Mtoto anayekadiliwa kuwa umri wa miezi 7 amekutwa ameuawa kikatili na mwili wake kutelekezwa katika kontena la taka lililopo soko la kihesa manispaa ya iringa. Akizungumza na mtandao huu Mwenyekiti wa Mtaa wa Sokoni AGUSTINO KIMULIKE amesema kuwa dampo hilo linatumika na mitaa mitatu hivyo kama serikali wanaendelea kushirikiana na wananchi ili kumbaini mwanamke aliyefanya kitendo hicho. Kwa upande wake Mtendaji wa Kata ya Kihesa SWEBE DATUS amesema kuwa wananchi wanapaswa kukomesha matukio kama hayo kwani yanaleta sifa mbaya katika jamii. Nao baadhi ya wananchi wa Mtaa huo Kata ya…
Soma Zaidi >>Day: February 5, 2019
SERIKALI YAWAGEUKIA WAMILIKI WA MACHAPISHO
Serikali imetoa notisi ya siku 24 kwa wamiliki wa machapisho (magazeti na majarida) ambayo bado hayajahuisha leseni zao kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kuhakikisha wanahuisha leseni hizo hadi ifikapo Machi 21, 2019 vinginevyo hayataruhusiwa kuchapishwa. agizo hilo limetolewa na Mkurugenzi Idara ya Habari na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi leo Jijini Dodoma wakati akiongea na Wanahabari kuhusu utekelezaji wa masuala mbalimbali ya Serikali ikiwemo utekelezaji wa Sheria ya Huduma ya Habari. “Kwa mujibu wa Sheria mpya ya Huduma za Habari ya Mwaka…
Soma Zaidi >>CCM NJOMBE YAADHIMISHA MIAKA 42 YA CHAMA KWA KUPANDA CHAI
Na.Amiri kilagalila Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Njombe kimeungana na wananchi wa kijiji cha uliwa kata ya Ihungilo mkoani Njombe katika zoezi la upandaji wa miche ya chai ili kukuza na kuendeleza zao hilo la kimkakati mkoani humo pamoja na kuadhimisha miaka 42 ya chama hicho tangu kilipozaliwa. Akizungumza wakati wa zoezi hilo, katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Njombe HITLA BENJAMINI MSOLA amesema kuwa chama hicho kimeamua kufanya maadhimisho hayo kwa kushirikiana na wananchi wa kijiji hicho ili kuakisi ukombozi wa uchumi wa Tanzania. “kwanza tumefikisha miaka…
Soma Zaidi >>HABARI KUBWA KWENYE MAGAZETI YA TANZANIA LEO FEBRUARI 5,2019.
Fahamu yote yaliyojiri katika Magazeti ya Tanzania leo Februari 5, 2019. Hapa unapata habari zote zilizopewa uzito katika kurasa za mbele na kurasa za nyuma za habari za michezo na burudani.
Soma Zaidi >>