WATENDAJI SEGEREA WAKOSA UAMINIFU KWENYE FEDHA ZA SERIKALI

Na Heri Shaban MBUNGE wa Segerea Bonah Ladislaus(CCM) amewalalamikia Watendaji kwa kukosa uaminifu katika fedha za Serikali. Bonah aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara Kata ya Vingunguti Jimboni Segerea Dar es salaam uliofanyika katika kata hiyo hii leo. Aidha alisema Rais wa awamu ya tano John Magufuli ametoa shilingi bilioni 2 kwa ajili ya miundombinu ya afya hivyo ni vema watendaji kushirikiana kikamilifu katika kuzisimamia ili miradi ikatekelezeke sawa sawa na ilivyopangwa. “Serikali imeleta fedha za kutosha shilingi bilioni 2 Jimbo la Segerea changamoto kubwa iliyokuwepo tuna watendaji wasio waminifu…

Soma Zaidi >>

SIMBA YAWAOMBA RADHI MASHABIKI WAKE, KUELEKEA KWENYE MCHEZO DHIDI YA AL AHLY

Na Shabani Rapwi. Klabu ya Simba SC imewaomba radhi mashabiki wake kuelekea kwenye mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri utakaopigwa siku ya kesho Jumanne kwenye dimba la Taifa, Jijini Dar es Salaam, Saa 10:00 Jioni, kuwa tiketi za Platinum hazitakuwepo kwenye mchezo huo. Taarifa iliyotolewa hii leo Jumatatu na klabu hiyo kupitia mtandao wa Twitter kuwa tiketi za Platinum hazitakuwepo kwenye mchezo wa hapo kesho dhidi ya Al Ahly kama awali ilivyo tangazwa, huku walikuwa wameshanunua tiketi hizo watarudishiwa pesa zao na…

Soma Zaidi >>

MKUU WA MAJESHI NCHINI ATUA MKOANI NJOMBE

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Venance Mabeyo amefanya kikao na Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoani humo kuhusu matukio ya mauaji ya watoto yaliyoanza Novemba mwaka jana. Jenerali Mabeyo ambaye ni Mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama amesema kuwa yuko mkoani humo kwa ajili ya kufuatilia maendeleo ya zoezi la kukabiliana na matukio hayo kwakuwa vyombo vya ulinzi na usalama vinashirikiana. “Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vinafanya kazi kwa kushirikiana ikiwa ni pamoja na jeshi. Na mimi kama Mwenyekiti wa vyombo vyote vya ulinzi…

Soma Zaidi >>

WAMBURA AACHANA NA SOKA

Aliyekuwa Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura kupitia kwa Mwanasheria wake Emmanuel Muga imeelezwa kuwa ameridhia adhabu ya kufungiwa Maisha na TFF na FIFA.  Pamoja na hayo Wambura kupitia kwa mwanasheri wake Emmanuel Muga ametangaza kuwa kwa sasa kuanzia leo February 11 2019, anaachana rasmi na shughuli za mpira wa miguu, atabaki kama mtu wa kawaida tu. Hata hivyo Wambura pia ameamua kufuta kesi zote alizokuwa amezifungua kuhusiana na kupinga maamuzi ya kamati ya maadili ya TFF.

Soma Zaidi >>

SHEIKH PONDA ALAANI KITENDO CHA KUSITISHA UJENZI WA MSIKITI UDOM

Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania imeeleza kusikitishwa na kitendo kilichofanywa na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuamua kusitisha ujenzi wa msikiti uliokuwa ukijengwa katika chuo hicho. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Jumuiya hiyo Sheikh Issa Ponda alisema, mwaka 2016 uongozi wa chuo hicho uliwapatia ekari 10 baada ya kukubali ombi la jumuiya hiyo la kutaka kujenga msikiti huo. Ponda alisema, walianza kushughulikia vibali vya ujenzi katika mamlaka za chuo hicho na nje na walifanikiwa kuvipata vyote na mwaka jana waliwasilisha…

Soma Zaidi >>

RONALDO JUVENTUS KUMENOGA

Na Shabani Rapwi. Mshambuliaji wa klabu ya Juventus, Cristiano Ronaldo amezidi kuwa tishia ndani ya Juventus baada ya usiku wa jana kutupia goli moja katika ushindi wa 3-0 iliyopata timu yake ya Juventus dhidi ya Sassuola, Sami Khedira ndiyo alikuwa wa kwanza kufunga goli dakika ya 23′, huku dakika ya 70′ Ronaldo akapachika goli la pili na Emre Can dakika ya 86′ akapachika goli la tatu. Ronaldo anakuwa kinara wa ufungaji wa magoli katika Ligi Kuu ya Italia akiwa na magoli 18 akifuatiwa na Fabio Quagliarella katika nafasi ya pili…

Soma Zaidi >>

AZAM FC KUIVAA LIPULI HII LEO, SAMORA

Na Shabani Rapwi. Klabu ya Azam FC leo Jumatatu, Februari 11, 2019 itakuwa ugenini kukipiga dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) utakaofanyika Saa 10: 00 Jioni Uwanja wa Samora, Iringa. Azam FC leo itakosa huduma ya mlinda mlango wake namba moja Razak Abalora ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo dhidi ya Alliance. Timu hizo (Azam na Lipuli) zilikutana mara nne kwenye mechi za Ligi, katika mechi tatu zilizopita Azam FC ilishinda mara moja huku mechi mbili wakienda sare, mara ya mwisho kukutana kwenye uwanja…

Soma Zaidi >>