30 WASHIKILIWA MAUAJI YA WATOTO NJOMBE,KESI KUFIKISHWA MAHAKAMANI JUMATATU

Jeshi la Polisi Makao Makuu  Kitengo Maalum cha Kupambana na uhalifu kikiongozwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, kimeshirikina na Jeshi  la  Polisi Mkoa wa Njombe  kuendesha Operesheni  Maalum  ya kukabiliana na matukio ya mauaji ya watoto wadogo ambayo yamejitokeza mkoani humo, mpaka sasa watuhumiwa 30 wamekamatwa waliojihusisha na matukio hayo, Mkuu wa Operesheni Maalum za Jeshi la Polisi Naibu Kamishna Liberatus Sabas, amesema watuhumiwa hao ifikapo Jumatatu watakuwa wamefikishwa Mahakamani kukabiliana na tuhuma  za mauaji ya watoto, Aidha Naibu Kamishna  Sabas, amewataka…

Soma Zaidi >>

TOZO YA USHURU YA MCHUZI WA ZABIBU YAPUNGUZWA TOKA Tsh 3,315 MPAKA Tsh 450,MBUNGE DITOPILE AUNGURUMA

Hatimaye Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Mh Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli imesikia kilio cha wakulima wa Zabibu mkoani Dodoma cha ukosefu wa soko la zabibu kutokana na tozo kubwa ya ushuru wa bidhaa iliyokuwa ikitozwa Tsh 3,315 kwa lita kwa kinywaji kikali kitokanacho na mchuzi wa zabibu. Akichangia leo Bungeni katika Muswada wa Marekebisho ya Sheria Na.2/2019 Mbunge wa Viti Maalum Mh Mariam Ditopile ameishukuru serikali kwa kuleta mabadiliko hayo ya ushuru wa bidhaa na kupunguza tozo hiyo ambayo itawasaidia wakulima kupata soko la uhakika wa…

Soma Zaidi >>

MA DC NA RC MSINIPONZE,WAZIRI MKUCHIKA

Waziri  wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Mkuchika, amewataka baadhi ya wakuu wa Wilaya na mikoa nchini kuacha kuwaweka ndani watu kwa saa 48 wakati hakuna sheria inayowapa mamlaka hayo. Mkuchika amewataka wakuu hao wa Wilaya kuacha kutumia mabavu kwenye utendaji wao wa kazi wa kila siku kwa kuwa wakiendelea na tabia hiyo watakuwa wanahatarisha kazi yake ya uwaziri. Ameyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia na kueleza kuwa wakuu wa wilaya na mikoa wanapaswa kutumia busara katika kuwaweka ndani raia, ambapo Waziri Mkuchika amesisitiza Wakuu…

Soma Zaidi >>

KONDOMU ZAADIMIKA MJI WA MAKAMBAKO,MADIWANI WAMPA SIKU SABA MKURUGENZI KUSHUGHULIKIA

Na.Amiri kilagalila Baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji wa Makambako Mkoani Njombe limetaarifu kuadimika kwa Kondomu kote madukani halmashauri ya mji wa Makambako mkoani Njombe hivyo kuwaagiza wataalamu wake kutafuta mwarobaini kwani ni kikwazo katika jitihada za kukabiliana na maradhi ya Ukimwi. Wajumbe wa Baraza hilo wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo hanana mfikwa walisema licha ya kuadimika hata zile zinazopatikana zimekuwa zikiuzwa hadi Tsh 800 kwa pakiti kiwango ambacho wanakitaja kutokuwa rafiki kwao. Madiwani wa kata mbalimbali katika Halmashauri ya Mji wa makambako wamekutana katika kikao cha baraza…

Soma Zaidi >>