DC MSAFIRI ASHIRIKI IBADA YA MFUNGO KUOMBEA MKOA WA NJOMBE

Na.Amiri kilagalila Mkuu wa Wilaya ya Njombe Ruth Msafiri ameshiriki katika ibada ya kuhitimisha mfungo na Maombi yakuombea mkoa wa Njombe yaliyofanyika kwa wiki moja katika kanisa la Tanzania Assemblies of God T.A.G lililopo mtaa wa Melinze halmashauri ya mji wa Njombe mkoani humo. Akiwa katika ibada hiyo Msafiri amewataka wakristo mkoani Njombe kuendelea kuombea mkoa wa Njombe kutokana na matatizo ya mauaji ya watoto yaliyojitokeza hivi karibuni huku akiwataka kuto kusahau kuombea maswala ya uchumi na familia kwa ujumla. “Naendelea kuwategemea sana watu wa Mungu hatutafika bila kuinua uchumi…

Soma Zaidi >>

MANARA ATANGAZA MWAKA WA KUACHA KAZI SIMBA SC

Na Shabani Rapwi. Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Haji Manara ametangaza kuachana na klabu hiyo, baada ya kuwepo kwa tetesi ya kutemwa katika nafasi hiyo. Leo February 10, 2019 kupitia ukurasa wake wa Instagram, Manara amesema kuwa anafahamu kuwa mashabiki wengi wa Yanga hawapendi kumwona akiwepo Simba na siku atakayoondoka watafanya sherehe. “Kuna watu wa Yanga hamu yao nife kabisa, nawaumiza sana na siku mtakaposikia sipo kikazi Simba, mtafanya sherehe. Ila nikuhakikishie kuwa Mungu akinipa uhai nitaacha kazi Januari 2021 tena kwa hiari” alisema Manara.

Soma Zaidi >>

ULEVI WAMPONZA MUUGUZI ARUSHA,ASIMAMISHWA KAZI MWAKA MMOJA

Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru Arusha Martin Chama amesimamishwa kazi ya kutoa huduma za uuguzi na ukunga kwa mwaka mmoja na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania.  Uamuzi huo ulifikiwa katika kikao cha baraza hilo cha 196 baada ya kumtia hatiani kwa makosa mawili kati ya manne yaliyowasilishwa katika baraza hilo Septemba mwaka jana na aameanza kuitumikia adhabu hiyo tangu Februari 7, 2019.  Msajili wa Baraza la Uuguzi na Ukunga, Agnes Mtawa ameyataja makosa hayo kuwa ni kufika kazini akiwa amelewa na kutaka kuhatarisha usalama wa wagonjwa na ndugu zao…

Soma Zaidi >>

CHADEMA YATHIBITISHA AJALI YA MBUNGE WAKE

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimethibitisha Mbunge wake wa viti maalum kutokea Zanzibar, Zainab Mussa Bakari kupata ajali katika eneo la Dumila mkoani Morogoro alipokuwa akitokea Jijini Dodoma kuja Dar es salaam kufuatia kuahirishwa kwa vikao vya Bunge.  Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene akisema kuwa Mbunge huyo anatarajiwa kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi. “Mbunge wa CHADEMA (VM) Zanzibar, Bi. Zainab Mussa Bakari amepata ajali eneo la Dumila akitoka Dodoma leo, abiria wote…

Soma Zaidi >>

WIZARA YA AFYA MAENDELEO YA JAMII JINSIA WAZEE NA WATOTO YATOA TAMKO MAUAJI YA WATOTO NJOMBE

Na Amiri kilagalila Wizara ya afya maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto imewashukuru waganga wa tiba asili na tiba mbadala kwa ushirikiano katika afya za binaadamu na maendeleo ya jamii kwa ujumla huku serikali ikiendelea kutambua umuhimu wa fani hiyo muhimu na kuwataka waganga wa tiba asili kuendelea kutoa ushirikianao katika zoezi la uhakiki ili waweze kufanya kazi kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na wizara ya afya. Akizungumza na waganga wa tiba asili na tiba mbadala katika ukumbi wa halmashauri ya mji wa Njombe kwa niaba ya katibu mkuu wa…

Soma Zaidi >>

MTOTO ALIYEKATWA KOROMEO NJOMBE AFARIKI DUNIA

Njombe.  Meshack Myonga (4),  aliyenusurika  kuuawa baada ya kutekwa na kukatwa koromeo wilayani Njombe amefariki dunia mchana Jumamosi Februari 9, 2019 katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya. Desemba 23, 2018  mtoto huyo alitekwa na mtu asiyejulikana  akiwa  nyumbani kwa wazazi wake mtaa wa Mji Mwema wilayani Njombe, kisha kupelekwa msituni na kukatwa  koromeo kabla ya kuokolewa na kijana mmoja. Baada ya kuokolewa alipelekwa Hospitali ya Mkoa ya Kibena-Njombe na baadaye  kuhamishiwa hospitali ya rufaa Mbeya kwa matibabu zaidi. mama mzazi wa mtoto huyo, Rabia Mlelwa amesema, “Leo tumekwenda Hospitali…

Soma Zaidi >>

DKT. GWAJIMA AZITAKA TIMU ZA AFYA MIKOANI KUJITATHIMINI KIUTENDAJI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, anayeshughulikia afya, Dkt. Dorothy Gwajima, ameziagiza timu za Afya za Mikoa (Regional Health Management Team- RHMT) yote nchini, kujitathmini hali yao ya utendajikazi na kuona kama wanatija inayokubalika kwa taifa. Gwajima ameitoa kauli hiyo, alipokuwa akizungumza na timu ya Afya ya Mkoa wa Dodoma inayo ongozwa na James Kiologwe, Mganga Mkuu wa Mkoa huo wakati alipofanya ziara yake ya kwanza toka ateuliwe kushika wadhifa huo Januari 08,2019 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John…

Soma Zaidi >>