kulevya na liliratibiwa na Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Asasi ya Binti Filamu, pamoja na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Related posts

Leave a Comment

This site uses Akismet to reduce spam. Learn how your comment data is processed.